Kwanini baadhi ya watu wana kumbukumbu zaidi?
Kesi ya Kumbukumbu Bora Zaidi
Huenda umewahi kutamani kuwa na kumbukumbu kamilifu ,kumbukumbu nzuri ,au namna ambavyo ungejiskia ukiweza kukumbuka mambo mengi yaliyotokea kwenye maisha yako ,wengi wanatamani uwezo huo au pengine unatamani uweze kukumbuka kila kitu ni vizuri kuwa makini na unachokitamani ,Baada ya kusoma barua iliyotumwa kwa Dk. James McGaugh hapa chini, unaweza kubadili mawazo yako.
Mpendwa Dk. McGaugh
Nimeketi hapa nikijaribu kutafakari wapi nianzie kueleza kwanini nakuandikia wewe na mwenzako barua hii, natumai kwa namna fulani mnaweza kunisaidia.Nina umri wa miaka thelathini na nne. Ninaweza kuchagua tarehe, kati ya 1974 na leo, na kukuambia ilikuwa siku gani, nilikuwa nikifanya nini siku hiyo na kama tukio lolote la umuhimu mkubwa lilitokea siku hiyo; naweza kukueleza pia. Siangalii kalenda kabla na wala sisomi shajara zangu za miaka ishirini na minne pia. Kila ninapoona tarehe kwenye televisheni (au mahali pengine popote kwa jambo hilo) akilini mwangu narudi kwenye tarehe hiyo na kukumbuka nilikuwa wapi, nilikuwa nikiendelea na nini, ilikuwa siku gani na kadhalika na kadhalika na kadhalika .. Haiwezekani kuzuia, haiwezi kudhibitiwa na inachosha sana mimi....Wengi wamekiita kipaji lakini mimi nakiita mzigo. Ninaendesha maisha yangu yote kichwani mwangu kila siku na inanichanganya sana!!!"
Chanzo:(McGaugh, 2017).
Uwezo wa kukumbuka namna hii unajulikana kama "highly Superior Autobiographical Memory (HSAM)" barua hiyo apo juu alitumiwa Dr James McGaugh na mtu ambaye alikuwa na uwezo huo
Kikawaida mambo yasiyo ya umuhimu husahaulika hasa ambayo hayana msaada kwako huko mbeleni hivyo Mara nyingine kusahau inaweza kuwa na manufaa kwani baadhi ya mambo hayana umuhimu wa kukumbukwa na mengine yanaweza kuleta madhara yanapoendelea kuzunguka akilini mwako
Kupoteza kumbukumbu kunapokuwa ugonjwa
Uwezo wa kukumbuka unaonekana kupungua kadiri umri unavyozidi kuongezeka ,ni kawaida lakini yapo magonjwa ambayo yanajulikana kuathiri kumbukumbu kama vile dementia ambapo mtu huanza kusahau kumbukumbu za muhimu za maisha yake na kupunguza ubora wa maisha ya mtu
Unachoweza kukifanya kuimarisha kumbukumbu?
Mazoezi yameonekana kwa kiwango kikubwa kuimarisha uwezo wa kukumbuka na pia kupunguza hatari ya matatizo ya kumbukumbu hasa "Dementia"
Jitahidi kuthibiti stress ,stress imeonekana kuathiri maeneo ya ubongo yanayohusika na kumbukumbu
1 comment
...but naswali kuhusu attachment style