Faida za kiafya za tangawizi
Zifuatazo ni faida za tangawizi kwa afya
- Husaidia kupambana na uvimbe "inflammation":
- Tangawizi ina sifa kubwa za kupambana na uvimbe, hasa kutokana na kemikali ndani yake iitwayo "gingerol"
- Utafiti umeonyesha uwezo wake wa kupunguza "inflammation" na kupunguza maumivu na kuboresha utendaji kazi wa viungo.
- Kwa mfano,tafiti zimeonyesha kwamba tangawizi inapotumiwa kwa wiki kadhaa, linaweza kupunguza maumivu ya goti na viungo
- Udhibiti wa Sukari ya Damu:
- Tangawizi inaweza kusaidia sana kwenye udhibiti wa sukari ya damu, hasa kwa watu wenye kisukari cha aina ya 2(type 2 diabetes)
- Tuliona katika baadhi ya machapisho yaliyopita kwamba tatizo la ukinzani wa insulin linazidi kuwa tishio na inapelekea magonjwa mengi sugu lakini tafiti zinaonyesha kuwa tangawizi inaweza kuboresha ufanyaji kazi wa homoni ya insulini na kupunguza viwango vya HbA1c hivyo kuleta unafuu kwa mgonjwa
- katika moja ya utafiti uliochapishwa na "national insititute of health" wagonjwa wa aina ya pili ya kisukari walifuatiliwa kwa muda wa takribani wiki 8 wakitumia tangawizi kila siku na matokeo yake ni kwamba hali zao ziliimarika "insulini ilionekana kufanya kazi vizuri zaidi"
- Rejea hapa kuona chapisho hilo https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/24559810/
- Kupunguza Maumivu:
- Tangawizi imeonyeshwa kuwa na sifa za kupunguza maumivu, hasa kwa maumivu ya awali ya hedhi na maumivu ya misuli.katika tafiti nyingi tangawizi "ginger supplements" zilionekana kupunguza maumivu haya
- rejea hapa kuona chapisho la utafiti kwa uhakika zaidi huo https://pmc.ncbi.nlm.nih.gov/articles/PMC8021506/
- Utafiti hapo juu unaonyesha kuwa tangawizi inaweza kuwa na ufanisi katika kupunguza dysmenorrhea (maumivu ya hedhi) na maumivu ya misuli
- uwezo wake wa kupambana na uvimbe "inflammation" wa tangawizi unachangia uwezo wake wa kupunguza maumivu.
- Afya ya Utumbo:
- Tangawizi inaweza kusaidia mmeng'enyo mzuri
- Pia inaweza kusaidia kupunguza dalili za gesi.
- Husaidia kupunguza dalili za mafua na kichefuchefu

Join the conversation