Sio Nzuri na Sio Mbaya pia

Sio Nzuri na Sio Mbaya pia 

Kulikuwa na mkulima na farasi aliyemsaidia katika kilimo. Wanakijiji walimwambia mkulima kila mara jinsi alivyokuwa na bahati ya kuwa na farasi mzuri sana. 

"Labda," alijibu mkulima

Siku moja, farasi alikimbia. Wanakijiji walikuja kwa mkulima kutoa pole zao. "Hiyo ni mbaya sana," wanakijiji walisema. 

"Labda," mkulima alijibu.

Siku chache baadaye, farasi alirudi nyumbani na farasi kumi  wa porini. "Hiyo ni nzuri, sivyo?" wanakijiji walisema. 

"Labda," mkulima alijibu tena.

Siku iliyofuata, mtoto wa mkulima alikuwa amepanda mmoja wa farasi hao alipomwangusha na kuvunja mguu. Wanakijiji walifika kutoa masikitiko yao. "Hiyo ni mbaya sana," walisema

 "Labda," mkulima alijibu.

Afisa wa jeshi alifika kijijini siku iliyofuata, akiwaajiri vijana wenye nguvu kwa ajili ya vita. Mtoto wa mkulima, akiwa na mguu wake uliovunjika, aliachwa. Wanakijiji walifurahi, "Mtoto wako ameokolewa. Ni bahati nzuri iliyoje!" 

Mkulima alitabasamu akasema. "Labda."

Kuna aina nyingi za kufikiri ambazo ni hatari kwa afya yako ya akili zinaitwa 'distorted thinking" leo itaelezewa moja hapa inayojulikana kama "All-or-Nothing Thinking" au "binary thinking"  Nzuri au mbaya ,kushida/kushindwa aina hii ya mawazo japo inafanya kazi kwenye baadhi ya maeneo inaweza kukuumiza katika mambo mengine

 Ili uimarishe afya yako ya akili unahitaji kubadili namna unavyofikiria mambo mbalimbali kila kitu kinaweza ni kizuri au kibaya kwa wakati huo Kuna mambo mengi mabaya yamekutokea, na bado una furaha sasa kwamba yamekutokea kwani yalibadilisha mwelekeo wa maisha yako

kwa kujua hilo utakuwa na utulivu ndani yako 



Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...