Siri nyuma ya mazoezi ya nguvu "strength training"


Upo uhusiano uliopo kati ya nguvu ya misuli "greater muscular strength' na hatari ndogo ya kupata ugonjwa wa saratani uhusiano huu umeonekana katika tafiti nyingi ambazo zimefanyika ikiwemo moja ambayo utaiona katika chapisho la leo katika utafiti wa wanaume takriban 8000 wa umri kati ya miaka 20 na 82 ambao walifatiliwa kati ya miaka ya 1980 hadi 2003 watafiti waliangalia uimara wa misuli katika mazoezi maalum (leg press na bench press) wanaume hao waliwekwa katika makundi mbalimbali kulingana na uimara wa misuli yao kisha watafiti waliangalia ni wangapi katika kila kundi walikufa kutokana na saratani wale waliokuwa na na uimara wa katikati "middle group" walipunguza hatari ya kupata saratani kwa asilimia 35% kulinganisha na kundi ambalo walikuwa na uimara mdogo ,kundi ambalo walikuwa na uimara wa juu zaidi walipunguza hatari kwa asilimia 40% ya kupata saratani

na watafiti hao waligundua kwamba kwa kuimarisha uimara wa misuli hatari ilipungua zaidi

kuna siri gani nyuma ya mazoezi ya nguvu "strength training"?

Mazoezi ya nguvu, kama aina nyingine za shughuli za mwili, yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza hatari ya saratani kupitia njia mbalimbali. kama ifuatavyo

  1. Udhibiti wa Homoni:
    • Mazoezi ya nguvu yanaweza kusaidia kudhibiti viwango vya homoni, kama vile insulini na estrojeni.
    • Viwango vya juu vya homoni hizi vimehusishwa na hatari kubwa ya saratani fulani, ikiwa ni pamoja na saratani ya matiti, saratani ya utumbo mpana na zingine
    • Kwa kudumisha usawa mzuri wa homoni, mazoezi ya nguvu yaani strength training yanaweza kusaidia kupunguza hatari ya kupata saratani.
  2. Kupunguza hali ya infammation:
    • Inflammation sugu ni kichocheo kikubwa sana cha ukuaji wa saratani.
    • Mazoezi ya nguvu yanaweza kusaidia kupunguza hali hii kwa kuchochea utolewaji wa vitu vinavyopambana na inflammation.
    • Kwa kufanya hivyo husaidia kutengeneza mazingira ambayo yatazuia ukuaji wa seli za saratani
  3. Husaidia kuboresha Muundo wa Mwili:
    • Mazoezi ya nguvu hujenga misuli na husaidia kupunguza mafuta mwilini.
    • Mafuta mengi mwilini, hasa mafuta ya tumbo haya yanahusishwa na hatari kubwa ya saratani
  4. Kuimarisha Utendaji wa Kinga:
    • Mfumo imara wa kinga ni muhimu kwa kutambua na kuharibu seli za saratani.
    • Mazoezi ya nguvu yanaweza kusaidia kuimarisha utendaji wa kinga, na kufanya mwili kuwa na ufanisi zaidi katika kupambana na saratani.
  5. Kuboresha usikivu insulini  kitaalamu "insilin sensitivity" :
    • Mazoezi ya nguvu yatakusaidia kujenga misili ambayo itasaidia kuimarisha "insulin sensitivity" hivyo insulini itafanya kazi vizuri mwilini mwako na hakutakuwa na viwango vya juu sana vya insulini
    • Kumbuka kwamba viwango vya juu sana vya insulini vinaweza kuchochea ukuaji wa seli za saratani.
    • Mazoezi ya nguvu husaidia insulini kufanya kazi kwa ufanisi zaidi mwilini 
  • Kumbuka ni muhimu sana kwako wewe kuhakikisha unaunganisha kwa pamoja mazoezi ya nguvu na mitindo mingine kama vile lishe bora na mazoezi ya aerobic kama kukimbia ,kuruka kamba ili kupata faida zaidi kiafya na kupunguza hatari ya saratani 
  • Jitahidi kujihusisha katika mazoezi ya nguvu yaani strength training kwani yana faida nyingi kiafya sio tu afya ya mwili bali afya ya akili pia 
Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...