Epuka haya kama una vidonda vya tumbo
Hapa utaona tabia/mienendo ambayo inaweza ikasababisha matatizo zaidi na yanaathiri tumbo lako
1.Usiruke milo
Ni muhimu sana kuzingatia hili kwani tabia ya kuruka milo itaruhusu asidi katika tumbo lako kukutana moja kwa moja na kuta za tumbo hivyo kuipa nafasi ya kusababisha irritations na kuchomeka kwa kuta za tumbo 'inflammation" haitoshi tu kula milo mizuri ya kiafya unahitaji kuwa na ratiba maalum na uepuke kuruka milo
2.Epuka kunywa maji wakati unaendelea kula
unapokunywa maji mengi wakati wa kula kunapelekea kupungua kwa asidi katika tumbo lako hali hii inasababisha kuzalishwa kwa wingi zaid kwa asidi kunywa maji ni muhimu ila jitahidi iwe nusu saa kabla ya kula na tulia kidogo baada ya kula ndipo unywe maji
3.Epuka vyakula vya moto sana/baridi
ni muhimu sana kuzingatia hili
4.Epuka matumizi ya madawa ya NSAID
mfano ibuprofein,asprin,diclofenac,naproxen kwani zinapotumika zinachangia kuharibu ukuta wa tumbo hivyo unakuwa mrahisi kupata madhara ya asidi inayozalishwa tumboni zingatia kumuuliza daktari nini cha kufanya
5.Epuka kulala muda mfupi baada ya kula
Kama umeshazoea kufanya hivyo basi jitahidi uache kwani kunaweza kukawa kunachangia zaidi maumivu unapofanya hivyo unafanya mchakato wa umeng'enywaji wa chakula uwe mgumu zaidi hivyo huleta hali kama kichomi na maumivu zaidi
6.Zingatia kufanya mazoezi
Nashauri kutembea angalau dakika hata 10 baada ya kula ili kurahisisha zaidi mmengenyo wa chakula na wakati unafanya mazoezi mengine zingatia kuusikiliza mwili wako kwani baadhi ya mazoezi yanaweza kukuumiza zaidi na kuongeza maumivu
7.Punguza ulaji wa chumvi na sukari nyingi
Ikitumika nyingi chumvi husababisha muwasho "irritation" zaidi katika tumbo pia sukari ikitumika kwa wingi nayo huleta madhara zaidi tumboni kwani husababisha "inflammation" zaidi na ongezeko la bacteria wabaya wanaoharibu kuta za tumbo hivyo kuleta madhara zaidi
8.Thibiti msongo wa mawazo
kwani huweza kuchangia ongezeko zaidi la maumivu
9.Pata usingizi wa kutosha
Kutokupata usingizi wa kutosha kunapelekea ongezeko zaidi la homoni za stress hivyo zingatia sana kupata usingizi wa kutosha kila siku
Join the conversation