Zingatia haya ili kubadili tabia usizozipenda
Je kuna tabia ambayo umeteseka kuibadilisha au umekuwa ukihangaika kuanza tabia ambazo ni nzuri kwako ipo wazi kwamba maisha yetu ni mjumuiko wa yale tunayofanya kila siku
1.Itumie kijanja "habit stalking" "Kuunganisha tabia"
Miaka kadhaa iliyopita kwa kujua umuhimu wake kwa afya yangu ya akili na viwango vyangu kiroho nilikuwa natamani sana kuwa na tabia ya kusali nilitamani nipate muda wa kukaa peke yangu kwa utulivu na kusali lakini kila siku nilijikuta nakosa muda siku moja nikasoma mahali nikasema niijaribu kwenye tabia hii ya kuomba ambayo nilitaka kuianza ilikuwa ni kanuni ndogo na rahisi Mbinu hii ni rahisi sana inatumika kuanzisha tabia mpya kwa kuziambatanisha baada ya zile ambazo tumeshazizoea
BAADA YA {tabia ya sasa ,ile ambayo umeshaizoea na unaifanya
kila siku} NITA {tabia ambayo unaihitaji }
kwa wakati huo nilikuwa na tabia ya kufanya mazoezi kila jioni nikaona nianzie hapo kuiweka tabia yangu mpya ya kusali
Kwamba “BAADA YA {KUTOKA MAZOEZINI} NITA {NITASALI KWA
DAKIKA KADHAA}”
Unajua kilitokea nini ? nilijikuta Napata muda wa kuomba kila siku na imekuwa katika ratiba yangu ya kila siku hiyo ndio namna habit stalking inaweza kukusaidia
Unaanza na tabia gani leo?
hapo mbele utaelewa mbinu ambayo baba aliyehangaika kwa miaka 40 akitamani kuacha kuvuta sigara bila mafanikio aliitumia na kufanikiwa endelea kusoma
2.Usipigane na tabia usiyoitaka
Mara ngapi umejaribu kupigana kwa nguvu na tabia usiyoitaka na unajikuta bado inajirudia na na unajilaumu?
Wakati nasoma kuhusu tabia na namna ya kuzibadili nilikutana na kisa kimoja cha baba ambaye alikuwa na tabia ya kuvuta sigara ila mara zote alikuwa akivuta sigara katika gari lake ili wanawe wasijue kwa miaka 40 ni tabia ambayo alitamani kuiacha bila mafanikio alijaribu kuiacha bila mafanikio kila mara kama wengi wetu alijikuta akirudia tabia hiyo japo alikuwa haipendi siku moja alipata kujifunza namna tabia zinavyofanya kazi alifanya hivi katika boksi la sigara aliondoa sigara zote akaweka pipi hivyo kila alipoingia kwenye gari alizikuta na badala ya kuvuta sigara alifikia kitu ambacho kina madhara madogo ukilinganisha na sigara
Mara nyingi tunapotaka kuacha tabia fulani tusiyoitaka tunatumia nguvu nyingi kupambana nazo Ikiwa unataka kuondokana na tabia, usipigane nayo. Fanya kazi na mzunguko wako wa tabia na utumie hatua chanya kuibadilisha.Elewa kwamba huwezi kuziondoa tabia kabisa unachokifanya ni kubadili hivyo badala ya kupigana nayo elewa mzunguko wa tabia yako na ubadilishe baadhi ya vitu katika mzunguko huo
Usishughulikie zaidi ya tabia moja mbaya kwa wakati mmoja; kadiri unavyojaribu kubadilisha vitu vingi, ndivyo nafasi zako za kubadilisha kitu chochote zinavyopungua. Wakati unaunda tabia yako mpya, hakikisha unajijali na kupata usingizi mwingi iwezekanavyo.
