Elewa dalili za mwanzo za kupoteza usikivu

Dalili hizi anaziona mtu anayeanza kupata tatizo la usikivu:

  • Kwanza ni ugumu wa kuelewa mazungumzo katika mazingira yenye kelele:
    • Hii ni dalili ya kwanza ambayo watu wengi huona. Unaweza kupata shida kufuata mazungumzo katika mikahawa, sehemu zenye watu wengi, au hata kwenye mikutano. japo haimaanishi ni wakati wote kwani maeneo haya hayakupi utulivu wa kuweza kusikia 
  • Kuhitaji kuongeza sauti ya televisheni au redio kuliko kawaida ama headphones/earpods:
    • Jaribu kuangalia kama unaona watu wengine wanalalamika kuwa televisheni au redio yako ni kubwa sana, inaweza kuwa ishara kwamba usikivu wako unapungua.
  • Mwisho ni kupata shida kusikia sauti za juu au laini/ndogo:
    • Unaweza kuanza kupata shida kusikia sauti za ndege, minong'ono, au sauti za watoto.

Tambua kwamba hizi ni dalili za mwanzo tu na haimaanishi kwamba una tatizo tayari,na kadiri upotezaji wa usikivu unaoendelea,baada ya muda dalili zinaweza kuwa kali zaidi. Ikiwa unapata mojawapo ya dalili hizi, ni muhimu kutafuta ushauri wa daktari wa masikio "audiologist" kwa uchunguzi na matibabu.

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...