Fanya haya kuimarisha afya ya tumbo "gut health"
Je umekuwa ukipata matatizo ya tumbo mara kwa mara kama vile maumivu ya tumbo,tumbo kujaa gesi,kutapika ama kuharisha?elewa kwamba haupo peke yako ni wengi wanakutana na tatizo hilo kila siku kwa kutambua hilo sasa unapaswa kujua nini kinaweza kusaidia na kuimarisha afya yako ya umeng'enywaji kama ifuatavyo
1.Lishe tumbo lako vyakula Sahihi
"you are what you eat" kile unachokila kinaweza kuimarisha zaidi au kuharibu na kukuletea matatizo hivyo jitahidi kuhakikisha usafi wa kile unachokila na pia ubora wa kile unachokila tumboni kwako ipo jamii ya viumbe wanaojulikana kama "gut micribiome" hawa wanafanya kazi kwa kutegemea kile unachokula mazingira yao yakikaa vizuri utakuwa sawa ila yakivurugika kutokana na kile unachokila watageuka na kuanza kukushambulia hivyo jitahidi kula vyakula vyenye mimea kwa wingi kama vile mbogamboga na matunda na pia punguza matumizi ya pombe na vyakula vyenye sukari nyingi kwani vinaweza kuleta mvurugiko tumboni na kusababisha matatizo ya tumbo
2.Dhibiti msongo wa mawazo
Hivi unajua kwamba msongo wa mawazo unaweza ukaathiri utendaji kazi wa tumbo lako?Unapokuwa na msongo wa mawazo, mwili wako hutoa homoni ambazo zinaweza kupunguza usagaji chakula, na na hasa kwa watu wenye tatizo la vidonda vya tumbo kudhibiti msongo wa mawazo ni muhimu sana kuhakikisha kwamba hali zao haziwi mbaya zaidi
3.Zingatia kunywa maji ya kutosha
Maji ni muhimu sana hasa katika kusaidia umeng'enywaji wa chakula na kuweka mambo sawa tumboni kwani husaidia katika kuvunja chakula, kufyonza virutubisho, na kuzuia kuvimbiwa. Hivyo lenga kunywa maji mengi siku nzima, hasa kabla ya milo.ili kupata faida zake zaidi na kujiepusha na matatizo yasiyo ya lazima
4.Zingatia kufanya mazoezi
Shughuli za kawaida za kimwili kama kutembea ni muhimu kwa afya ya tumbo. Mazoezi husaidia kuchochea mfumo wako wa usagaji chakula, hivyo huimarisha mchakato mzima wa umeng'enywaji na pia kumbuka kwamba huna haja ya kukimbia mbio ndefu au kufanya mazoezi magumu sana kwani hata kutembea kila siku au kunyoosha mwili kidogo tu kunaweza kuleta mabadiliko makubwa.
5.Angalia kama unakutana na kile kinachoitwa "food intolerance"
kama unaiona dalili moja wapo kati ya hizi
kuharisha,tumbo kujaa gesi,kutapika,acid reflux,uchovu,maumivu ya tumbo jitahidi kuondoa baadhi ya vyakula ambavyo vinakufanya uwe na mojawapo ya dalili hizi
6.Punguza ulaji wa vitu vyenye sukari nyingi
Zingatia mlo wenye vyakula vyenye nyuzi nyuzi "fibers" kwa wingi na pia ulaji wa mbogamboga na matunda za kutosha humo upata virutubisho viitwavyo polyphenols ambavyo pia vipo katika vitu kama vile kahawa
Join the conversation