Hivi unaelewa ajabu ya mambo madogo unayofanya kila siku?elewa namna mambo madogo unayofanya kila siku yanaweza kuleta matokeo makubwa kwenye afya yako
3.Elewa nguvu ya mambo madogo
kuna nguvu kubwa sana katika mambo madogo madogo tunayoyafanya kila siku inaitwa "compaund effect"
"wewe ni ujumla wa yale unayofanya kila siku"
fikiria hii afya yako ya kinywa na meno kwa asilimia kubwa imetokana na dakika 2-5 unazozitumia kuswaki miaka mingi iliyopita mpaka leo kama ni dakika mbili zimekuwa na faida nyingi kwa muda mrefu dakika 30 za mzoezi kila siku zitakuwa na faida nyingi sana pia ,kutembea dakika 10 baada ya kula kutakuwa na msaada mkubwa kwa afya yako pia jaribu kuanzia leo
Jaribu Kuwa bora kwa 1% kila siku
Nadhani unaijua ile methali, "Pole pole ndio mwendo" na sidhani kama pia ulikosa kusikia hadithi kuhusu kobe na sungura si ndio? mimi ni kobe. Nipe muda wa kutosha, na nitamshinda karibu mtu yeyote, wakati wowote, katika mashindano yoyote. Kwa nini? Sio kwa sababu mimi ndiye bora au mwenye akili zaidi au mwenye kasi zaidi. Nitashinda kwa sababu ya tabia chanya nilizojijengea, Mimi ndiye muumini mkubwa zaidi duniani wa uthabiti. Mimi ni ushahidi hai kwamba ndio ufunguo mkuu wa mafanikio, lakini ni mojawapo ya vikwazo vikubwa kwa watu wanaopambana kufikia" asema Kobe
4.Unahitaji sababu yenye nguvu ya kuacha/kuanza tabia hiyo
He who has a why to live for can bear almost any how
Kwanini unataka kuiacha tabia hiyo? au kwanini unataka kuanza tabia hiyo? kwa kuelewa hiko itakusukuma na kukupa nguvu ya kuacha/kuanza mfano kwanini uanze kufanya mazoezi na kuzingatia kula milo mizuri ya kiafya ni kwa sababu ya afya yako afya ni kama meza ambayo kila kitu kwenye maisha yako kinakaa juu ya meza hiyo unaweza ukaondoa chochote juu ya meza hiyo wala haitakuwa na madhara sana ila ukiondoa meza kila kitu kinaharibika
tafuta sababu ya nguvu wakati mwingine tunashidwa kuanzisha tabia nzuri/kuacha zile ambazo hatuzihitaji sababu tumekosa sababu yenye nguvu
mara nyingi tunahitaji kupoteza kitu ili tunadilike au tukio baya litokee ili tubadilike unahitaji kuambiwa kwamba unaumwa na umebakiza miezi kadhaa ili uiage dunua hapo utaona mtu kaanza kufanya mazoezi na kula vizuri ,kwanini usubiri hadi ifike hatua hiyo? wengi tunasubiri tuambiwe kwamba sasa una ugonjwa wa kisukari ndipo uanze kula vizuri na kufanya mazoezi kwanini usubiri hadi ifikie hatua hiyo? wakati unaweza ukaanza leo?
5.Tengeneza utambulisho juu ya tabia unayoitaka
Utambulisho una nguvu na kuna uwezekano mkubwa wa kufanya kitu ambacho kinaendana na utambulisho wako linapokuja swala la kuwa mwenye afya unahitaji utambulisho wa kuwa mwenye afya kwamba “wewe ni mwenye afya” kwa utambulisho huo utaambatanisha tabia zinazoendana na utambulisho wako kwamba mtu mwenye afya huwa anafanya nini? Mwenye afya huwa anafanya mazoezi,mwenye afya anakula chakula kizuri itakurahisishia sana kuanza tabia unazozitaka na kuacha zile ambazo huzipendi kwani haziendani na utambulisho wako
kuelewa kwamba "wewe ni mtu wa kufanya mazoezi kila siku" utambulisho huo utakusukuma kufanya tabia ambazo zinaendana na utambulisho wako
tabia za kila siku ni picha ya utambulisho wako mfano unapopanga chumba chako vizuri ni picha ya mtu mwenye mipangilio mizuri "organized person" kama unakwenda kufanya mazoezi kila mara ni utambulisho kwamba wewe ni mtu unayependa mazoezi na kujali afya yako tabia ni kishiria cha utambulisho wako badili utambulisho badili tabia
6.Kama unataka kuacha tabia ,lala
Moja ya mambo yenye ufanisi zaidi unayoweza kufanya pia ni rahisi zaidi: pata usingizi mzuri wa usiku. Chochote kile unachojaribu kuboresha
kama unajaribu kuwa na umbo bora"good shape", kupata usingizi wa kutosha huboresha kasi yakozaidi,labda unajaribu kupunguza uzito au kula kiafya zaidi, ukosefu wa usingizi utapunguza leptin, homoni inayopa mwili wako ishara kwamba umeshiba. Pia husababisha ongezeko la ghrelin inayojulikana kama ‘homoni ya njaa’, ambayo husababisha kuongezeka kwa hamu ya kula na uhifadhi wa mafuta, na inaweza kusababisha kufanya chaguzi za vyakula visivyo na afya.
Kwa hivyo, ikiwa unataka kuvunja tabia za zamani na kuunda mpya, sahau vidokezo/mbinu ngumu, na uzingatie mambo ya msingi – utafanikiwa ikiwa unajisikia vizuri, ikiwa hauna msongo wa mawazo kupita kiasi na ikiwa umepata usingizi mzuri wa usiku.usingizi ni muhimu

Join the conversation