Kutokwa na jasho kupita kiasi
Hali ya kutokwa na jashi jingi inaweza kuleta usumbufu "discomfort" kwa mtu hali hii kitaalamu huitwa "hyperhidosis"
Hyperhidosis ni nini?
ni pale ambapo mtu anatokwa na jasho jingi isivyo kawaida inaweza kuwa ni eneo moja mfano kwapa,uso,migu
uni,viganja vya mikono au mwili mzima ,hali hii inaweza kukuletea wasiwasi na ukashindwa kuendelea na kazi zingine za kila siku
sababu ya hali hii kutokea?
Baadhi ya sababu hazijulikani ila kuna mambo mengine ambayo yanaweza kusababisha hali hii ikiwemo baadhi ya dawa,au ugonjwa fulani ambao mtu anaumwa kwa wakati huo kama vile
1.Kisukari
2.Kifua kikuu
3.Aina fulani za saratani na mabadiliko ya homoni mwilini
4.Pia hali hii huonekana kipindi cha mzunguko wa hedhi hasa nyakati za usiku
5.Homa kali inaweza kuambatana na dalili hii pia
Sababu zingine zinaweza kuwa ni mabadiliko aliyoyafanya mtu mfano baadhi ya watu walioacha pombe/dawa za kulevya huonekana kama dalili moja wapo ya kile kinachoitwa "withdraw" kwa watu wengine pia wakiwa na wasiwasi mkubwa hujikuta wanatokwa na jasho

Join the conversation