Shadow sentences
Kila mara tunapoambiwa namna ya kuimarisha afya zetu za akili jambo moja ni tunaambiwa kuwa muwazi mara nyingi tunajaribu ila huwa tunatumia zile ambazo huitwa "shadow sentences
Shadow sentences ni lugha ambayo tunaitumia tukidhani kwamba wenzetu watatuelewa sana unaongea kitu ambacho unahisi mwenzako atakielewa na kukasirika wasipokuelewa inakuwa kama hujaomba chochote unatumaini kwamba utaeleweka ila hutumii lugha ya moja kwa moja
Hatari yake ni kwamba ni hafifu Hazina uwazi, na kufanya iwe vigumu kuelewa kile ambacho mzungumzaji anataka kwani Hudokeza mahitaji badala ya kuyasema waziwazi.
Hapa ni baadhi ya mifano
| Hitaji halisi | Sentensi kivuli/shadow statement | Tatizo katika mawasiliano |
Umefika kwa rafiki yako na hukupata muda wa kula kabla ya kufika pale unatamani akupe chochote kitu unataka useme "hey man sijala kabla ya kufika hapa unaweza ukanisaidia chochote ambacho naweza kula?" | Ila unasema "yaani leo ningekula sana ila sijala" | Mwenzako hataelewa kwamba kweli unahitaji chakula |
Umekuwa katika mahusiano na mtu na hamjaonana kwa muda unauliza anafanyaje anasema yupo na rafiki zake Unahitaji kusema "Hatujaonana kwa muda sasa nahitaji kukuona mapema na inanipa wasiwasi hutumii muda pamoja na mimi" | Ooh ni usiku wa muhimu tena kuwaona rafiki zako naonauna muda mwingi sana wa kukaa nao | Umejitahidi kuongea lakini hujaweka wazi nini unakitaka |
Umeongea na rafiki yako kwa muda na unaona muda umeenda na unahitaji kumaliza maongezi uendelee na kazi zingine | Unasema "Muda umeenda!! " | Rafiki yako anaweza fikiria kuwa wewe unataja tu muda hataelewa unachokitaka hasa |
Upo Dinner na mtu alafu kila mara yupo bize na simu unahitaji kusema "Hey ningependa tuongee na najua upo bize ila inanifanya nijiskie vizuri zaidi ukiongea na mimi badala a kuwa bize na simu tu unaweza kuacha simu hadi baadae" | Ila unasema "mhhh huenda ni mesej ya muhimu kweli ambayo unahitaji kuijibu muda huu" | Hawezi akaelewa kwamba unahitaji nini hasa |
Nahitaji kubadilisha hali hii ya sasa au jambo hili | Natamani mambo yangekuwa tofauti | Anayekusikiliza hatojua unachotaka hasa |
Kuna jambo halipo sawa unaongea na rafiki yako unajua kwamba unahitaji msaada wa kihisia "emotional support | "Nipo sawa." (huku haupo sawa kabisa) | Anayekuskiliza anaweza akahisi upo sawa kwani hujaweka wazi kuwa unahitaji msaada |
Matumizi ya sentensi kivuli yanaweza kusababisha:
Kutoelewana: Msikilizaji huenda asielewe kwa usahihi hitaji la mzungumzaji.
Kuchanganyikiwa: Mzungumzaji anaweza kuhisi mahitaji yake hayakidhiwi, huku msikilizaji akihisi kuchanganyikiwa au kutokuwa na uwezo wa kusaidia
Kinyongo: Baada ya muda, mtindo wa mawasiliano usio wa moja kwa moja unaweza kuleta kinyongo na msuguano katika uhusiano kwani unahisi kwamba unaongea na hupati msaada
Ufanisi mdogo: Inaweza kuchukua muda mrefu kupata mahitaji, kwani pande zote zinapaswa kupitia lugha isiyo wazi
Join the conversation