Maumivu makali ya hedhi “severe painful periods
Maumivu makali sana ya hedhi “severe painful periods
Maumivu yanatokea wakati wa hedhi ila kwa wengine maumivu
haya yanakuwa makali sana kiasi cha kuharibu mpangilio wa maisha yako ya kila
siku changamoto hii imezidi kuongezeka na kibaya zaidi ni kwamba wengi
wanapopitia changamoto hii wanatafuta suluhisho la haraka matumizi ya vidonge
kama vile ibuprofein kwa muda mrefu yanaweza kuwa na athari nyingine kama
kuumwa kichwa na mara nyingi matumizi ya dawa kiholela yanaweza
yakaonekana kuleta unafuu kwa muda mfupi ila tatizo linakuwa bado halijatatuliwa
kabisa ni muhimu kuelewa hali hii inazidi kuwa ngumu zaidi kwa kuelewa haya
inaweza kusaidia angalau kutatua
Baadhi ya mbinu hizi zinaweza kuleta unafuu
- Sababu
ya kwanza ni upungufu wa virutubisho katika vyakula ambavyo vinatumika kwa
wingi
Virutubisho kama vile magnesium husaidia na omega -3
husaidia sana kupumzisha misuli na kupunguza “inflammation” na kupunguza
uzalishwaji wa kemikali ambazo zinaweza kusababisha ongezeko zaidi la maumivu
Unadhani nini kitatokea ukivikosa hivi?
Katika moja ya utaifi uliochapishwa na “National institute
of health (NIH)” wanawake wa umri kati ya miaka (18-22) waliokuwa wakipitia
maumivu ya hedhi walisimamiwa kutumia virutubisho vya omega-3 kwa muda wa miezi
mitatu matokeo yake ni kwamba wale waliofanya hivyo hawakuhitaji dose kubwa ya
ibuprofen na matumizi hayo yalipunguza ukali wa maumivu.tafiti zilionyesha
matokeo hayo pia kwa magnesium
Hivyo jitahidi kuhakikisha mlo wako una vyakula ambavyo vinakupa virutubisho vya kutosha
Unavipata wapi ? katika mboga mboga za majani kwa
wingi,Samaki,almonds,chia seeds,parachichi hakikisha unakula mlo kamili
- Vyakula
vya kisasa
Vingi utakuta kwamba vina vitu ambavyo vinachochea zaidi
“inflammation” huvuruga afya ya tumbo lako “gut health” hasa husababisha
kupotea kwa jamii ya bacteria waitwao “estrobolome” ambao wanahusika na
kuchakata na kusaidia kuondoa estrogen mwilini hivyo kuleta balance
vyakula vyenye sukari nyingi vinajulikana kwa kuchochea zaidi "inflammation" na dawa kama vile ibuprofen ambayo hutumiwa na wengi kipindi hiki inasaidia kupunguza maumivu hayo kwani ni "anti inflammatory' yaani ianapambana na inflammation hivyo ukipunguza ulaji wa vitu vyenye sukari nyingi utapunguza inflammation na maumivu pia yanaweza yakapungua
Unafikiri nini kitatokea wakipotea hao?
Mchakato huo hautafanyika kwa ufanisi kinachofata ni kwamba
viwango vya estrogen mwilini vinakuwa vikubwa zaidi “estrogen excess” na
kupelekea maumivu kuwa makali zaidi au kuendelea kwa muda mrefu zaidi
- Kukosa mazoezi pia kunachangia
Swala la mazoezi ni changamoto kwa wanawake kutokana na
baadhi ya fikra ambazo tayari wameshajijengea hivyo wengi hawafanyi mazoezi
jambo ambalo linaongeza hatari zaidi mazoezi yanasaidia sana katika kuhakikisha
“hormone balance” hasa yanasaidia balance katika homoni ya estrogen ,kupunguza
“inflammation” na pia husaidia kupunguza maumivu ya hedhi
Mazoezi unayoyaepuka yanaweza kukusaidia sana.
Katika moja ya tafiti watu 1808 waliomaumivu yalionekana
kupungua kutokana na ufanyaji wa mazoezi ,mazoezi yalionekana ni njia nzuri
sana ya kupunguza maumivu kipindi cha hedhi
rejea chapisho halisi la utafiti huo (national institute of health)
Matokeo ya namna hiyo yameonekana katika tafiti zingine
nyingi sana
mazoezi yanasaidia kwanza ni kwasababu yanapunguza inflammation na kuziweka homoni katika utaratibu sahihi
Je utaanza kufanya mazoezi?
Namna rahisi za kuanza kufanya mazoezi ni kuanza tenga muda
wa kufanya mazoezi,tembea,ruka kamba jizoeshe yatakusaidia kukuweka sawa
kimwili na kiakili pia
- Msongo
mkali wa Mawazo “chronic stress”
Msongo mkali wa Mawazo “chronic stress” ni moja kati ya
wavurugaji wakuu wa “hormone balance” ongezeko la homoni za stress
husababisha homoni zingine kama progesterone zisiweze kufanya kazi vizuri hivyo
hupelekea maumivu makali zaidi “intense contraction and painful scramps”
- Shida
katika ini "liver problems"
Ini linahusika katika kuchakata homoni zifanye kazi kwa
ufanisi zaidi nini kitatokea kama kazi hiyo haifanyiki vizuri?
Yanayoweza kuathiri utendaji kazi wa ini ni vitu kama vile
pombe,utegemezi wa madawa,na sumu mbalimbali
Ini litashindwa kuchakata homoni kama “estrogen” kwa ufanisi
na kuhakikisha kwamba ipo kwa kiwango sahihi hivyo homoni hiyo huwa nyingi na
kupelekea maumivu kuwa makali zaidi
- Sababu
nyingine ni “endocrine disruptors” kemikali ambazo zinajificha katika
baadhi ya vitu ambavyo tunavitumia kila siku iwe nim aji,vyakula,bidhaa za
urembo
Baadhi ni kama
Bisphenol A (BPA): Inatumika kwenye plastiki na mipako ya
ndani ya baadhi
Phthalates: Inapatikana kwenye plastiki, vifungashio vya
chakula, na bidhaa za kujipamba.
Dawa za kuua wadudu: Kama vile DDT, atrazine, na
chlorpyrifos.
Sikuwahi kulichukulia swala hili kwa uzito zaidi hadi pale
nilipokutana na kichwa cha Habari katika gazeti la mwananchi “Chembe za
plastiki zinaathiri ubora wa mbegu za kiume” Habari hii ilielezwa na Profesa
Mohamed Janabi ambaye ni mkurugenzi wa hospitali ya taifa Muhimbili alieleza
kwa undani namna ambavyo kemikali kama vile BPA ambayo inatumika katika
kutengeneza plastiki na inatumika katika vyombo vya chakula kama ulivyoona hapo
juu na namna ambavyo zina athari katika afya ya uzazi na kuoenekana kama jambo
ambalo linachangia baadhi ya matatizo katika afya ya uzazi
Kwanini zinaleta athari hizi?
Kemikali hizi zinafanya kazi kama homoni za mwili hivyo
zinaweza kuharibu utaratibu wa kawaida au kupelekea ongezeko la baadhi ya
homoni Fulani na kupungua kwa nyingine hivyo hupelekea maumivu makali kwa
mwanamke
Jitahidi kupata ushauri wa daktari unapopitia hali hii
tafuta msaada na ushauri wa kitaalamu utapata dawa na kushauriwa nini cha
kufanya pia
.jpg)
Join the conversation