Elewa kuhusu insulin resistance
Insulin na insulin resistance ni vitu gani?
Insulin ni homoni mwilini mwako inayosaidia kudhibiti
kiwango cha sukari katika damu tofauti na homoni zingine homoni ambazo nyigi
hugusa sehemu fulani pekee homini huu hugusa kila seli mwilini mwako ,yaani
baada ya wewe kula homoni hii huachiliwa katika damu na husaidia kupandisha
sukari ya damu yaani ‘glucose” ili ipate kutumika na seli zote mwilini mwako
“Insulin resistance” ni pale ambapo insulin ipo
lakini haiwezi kufanya kazi yake ipasavyo yaani haipandishi sukari ya damu ili
itumike na seli mablimbali za mwili wako na kudhibiti sukari ya damu matokeo
yake ni kwamba kunakuwa na kiwango kikibwa cha sukari katika damu
hiki ndio chanzo cha magonjwa sugu mengi
Nini chanzo cha insulin resistance?
Japo hali hii inaweza kuchangiwa na genes na urithi lakini
sababu hizi pekee haziwezi kueleza vya kutosha kwanini kumekuwa na ongezeko
kubwa sana la magonjwa sugu kila mwaka watu takriban milioni 10 hufariki
kutokana na saratani,milioni 20 kutokana na magonjwa ya moyo
Sababu hizi za genes na urithi haziwezi kueleza ni kwanini
kumekuwa na ongezeko kubwa namna hii katika miaka michache tu
Huenda kuna sababu nyingine ukiachana na hizi mbili ambazo
zimechangia na kuendesha ongezeko la matatizo haya
Mabadiliko makubwa sana katika kile ambacho tunakila na
mfumo wa maisha una mchango mkubwa sana katika ongezeko la magonjwa haya sugu
nasema hivyo kwa ujasiri hasa katika mazingira yetu haya ya kiafrika kwani
wakati nchi za ulaya na marekeni zilipoanza kukutana na matatizo haya walianza
kutafiti kinachioendelea huku kwetu waliangalia nchi mbalimbali za afrika jamii
na makabila mbalimbali walishangazwa kwani walikuta viwango ni vidogo sana na
kuna jamii hazikuwa na magonjwa hayo kabisa hivyo basi magonjwa haya sababu
zake ni chache sana kuhusu genes na urithi na nyingi kuhusu kubadilika kwa
mitindo yetu ya kimaisha na vyakula na vitu ambavyo vipo katika mazingira yetu
taka hewa na mengine mengi
Ambayo yameamsha vitu ambavyo vinatusababisha kupata
magonjwa haya
Join the conversation