Dalili za ukinzani wa insulin

Jambo moja ambalo unaweza ukalifanya leo ni kuhakikisha unaichunguza afya yako ili kujua kinachoendelea mwilini mwako kwani ni wengi wana hali hii tayari ila hawajui sana kwa sababu hali hii huendelea taratibu na mwishowe hali hii hupevuka na kuingia katika matatizo halisi kama kisukari na magonjwa mengine sugu vishairia vyake ni kama vifuatavyo

1.Kiwango cha insulin ya zaidi ya sita yaani 6uU/ml katika kipimo cha maabara

2.Kipimo cha kiuno “waist circumference” kwa wanaume upana wa kiuno zaidi ya inchi 40 na wanawake upana wa kiuno wa inchi 35 ni kiashairia kuwa tayari mtu anapitia hali ya ukinzani wa insulin sana kwa sababu mafuta mengi katika eneo hili yanajulikana kuchangia ukinzani wa insulin

3.Shinikizo la juu la damu ,kipimo zaidi ya 140/90 mmHg pia ni dalili ya ukinzani wa insulin

4.Wanaotumia pia dawa za kupunguza shinikizo la juu la damu ni dalili ya wazi kabisa kwamba kuna ukinzani wa insulin

5.Wingi wa sukari zaidi ya 100mg/dl ni dalili pia ya kuwa na tatizo hili la ukinzani wa insulin mwilini

6.Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa yaani libido ndogo na kwa wanaume kukosa nguvu za kiume japo sio muda wote ila nacho ni kishiria cha ukinzani wa insulin

7.Dalili zingine ni kama vile kushindwa kulala “insomnia” kupanda na kushuka kwa nguvu za mwili ,,kuhisi kuchoka sana baada ya kula,maumivu ya magoti na viungo KUMBUKA  hizi dalili zinaweza kuwa ni kutokana na tatizo lingine na isiwe ukinzani wa insulin cha muhimu ni kujua chanzo cha dalili hizi ni nini

8.Matatizo katika homoni kama vile PCOS yaani polycystic ovarian syndrome

Kama nilivyotangualia kusema hapo mwanzo inabidi tuwe na mkakati wa kuchunguza na kujua hali zetu za kiafya kumbuka inachukua miaka hadi 10 kutoka ukinzani wa insulin hadi kuona mtu ana kisukari

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...