Anzisha mitindo ya kiafya leo


 UKIJENGA TABIA ZAKO LEO ZITAKUJENGA KESHO

Je unahitaji kuanza tabia ya kufanya mazoezi? unahitaji kupungua uzito? unahitaji kuwa na afya njema ? yote hayo yanawezekana ukielewa namna ambavyo unaweza kujenga tabia zitakazokusaidia kufikia malengo hayo tabia zinanguvu kwani."We are what we repeatedly do" sisi ni ujumla wa yale ambayo tunayarudia kila mara na hasa kipindi hiki ambacho kuna ongezeko kubwa la magonjwa sugu tunahitaji kutengeneza misingi mizuri ya tabia za kiafya na nimeweka "apps" zitakazokusaidia katika mchakato huu 

Mara nyingi watu huchukulia poa nguvu ya mabadiliko madogo lakini wewe ni shahidi wa namna ambavyo mambo madogo unayofanya kila siku yanavyoweza kukusaidia 

#

 Hapa nimeeleza mambo kadhaa toka katika kitabu cha "atomic habits" ambayo yanaweza yakakusaidia kubadili tabia na kuanzisha zile unazozihitaji


Nguvu ya Kuongezeka Kidogo Kidogo (Kanuni ya 1%):  


James Clear anasema kwamba ukiweza kujiboresha kwa asilimia 1 tu kila siku katika jambo fulani mara nyingi inaonekana sio muhimu sana/haina matokeo ila baada ya muda mrefu, matokeo ya mkusanyiko ni ya kushangaza angalia kwa mfano Kujiboresha kwa asilimia 1 kila siku hupelekea kuwa bora mara 37 mwishoni mwa mwaka na kinyume chake, kupungua kwa asilimia 1 kila siku hupelekea karibu sifuri. Hii inaonyesha kwamba tabia ndogo ndogo ni kama chembe ndogo "atoms" za matokeo makubwa.


chukulia kuna barafu juu ya meza "ice cube" ukaanza kuongeza joto taratibu kwa digree 1 moja kila wakati 20-21-22-23-24-unaona bado barafu haiyeyuki unavyoendelea kuongeza zaidi unashangaa imeyeyuka badiliko dogo limeleta matokeo makubwa

changamoto kubwa ni kwamba mara nyingi matokeo hayaonekani mapema mwanzoni utakutana na kile kinachoitwa "the valley of disappointment" pale ambapo umeamua kuanza ila huoni mabadiliko labda umekuwa ukifanya mazoezi kwa mwezi mmoja sasa na ni kama huoni matokeo elewa kwamba juhudi zako sio kwamba zimepotea bure zinaendelea kuunganika na kuwa kubwa zaidi kuleta matokeo makubwa.

Mabadiliko yanachukua muda hivyo kuwa mvumilivu 

Kama unataka kujua labda hali yako ya kiafya itakuwaje angalia unayoyafanya kila siku yanaendelea kujikusanya na kwa muda mrefu yanakupa matokeo.

Kuvunja Ukuta wa Uwezo Uliofichika: Mara nyingi, tunapoanza kufanya tabia mpya,labda umejiwekea lengo la kupungua uzito mara nyingi unaweza usione matokeo ya haraka "inakatisha tamaa". ila James Clear anaelezea kipindi hiki  unapswa kuelewa kwamba juhudi ndogo ndogo zinazoendelea zinajenga nguvu kimya kimya na hatimaye, utavunja ukuta huu na kuona maendeleo makubwa

Elewa umuhimu wa tabia zinazotokana na utambulisho "indentity change": James clear anasisitiza kwamba hamisha mtazamo kutoka kwa tabia zinazolenga matokeo (mfano, "Ninataka kupunguza uzito") kuwa tabia zinazotokana na utambulisho (mfano, "Ninataka kuwa mtu mwenye afya"). Tabia zako zinapoungamana na utambulisho wako hii inashangaza kwa sababu mara nyingi tunafikiria kuhusu malengo tunayoyataka kwa muda labda "kupungua uzito,au kujengwa mwili" na si kuhusu tunataka kuwa nani. lengo liwe ni mtu unayetaka kuwa kwamba unataka kuwa mwenye afya kisha mienendo yako iendane na mtu unayetaka kuwa

Sheria Nne za Mabadiliko ya Tabia:

  1. Ifanye Ionekane Wazi (Ishara): Hapa sana ni kuhusu wewe kuunda vichocheo wazi kwa tabia ambazo unazitaka. jaribu moja wapo kati ya hizi 
      • Mazoezi: Andaa nguo zako za mazoezi na viatu karibu na kitanda chako usiku kabla.kwa kufanya hivi utarahisisha kuanzisha tabia hiyo
      • Kula vizuri Kiafya: Weka matunda jikoni/sehemu ambayo itakuwa rahisi kuyaona na ficha/ondoa vyakula ambavyo hutaki kuvila hasa vyenye sukari nyingi ili iwe vigumu kufikia.
      • Unywaji wa Maji: Weka chupa ya maji kwenye kwenye gari lako/karibu na meza unayofanyia kazi
      • Kuunganisha tabia"habit stalking": hapa unaunganisha tabia unayoitaka na ile ambayo tayari unaifanya kila siku mfano baada ya kupiga mswaki, nitakunywa glasi ya maji. baada ya kula nitatembea kwa dakika 10,baada ya kupiga mswaki nitapiga pushup 10
  2. Ifanye Ivutie : Hapa fanya tabia unazozitaka zivutie kwa kuziunganisha na vitu unavyovifurahia.
    • Mifano:
      • Mazoezi: Sikiliza nyimbo/podcast unazozipenda wakati unafanya mazoezi.
      • Ungana na watu wengine:hapa tafuta rafiki wa kufanya naye mazoezi ili kufanya mazoezi kuwa shughuli ya pamoja
  3. Ifanye Iwe Rahisi : Ili tabia unayoitaka iwe rahisi jitahidi kupunguza msuguano ama ugumu unaokuzuia kuanza tabia hizo
    • Mifano:
      • Utaratibu wa Mazoezi: Anza na mazoezi madogo na yanayoweza ambayo ni marahisi kama vile tembea kwa dakika 10 taratibu utaweza kuanza mazoezi mengine
      • Elewa kanuni ya dakika mbili: Unataka kuanza tabia gani ya kiafya? ni mazoezi? jaribu kuianza kwa dakika mbili mfano kuruka kamba kwa dakika mbili isitumie muda mrefu
  4. Ifanye Iridhishe : Imarisha tabia zako zenye afya ikupe kuridhika haraka 
    • Mifano:
      • Baada ya Mazoezi: Jizawadie smoothie/juice au kujinunulia nguo mpya za mazoezi
      • Fuatilia Maendeleo yako: Tumia program maalum kufuatilia tabia au jarida kurekodi maendeleo yako na kusherehekea mafanikio yako. tumia app kama vile Habitica,Loop Habit Tracker,TickTick
      • Tafuta "accountability partner" kwa uwajibikaji: Shiriki malengo na rafiki labda umepanga kuanza kufanya mazoezi wajulishe ili wakuwajibishe 

Kila mmoja wetu ana tabia moja au zaidi asiyoipenda na anatamani kuiacha na huenda umeangaika muda mrefu huenda mbinu unayoitumia ndio haijaweza kukuletea mafanikio elewa namna  ambavyo mtu aliyehangaika kwa miaka 40 kuacha kuvuta sigara alivyofanikiwa kuiacha tabia hiyo zingatia haya unapoanzisha tabia mpya

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...