Usingizi na homone balance
Upo uhusiano mkubwa sana kati ya usingizi na usawa wa homoni. Usingizi wa kutosha ni muhimu kwa kudumisha usawa wa homoni mbalimbali mwilini
Homoni Muhimu Zinazoathiriwa na Usingizi:
- Cortisol"homoni ya msongo wa mawazo": Kukosa usingizi husababisha kuongezeka kwa viwango vya cortisol, "homoni ya msongo wa mawazo."
- Cortisol nyingi sugu inaweza kuvuruga kazi ya kinga ya mwili,hisia na usawa wa homoni
- Melatonin: Melatonin, "homoni ya usingizi," .
- Kuvurugika kwa mifumo ya usingizi "sleep patterns" kunaweza kupunguza uzalishaji wa melatonin.hivyo upo uwezekano mtu akapata tatizo la kutokupata usingizi "insomnia" ambalo nalo linaweza kupelekea matatizo mengine zaidi kama halitashughulikiwa
- Leptin na Ghrelin: Homoni hizi hudhibiti hamu ya kula.
- Kukosa usingizi hupunguza leptin (homoni ya kushiba) na huongeza ghrelin (homoni ya njaa), na kusababisha hamu ya kula kuongezeka na uwezekano wa kuongezeka kwa uzito. ndio maana ukijiangalia siku ambayo hujapata usingizi wa kutosha unaweza ukajikuta umechoka na unahisia njaa isiyo kawaida
- Insulini: Kukosa usingizi wa kutosha unaweza kuharibu uwezo wa insulini kufanya kazi, na kuongeza hatari ya ukinzani wa insulini na kisukari cha aina ya 2.
- Homoni ya Ukuaji yaani "growth hormone": Homoni hii hutolewa hasa wakati wa usingizi mzito na ni muhimu sana kwa ukarabati wa seli na kuzaliwa upya kwa tishu.fikiria nini kitatokea kama kukiwa na mvurugiko katika usingizi? au ikiwa hupati usingizi wa kutosha?
- Homoni za uzazi: Kukosa usingizi kunaweza kuathiri uzalishaji wa homoni za ngono kama testosterone, na kuathiri libido "hamu ya tendo" na afya ya uzazi.
Umuhimu wa Usingizi Bora:Usichkulie poa usingizi!!!
- Kudumisha ratiba maalum ya usingizi, tengeneza mazingira mazuri ya kulala, na upe usingizi wa kutosha kipaumbele kwani ni muhimu kwa afya ya homoni.
- Na kama una matatizo ya kupata usingizi kama vile "insomnia" ni muhimu sana kutafuta suluhisho

Join the conversation