Elewa mitazamo na dhana potofu kuhusu uume
Kuna mitazamo mingi na dhana potofu kuhusu ukubwa wa uume, mara nyingi zikiendeshwa na shinikizo la kijamii, upotoshwaji, na maonyesho mbalimbali katika matangazo na ponografia. Dhana hizi zinaweza kusababisha wasiwasi na aibu na matatizo mengine ya afya ya akili,na mara nyingi wengi wao utakuta wapo sawa kabisa na hawana tatizo lolote mitazamo hii inaweza kuwaweka katika hali ya kujiona kuwa una tatizo wakati huenda upo sawa kabisa hii hapa ni baadhi ya mitazamo na dhana potofu kuhusu uume na ukubwa wa uume
-
Ukubwa ndio deal: Niseme kwamba hii ndio iliyoenea zaidi na inayozidi kuenea zaidi na wengi wamekuwa na wasiwasi hata kufikia hatua ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kutafuta dawa Ingawa baadhi ya watu wanaweza kupenda size kubwa, tafiti zinaonyesha kwamba watu wengi wanaridhika na ukubwa wa uume wa mwenza wao bila kujali kipimo. ni muhimu kuelewa kwamba ni mambo kama Utendaji "functional", ukaribu"intimacy", na uhusiano wa kihisia"emotional connection" ni mambo muhimu zaidi katika kuleta kuridhika kimapenzi na sio ukubwa wa uume na zaidi hali yako ya kisaikolojia pia ni muhimu sana katika ufanisi kwenye tendo
-
Kuna "ukubwa sahihi" au "bora": Ni muhimu kuelewa kwamba hakuna "ukubwa sahihi" mmoja. Ukubwa wa uume unatofautiana sana baina ya watu mbalimbali na hatufanani hivyo inaweza kutokea kwamba kile unachochukulia kuwa ni "kawaida" ni kiwango kikubwa. Kuzingatia kipimo maalum kama bora sio kweli na kunaleta shinikizo na mahangaiko mengi ambayo kiukweli sio ya lazima.
-
Ukubwa wa uume huamua uwezo wa kijinsia ama ushujaa: Mtazamo huu nao hauna ukweli ndani yake japo unazidi kuenea kwa wingi kimya kimya kwani. Ujuzi wa kijinsia, mawasiliano, na ukaribu wa kihisia"intimacy" ni muhimu zaidi na yenye kuridhisha kuliko ukubwa wa uume. Ukubwa hauna uhusiano na uwezo wa mwanaume kumfurahisha mwenza wake hivyo usidanganyike kwani huenda anayesukuma mtazamo huu kwako kuna kitu anataka kukuuzia
-
Wanawake wanajali zaidi kuhusu ukubwa wa uume: mtazamo huu nao unazidi kuenea na kuleta hali ya kutokutulia kisaikolojia kwa wanaume wengi ukweli ni kwamba ingawa baadhi wanaweza kuwa wanajali zaidi kuhusu ukubwa elewa kwamba wanawake wengi katika uhusiano wa kimapenzi kipaumbele cha muhimu zadi kwao ni mambo mengine kama vile uhusiano wa kihisia, mawasiliano, na ujuzi wa kijinsia kwa ujumla(emotional connection, communication, and overall sexual skill).Ni mara chache kwamba ukubwa wa uume mara chache huwa kipaumbele kwao
-
Kuna njia za kuongeza ukubwa: Ni muhimu kuelewa kwamba njia nyingi zinazotangazwa na vchochote kinachoahidi kuongeza ukubwa wa uume hazifanyi kazi na zinaweza kuwa hatari. Hakuna kidonge "magic pill" au zoezi la kuongeza ukubwa wa uume kwa kiasi kikubwa
Elewa kwamba pornografia inaweza kukusababisha kuwa na mitazamo ya aina hii kwani nyingi huonyesha viwango vya mwili na uwezo mkubwa katika tendo pamoja na ukubwa wa uume.kama umekuwa ukiangalia na unahitaji kujiondoa ni vizuri kutafuta msaada pia ushujaa wa mwanaume hauji kwa kuwa na uume hivyo usidanganyike na kujiskia vibaya upo sawa kabisa na hauna tatizo
MWISHO: Ni muhimu kukumbuka kwamba kujikubali na kuwa na mtazamo chanya wa mwili wako ni muhimu. Zingatia afya yako kwa ujumla,na mahusiano badala ya kuhangaika mawazo na mitazamo yasiyo ya kweli . na kama una wasiwasi kuhusu ukubwa wa uume ama tatizo lolote katika afya yako ya uzazi jaribu kuzungumza na daktari/mtaalamu wa afya kwani kunaweza kukupa taarifa sahihi kuhusu afya yako na nini cha kufanya.
.png)
Join the conversation