Baadhi ya aina za PCOS

PCOS inaweza ikajionyesha kwa namna tofauti tofauti kulingana na sababu mbalimbali na tafiti zimeonyesha aina kadhaa zimeelezwa hapa chini

1.Insulin resistant PCOS 

hapa inahusishwa na ukinzani wa insulini  kwa hapa utatuzi utakuwa ni kukabiliana na ukinzani wa insulini 

inahisishwa na zaidi ya asilimia 50 kwamba wanawake wengi wenye tatizo la PCOS utakuta wana tatizo la ukinzani wa insulini (dalili zake zinakuwa kama vile kuongezeka uzito sana mafuta mengi kwenye eneo la tumbo "central obesity",uchovu mkali ,tamaa kubwa ya vitu vyenye sukari "high sugar cravings")

2.Post pill PCOS like symptoms 

hali hii inahusisha dalili zinazoonekana kwa mtu mwneye PCOS ila zinaonekana baada ya kuacha kutumia vidonge vya uzazi wa mpango "birth controll pills" wanapata changamoto hii kwa muda mfupi inatokea sababu mwili unaanza kuangalia namna ya kufanya kazi bila vidonge hivyo ,baada ya muda dalili zake huisha mwili unapoweza kufanya kazi bila vidonge hivyo ,cha kufanya hapa ni kwamba kuweka mkakati wa mitindo mizuri ya kiafya kama vile mazoezi,milo na virutubisho mbalimbali na pia kuthibiti msongo wa mawazo kabla ya kuacha vidonge na ningeshauri uzungumze na daktari kabla ya kuchukua hatua ya kuacha vidonge

3.Inflammatory PCOS 

Hii inatokea pale ambapo mwili unazalisha baadhi ya homoni kwa wingi kutokana na "inflammation" au wakati mwingine kuzalishwa kwa uchache kwa homoni zingine na inapotokea "hormone imbalance" inamueka mtu katika hatari zaidi na mwishowe anaanza kuonyesha dalili za PCOS

4.Adrenal PCOS 

hii inatokea pale ambapo tezi za adrenalini zinapozalisha kwa kiwango kikubwa "androgens" homoni za kiume kutokana na stress au ugonjwa mwingine 

Najua unashangaa homoni za kiume "androgens" zinafanya nini kwa mwanamke?

Testesterone ambayo inajulikana sana kama homoni ya kiume ipo kwa wote ,wanawake na wanaume kilichotofautiana ni viwango tu na ina umuhimu wake

Estrogen pia ambayo inajulikana kama homoni ya kike ipo pia kwa wanaume na ina umuhimu wake kinachotofautiana ni kiwango tu kwamba kwa wanawake ipo kwa wingi zaidi



Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...