Vipimo 10 vya muhimu kwa mwanaume kuvipima na kujua hali yake ya kiafya

 Moja kati ya vitu ambavyo wanaume wengi hawavipendi ni kwenda kupima ama kucheki afya zao lakini kwa kipindi hiki tunachoishi hasa ukizingatia mabadiliko makubwa ya mitindo ya kimaisha magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa yakisababisha matatizo mengi na kibaya zaidi mengine ni "silent killers" yaani unaweza ukawa nayo na usijue hivyo swala la kwenda kupima si swala la kuchukulia poa ni swala la muhimu sana kwani utaweza kuijua hali yako ya kiafya na kuwa ya mitindo mizuri ya kiafya ukiachana na vipimo vya ugonjwa wa UKIMWI zingatia vipimo hivi vya muhimu sana

  • Shinikizo la Damu: Shinikizo la damu lisilodhibitiwa linaweza kusababisha matatizo ya moyo, kiharusi, na figo.na mara nyingi ni ngumu kuona dalili zake mwanzoni
  • Kiwango cha Sukari: Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababisha matatizo mengi ya kiafya, ikiwa ni pamoja na upofu, kushindwa kwa figo,matatizo katika mfumo wa uzazi na kupoteza miguu.
  • Cholesterol(lehemu): Viwango vya juu vya cholesterol vinaweza kuongeza hatari ya ugonjwa wa moyo.
  • Uchunguzi wa Prostate(tezi dume): Kwa wanaume wenye umri wa miaka 50 na zaidi, uchunguzi wa prostate ni muhimu kugundua mapema saratani ya prostate.na hata kwa vijana wadogo ni muhimu pia kwani kuna mabadiliko mengi sana katika mitindo ya kimaisha 
  • Uchunguzi wa Saratani ya Testisi: Uchunguzi wa binafsi wa mara kwa mara na uchunguzi wa kimatibabu unaweza kusaidia kugundua mapema saratani ya testisi.
  • Vipimo vya Utendaji wa Figo: Figo zina jukumu muhimu katika kuchuja damu. Vipimo vya utendaji wa figo vinaweza kuonyesha kama kuna matatizo yoyote.
  • Vipimo vya Utendaji wa Ini: Ini lina jukumu muhimu katika kusafisha damu. Vipimo vya utendaji wa ini vinaweza kuonyesha kama kuna matatizo yoyote, kama vile hepatitis ,homa ya ini na matatizo mengine
  • Hesabu kamili ya Damu(total blood count): Hesabu kamili ya damu inaweza kugundua anemia, maambukizi, na matatizo mengine ya damu.
  • Vipimo vya Homoni: Vipimo vya homoni vinaweza kutumika kutathmini afya ya uzazi(reproductive health,fertility) na viwango vya testosterone hii husaidia kujua na kurekebisha matatizo ya uzazi kwa haraka kabla hayajawa changamoto zaidi
  • Uchunguzi wa Ugonjwa wa Moyo: Electrocardiogram (ECG) na echocardiogram ni vipimo vya kawaida vya kutathmini afya ya moyo ikumbukwe kwamba ugonjwa wa moyo 'silent killer" umekuwa ukisababisha vifo vya ghafla vya wengi kila mwaka na mara nyingi watu wametembea na ugonjwa huu bila kujua ndio yale utaskia "yaani ni ghafla tu kaanguka" ukweli ni kwamba magonjwa kama haya siyo ya siku moja tu (sio ghafla) yanakuwa kwa muda mrefu mwilini 
  • "Jifunze chukua hatua" tambua hatari mapema na ujikinge mapema
  • Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
    Howdy! How can we help you today?
    Type here...