Wanaume na afya ya akili wafanye nini?
Jiulize mara ya mwisho umeskia mtu kajiua alikuwa mwanaume au mwanamke? au mara nyingi unaposikia habari hiyo huwa ni akina nani wanaongoza zaidi kujitoa uhai? kwanini ni wanaume zaidi?
Nini kinaendelea kwa upande wa wanaume?
Binafsi nimekuwa na wasiwasi juu yangu na kuhusu wavulana na wanaume kwa ujumla wasiwasi wangu upo sana juu ya ustawi wao hasa katika eneo la afya ya akili kwani tumekua katika jamii ambayo inajaribu kutujengea misingi ambayo tusipokuwa makini itazidi kutuangamiza katika ukimya tumejengwa katika misingi ya kuogopa kufunguka kuhusu kinachoendelea katika maisha yetu/magumu ambayo unayapitia tunatupiwa jumbe mbalimbali tangu utotoni kwamba "real men dont cry" ni kwa lengo zuri la kutufanya wakomavu lakini kuna kipindi haifanyi kazi tusisahau kwamba sawa ni mkomavu sawa ni shupavu lakini usisahau kwamba wewe ni binadamu na kama mtu ni kuna wakati utakutana na mazingira magumu kuna kipindi utapitia maumivu ya kihisia kuna kipindi mahusiano yatavunjika na kwa bahati mbaya hatuna mbinu za kutosha za namna ya kupambana na hali hizi hivyo tunazificha ndani yetu kama siri tunateseka peke yetu kwasababu hujafunguka na wakati mwingine maumivu haya yanapozidi tunatafuta namna ya kupooza maumivu haya labda ni kwa pombe,au video za ngono na mengine tunatumia mbinu hizo kupooza maumivu hayo bila kuyatatua kabisa tunadhani tupo sawa tunasahau kwamba mwili hausahau mwili unatunza maumivu hayo kidogo kidogo yanaendelea kujikusanya ndani japo hayaonekani taratibu yanaanza kukusumbua zaidi na mwisho wa siku kama bomu hulipuka puuuh utaskia fulani kajitoa uhai unashangaa mbona alikuwa sawa? mbona jana nilikuwa naye? hapana hakuwa sawa amevumilia vya kutosha na hakuwa na cha kufanya kwa kuogopa aibu na kuogopa kwamba nitaonekanaje nikisema nateseka na kitu hiki suluhisho pekee kwake lilikuwa hilo
Nini ufanye?
Elewa kwamba wewe ni jasiri lakini hauna kinga juu ya majanga tuliyoyaona hapo juu kuna muda yatakupata,utakutana nayo katika maisha yako labda hata unapitia muda huu unapoisoma makala hii elewa kwamba ni kawaida lakini hupaswi kuteseka nalo peke yako elewa kwamba unapoendelea kuficha yanayokutesa ndani yako yatakuletea madhara zaidi tafuta msaada tafuta msaada na badala ya kuchukua uamuzi mbaya au kukata tamaa au kuona maisha hayana thamani tena kwako tafuta kujua sababu ya hayo unayoyapitia
zi ili zisiendelee kutuumiza"
usiteseke peke yako tafuta msaada

Join the conversation