Ielewe PCOS
UGONJWA WA PCOS
Ni tatizo la homoni ambalo linawaathiri sana wanawake wengi waliopo katika umri wa kuweza kuzaa "reproductive age"(hasa miaka 20 na kuendelea) ni chanzo kikubwa cha utasa "infertility" kwa wanawake wengi kutokana na tatizo hili
tafiti zinaonyesha kwamba karibu asilimia 15 ya wanawake wote duniani wanakumbana na tatizo hili japo inaaminika kwamba ni wanawake wengi wanakumbana na tatizo hili na hawajui kama wanapitia hali hii karibu asilimia 70 ya wanawake wenye ugonjwa huu hawafahamu kama wana ugonjwa huu kwani mara nyingi tatizo hili linaambatana na baadhi ya dalili ambazo zinaonekana ni kawaida kuwapata wanawake wengi wanaishia kutulia nao wanaona ni sehemu ya kuwa mwanamke "just part of being women"
Japo jina linaonekana ni jipya lakini tatizo hili lilikuwepo kwa muda mrefu miaka na miaka ni kwamba tu mazingira na mitindo ya maisha ya kisasa inazidi kufanya tatizo hili kuwa kubwa zaidi kila kukicha
huenda mpaka sasa unajiuliza PCOS ni nini na unatamani kuelewa nini ambacho kinatokea endelea kusoma ..
Kwahiyo PCOS ni nini hasa? nini kinatokea?
Kama ulivyoona hapo mwanzo kwamba ni tatizo la homoni usawa unakosekana katika homoni za uzazi "hormonal imbalance" utakuta ongezeko la homoni za kiume "androgens' kama vile testesterone na pia ongezeko la homoni kama vile insulini inapotokea hii inasababisha matatizo katika "ovary"(zinahusika kuzalisha mayai ya uzazi) hivyo ovary hushindwa kuzalisha mayai
Homoni za kiume na za kike?
Katika tatizo hili la PCOS zinazojulikana kama homoni za kiume huzalishwa kwa wingi kwa mwanamke husika
Japo tumezoea kusikia baadhi ya homoni zikiitwa kuwa ni za kiume na nyingine zikiitwa ni za kike lakini mfano homoni ya "testesterone" huitwa homoni ya kiume lakini ipo pia kwa wanawake na ina kazi zake ,homoni ya estrogeni ipo kwa wingi kwa wanawake lakini pia ipo kwa wanaume na ina kazi zake
Hali halisi ya tatizo hili
Tafiti zinaonyesha kwamba tatizo hili linazidi kuongezeka kipengele cha urithi kina mchango wake ila haiwezi kutupa majibu ya sababu ya ongezeko kubwa la tatizo hili hivyo mazingira ,vyakula,na mitindo ya kimaisha kwa ujumla yanaonekana kuwa na mchango mkubwa pia
Dalili za PCOS
Dalili zinatofautiana toka kwa mtu mmoja na mwingine baadhi ni kama vile mvurugiko wa hedhi,hedhi zisizo za kawaida,ukuaji wa nywele kupita kiasi,chunusi,kuongezeka uzito hasa eneo la tumboni,madoa meusi katika ngozi,utasa "infertility",kupoteza nywele ,ukinzani wa insulini,mabadiliko ya mood
Sababu za tatizo hili
Sababu halisi za tatizo hilo bado hazijulikani ila linahusishwa na baadhi ya mambo haya
1.Ukinzani wa insulini tatizo ambalo nalo linazidi kuongezeka sana na linachangia mvurugiko wa homoni bado upo ubishani kati ya PCOS na ukinzani wa insulini kwamba yupi anayemsababisha mwenzake 'kuku ni yupi?, yai ni lipi?" lakini kwa asilimia kubwa wanawake wenye tatizo hili utakuta wana ukinzani wa insulini ila kuna wengine hawana ukinzani wa insulin
2.Historia ya familia kama tatizo hili limeonekana kusumbua ndugu wa familia fulani inaongeza hatari zaidi kwa anayetokea katika familia hiyo kujikuta ana tatizo hili
MUHIMU: Elewa kwamba kuwa na historia ya tatizo fulani katika familia haimaanishi siku zote kwamba unaweza ukapata tatizo hilo unaweza ukachukua hatua na kupunguza hatari zaidi ya wewe kupata ugonjwa huu kwani mazingira unayoishi ,vyakula unavyokula na mitindo ya maisha yana mchango sana wa kuamua kwamba upate tatizo hili au la
"Genes loads a gun ,enviroment and lifestyle pulls a trigger"
Uwepo wa historia ya ugonjwa katika familia haukuaandikii sentensi kwamba utapata tatizo hilo bado kuna kitu unaweza ukakifanya
3.Inflammation
Japo mchakato huu ni muhimu mwilini, inapokuwa sugu ni hatari kwa afya kwani inaweza kuchangia ongezeko zaidi la homoni za kiume "androgens" na pia inaweza kuongeza zaidi dalili za ugonjwa huu
inflammation sugu inachangiwa sana na mambo kama vile ukosefu wa mazoezi,utumiaji wa vyakula vyenye sukari nyingi,mafuta mabaya "unhealthy fats",msongo mkali wa mawazo
Upimaji unafanyikaje?
tatizo hili linagundulika kwa kufanyiwa vipimo mbalimbali ikiwemo vile vitakavyoangalia viwango vya homoni ,kuangalia historia ya mtu,au kupitia"ultrasound"
Matibabu na suluhisho
Mabadiliko ya mtindo wa maisha kama vile kufanya mazoezi,kuzingatia lishe bora yameonekana kupunguza hatari ,pia kupunguza uzito kunaweza kusaidia sana kwa tatizo hili baadhi ya dawa za kuoambana na "androgen" pia hutumika ,vidonge vya uzazi wa mpango na pia kusuluhisha magonjwa sugu kama kisukari kunaweza kupunguza ukali wa tatizo hili
Join the conversation