Tabia ndogondogo zinazokuongezea depression

Depression inaweza kutokea pale ambapo mambo madogo madogo ambayo yanaendelea katika maisha yako na unaweza ukawa huyaoni yakiunganika kwa pamoja unapoweza kuyaona hayo mambo madogo "micro patterns" unaweza kuimarisha afya yako ya akili tunzinagalie zaidi hapa chini.

  • Kujitenga na Jamii: Tabia ya wewe kujitenga na watu wa karibu hasa ukiwa katika kipindi kigumu kunaweza kuongeza hisia za upweke na kutakufanya ujiskie vibaya 
  • Ukosefu wa Shukrani "lack of gratitude": Hapa ni pale ambapo unazingatia  tu vipengele hasi vya maisha na unapuuzia  mambo mazuri ambayo yametokea kwenye maisha yako hali hiyo inaweza kukuongezea zaidi kujiskia vibaya
  • Kujiwekea matarajio makubwa toka kwa watu "high expectations" mara zote unapoweka matarajio makubwa sana kwa mtu anaweza isistokee kama ulivyotaka ikakuacha ukijiskia vibaya sana 
  • Kuongeza ukubwa wa Matukio"Catastrophizing": Kukuza ukubwa wa matatizo na kutarajia hali mbaya zaidi kunaweza kukuongezea wasiwasi na msongo wa mawazo.
  • Kuahirisha Mambo mara kwa mara: Kuahirisha kazi mara kwa mara kunaweza kusababisha hisia za kuzidiwa, hatia, na kupungua kwa ufanisi wa kibinafsi.
  • Kutafakari sana mambo mabaya yaliyopita "ruminations": Kurudia mara kwa mara matukio au mawazo hasi akilini mwako, bila kutafuta suluhisho, kunaweza kuendeleza hisia za huzuni na kukufanya kukata tamaa..
  • Matumizi Kupita Kiasi ya Mitandao ya Kijamii: Kujiweka muda mwingi kunakupelekeahisia za kutostahili na kunaongeza kujilinganisha na wengine mambo ambayo yatakufanya ujiskie vibaya zaidi
  • Mazungumzo Hasi ya "negative self talk" hii inatokea pale unapojihusisha na kujikosoa mara kwa mara, kujilaumu, na kujitabiria mambo mabaya kwamba ndiyo atakayokupata 
  • Kupuuza kujijali: kufanya mambo kama vile kukosa usingizi,ulaji mbaya,kuwa na maisha ya kukaa tu "kukosa mazoezi" zote hizi husaidi kwa namna moja ama nyingini kukuweka sawa hivyo unapokuwa hauvifanyi hautakuwa sawa u
"The good news is that joy is collected over time what joy are you collecting today?"
fanya mambo ambayo yanaiweka sawa afya yako ya akili na sio kuidhuru


Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...