Kwanini viwango vya depression vimeongezeka ?

 


Japo sababu za kibaiolojia zina mchango pia na mabadiliko ya mitindo yetu ya kimaisha na mazingira tunayoishi hivi sasa yote hayo yanachangia lakini baiolojia peke yake haiwezi kuelezea kwanini kumekuwa na ongezeko kubwa la hali ya unyongofu “depression” vipi kama kuna sababu nyingine ambayo inakwenda mbali zaidi ambacho wengi tunafikiri ndicho kinachochangia ongezeko la depression

Ukweli ni kwamba depression inaogezeka na kuzidi kuongezeka kunapelekewa pia na namna ambavyo tunaishi hivi sasa kama ifuatavyo

ü  Upweke /kutenganishwa na watu tupo katika kipindi ambacho tumeunganishwa na mitandao ya kijamii na teknolojia mbalimbali lakini ubora wa mahusiano ni mdogo kwa wengi hivyo kadiri siku zinavyozidi Kwenda tunazidi kuwa wapweke japo kwa nje tunaonekana tuna watu na jamii kubwa iliyotuzunguka na upweke huo unatupeleka katika hali ya unyongofu “depression”

ü  Kutenganishwa na kazi yenye maana “disconnection from meaningful work” moja ya hitaji la kisaikolojia ni hili “wewe kuhisi kwamba una mchango au una umuhimu katika maisha ya wengine pia ‘ unapofanya kazi ambayo inakupa kuona kwamba una mchango halisi katika wale wanaokuzunguka huambatana na tumaini na unapokuwa na tumaini kinachotokea ni kwamba hatari ya kupata unyongofu inapungua

ü   Junk values hii hasa inachochewa na kile ambacho tunakiona katika mitandao tunaowaona mtandaoni naziita “junk values” ni mitazamo mbalimbali inayotufanya tuwe na mtazamo fulani juu ya maisha na furaha mitazamo mara nyingi wanatufanya tuone kwamba kuna njia rahisi ya kufikia mafanikio mtazamo wako utakuwa juu ya namna gani watu wengine wanakutazama mwisho wa siku inakujengea hali ya wasiwasi wa kila mara 

ku Kukosa tumaini la maisha fikiria mtu ambaye hana kazi na hajui nini cha kufanya fikiria mtu ambaye anasumbuliwa na magonjwa sugu kama kisukari ,saratani ni hali ambazo zinahitaji gharama nyingi na usimamizi mkubwa watu wengi wenye hali hizi hukosa tumaini la maisha pia fikiria mtu ambaye anapitia hali ngumu ya kiuchumi mtu huyo naye ana hatari kubwa zaidi ya kujikuta katika hali ya unyongofu  

ü  Trauma mambo magumu mtu aliyopitia utotoni mwake kama kurubuniwa,kulawitiwa,kubakwa ndizo zinazoitwa trauma na watu waliokutana na hali hizi mara nyingi wapo katika hatari kubwa zaidi ya kujikuta wanakumbwa na unyong’ofu

ü  Mabadiliko katika ubongo na mchango wa vinasaba ni kweli kwamba pia wapo baadhi ya watu ambao wanakuwa katika hatari ya kupata hali ya unyongofu sababu ya vinasaba Fulani lakini ikumbukwe kwamba kuwa na vinasaba vya tatizo fulani haimaanishi una tatizo hilo bali tatizo hilo linaweza kujitokeza utakapokuwa katika mazingira fulani “genes load a gun environment pulls the trigger”

ü   

 

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...