Faida za mwanga wa jua asubuhi

Kupata mwanga wa jua asubuhi na mapema huwa na faida nyingi za kiafya, zikiathiri afya ya mwili na akili mood na siku yako kwa ujumla chini hapa ni faida hizo

Faida za Kiafya za Kimwili:

  • Uzalishaji wa Vitamini D:
    • Mwanga wa jua wa asubuhi ni chanzo kikuu cha vitamini D, ambayo ni muhimu kwa ufyonzwaji wa madini kama vile calcium na ni muhimu sana kwa afya ya mifupa, na utendaji wa mfumo wa kinga.
    • Viwango vya kutosha vya vitamini D ambavyo unaweza kuvipata kwa mwanga wa jua husaidia mifupa yenye nguvu,imara na kupunguza hatari ya mifupa milaini.
  • Husaidia udhibiti wa Mzunguko wa Mwilini (yaani Circadian Rhythm):
    • Mwanga wa jua wa asubuhi husaidia kudhibiti mzunguko wa asili wa kulala na kuamka wa mwili (mzunguko wa circadian).mwanga wa jua wa asubuhi husaidia kuweka sawa mzunguko huu hivyo kukusaidia na kuweka sawa mzunguko wako wa usingizi na kuzuia mvurugiko wa usingizi "sleep disruption" 
    • Hurahisisha kupata usingizi usiku baadhi ya watu wana pata changamoto hii kwamba hawapati usingizi ,kupata mwanga wa asubuhi huweza kusaidia kuondokana na tatizo hili
    • Kwa kufanya hivyo udhibiti huu husaidia ubora wa usingizi tafiti nyingi zinaonyesha uhusiano mkubwa uliopo kati ya kupata mwanga huu asubuhi na ubora wa usingizi pia husaidia kuondoa dalili za kuwa na usingizi asubuhi "morning sleepiness"
  • Husaidia kuimarisha mfumo wa Kinga:
    • Vitamini D, inayozalishwa kutokana na mwanga wa jua, ni muhimu katika kuimarisha mfumo wa kinga, na kuufanya mwili uwe na uwezo zaidi wa kupambana na maambukizi.
    • Pia katika baadhi ya tafiti kuwa na vitamin D ya kutosha mwilini pia hupunguza hatari ya magonjwa ya saratani
  • Faida kwa afya ya akili
    • Kuboresha Hali ya Kihisia:
    • Mwanga wa jua hasa asubuhi husaidia kutolewa kwa serotonini,ambayo husaidia kuleta furaha.
    • Hii inaweza kusaidia kupunguza dalili za unyogovu yaani depression na wasiwasi, ikiwa ni pamoja na baadhi ya matatizo ya mood
  • Kuongeza Viwango vya Nishati na nguvu:
    • Mwanga wa jua wa asubuhi husaidia kupunguza viwango vya melatonin, homoni ya usingizi, na kuongeza cortisol, homoni ambayo hukuza umakini na nishati zaidi na hii husababisha
    • Kuongezeka kwa uchangamfu na umakini  siku nzima. kwahiyo usishangae kuona ukawa mchangamfu baada ya kujaribu 
Mambo ya kuzingatia
  • Ingawa mwanga wa jua una faida nyingi ni muhimu kuzingatia kiasi ili kuzuia  uharibifu wa ngozi.
  • Mwanga wa jua wa asubuhi na mapema ni salama zaidi, kwani nguvu ya miale ya UV ni ndogo.HIvyo hauna madhara kwako 
  • Kwa kuweka katika ratiba yako ya kila siku dakika chache za kupata mwanga wa jua wa asubuhi kutakusaidia kupata faida ulizoziona hapo juu 
Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...