Mtazamo Unaweza kuimarisha afya yako ya akili
Mara nyingi utaskia kuhusu “mentally strong people “ watu wawili wanapatwa na tatizo fulani ila mmoja analishinda mwingine anabakia hapo hapo nini kinawatofautisha? Dakika mbili zijazo utaelewa nini hasa kinaleta utofauti…
Lakini ukichunguza kwa undani, kuna mtazamo mmoja ambao umeonekana kwa kila mmoja wa watu hawa:
Wote wana Eneo la Ndani la Udhibiti Yaani internal locus of control
Eneo la Udhibiti ni dhana ya kisaikolojia iliyoanzishwa kwanza na Julian Rotter mnamo 1954 ambayo inaelezea jinsi watu wanavyotambua sababu za matukio katika maisha yao.
Wale walio na Eneo la Nje la Udhibiti “external locus of control “ huamini kwamba matokeo yao huamuliwa na nguvu zilizo nje ya udhibiti wao.
Wale walio na Eneo la Ndani la Udhibiti yaani internal locus of control huamini wana udhibiti juu ya matokeo yao kupitia juhudi, umakini, na mtazamo.
Inaonekana, mtazamo huu mmoja—unaweza kutuambia kwanini baadhi ya watu huishia kukosa matumaini baada ya tatizo fulani na wengine kuinuka na kuendelea mbele
Eneo la Nje la Udhibiti limehusishwa na hali ya kukata tamaa , mtazamo wa mwathirika yaani victimhood mentality na kuepuka changamoto “escapisim”
Eneo la Ndani la Udhibiti limehusishwa na ustahimilivu mkubwa, afya bora ya akili, viwango vya chini vya stress ,mafanikio ya juu, na utatuzi wa matatizo
Uliza maswali haya ili kurejesha Eneo lako la Ndani la Udhibiti labda unapitia changamoto fulani jiulize haya
- Sehemu gani ya hali hii iko ndani ya udhibiti wangu?
- Ni hatua gani ndogo ninaweza kuchukua sasa hivi?
- Ikiwa rafiki yangu wa karibu angepata changamoto hili, ningempa ushauri gani?
Join the conversation