Elewa kuhusu addiction na nini cha kufanya
Miaka michache iliyopita nilikutana na case ya mwanamke ambaye ni moja wa waandishi wakubwa kipindi hiki anasema watoto wake walipokuwa kiasi kwamba walifikia hatua ya kujitegemea kipindi ambacho hawakuwa karibu naye sana ndipo alipoanza kuwa addicted na "erotic novels" Yaani zile novel zinazohusu mapenzi "erotic" Alifanya hivyo kama njia ya kukabiliana na hisia za upweke ambazo alikuwa anazipitia baada ya wanawe kuwa mbali na yeye alifanya hivyo kwa muda mrefu ilianza taratibu ikafikia mahali anahitaji kusoma novels nyingi zaidi na ambazo zipo deep zaidi ili kufikia kiwango kile kile cha "pleasure" "Raha" Kama alivyoizoea kila siku
"We are social creatures we have innate need to bond if we lack that bond with other humans we find it in external things and we become addicted to them"
Kila mmoja wetu ana hitaji la ndani la kuungana na kuwa pamoja na watu wengine wa karibu hitaji hilo lisipotimizwa (tukiwa wapweke na tukipitia matatizo bila msaada) tutatafuta katika vitu vingine na tunakuwa waraibu wa vitu hivyo
Ndicho kilichotokea kwmwanamke huyo hapo juu alipokosa muunganiko(bond) na wanae alitafuta pengine ila ilimgharimu
Kwanini nazungumzia kuhusu "addiction"?
Nazungunzia hii sababu ndio uhalisia wa vile vitu ambavyo tunajikuta tupo addicted navyo mwanzoni vinaanza taratibu tunafanya kidogo ila kadiri siku zinavyokwenda tunahitaji kufanya zaidi na kwa muda mrefu ili tuhisi kuridhika inakuwa ndio maisha yako unaona huwezi kuishi bila hiko kitu na mara nyingi unatamani kukiacha lakini unashindwa kila ukijaribu unajikuta umekirudia unajiskia vibaya kisha unaendelea tena na kuendelea
Hapa cha kujifunza ni nini?
Tatizo halikuwa novel tatizo lilikuwa ni hisia za upweke alizokuwa nazo ma zikamsukuma kutafuta kitu cha kujituliza nacho
Amekipata na inafikia mahali anakihitaji tena kwa wingi zaidi na anapata madhara
Chochote ambacho kina mzunguko wa namna hiyo ni addiction kiwe ni kitu/tabia fulani
Kwahiyo linapokuja swala la kusulihisha addiction ni muhimu kujua nini kipo nyuma ya addiction hiyo inakupa nini ambacho umekikosa mwanzoni? Inakupa faida gani? Na je kuna namna nyingine unaweza ukakipata kwa njia ambayo haina madhara makubwa?
Pia elewa vitu ambavyo vinakusukuma kufanya/kujihusisha na tabia hiyo "triggers"
Labda ni mazingira kwamba ukiwa kwenye mazingira fulani unajikuta unakifanya au ni hisia fulani labda ukiwa na huzuni/mpweke/una mawazo ndipo unapojikuta ukifanya hiko kitu
Mambo yanayokuweka katika hatari zaidi ya kuwa addicted
Katika tafiti nyingi yameonekana mambo haya kuchangia zaidi mtu kuwa mraibu cha kwanza ni "lack of meaning" Hapa mtu anapokuwa hana kusudi maalum labda amekaa tu hana anachojihusisha nacho inakuwa rahisi zaidi yeye kujikuta amekuwa mraibu wa kitu fulani pia upweke watu "loneliness fuels addiction" Upweke unaweza kumfanya mtu akatafuta kitu cha kujipooza nacho na ukiendelea kwa muda mrefu anakizoea na anakuwa mraibu wa hiko kitu
Jambo lingine ni "emotional discomfort" Kutokuwa sawa kihisia mfano mtu akiwa na stress wengi bila kujua watatafuta kitu ambacho kitawafanya wajihisi wamepoa
Suluhisho la addiction ni wewe kujiunga tena na kile ambacho ulikikosa mwanzo kama binadamu tunahitajiana na uhusiano baina yako na wenzako usipokuwa mzuri kuna mahitaji yako ya kisaikolojia utayakosa na ukiyakosa hayo utayatafuta katika vitu vingine utavipata ila vinakuja ma gharama kubwa sana
Join the conversation