book of moods
Moods zinaweza kuathiri mawazo na namna tunavyoishi hata kama usipolijua hilo na mara nyingi moods zinatokana na matukio au mambo yanayotokea na namna tunavyoyaona mambo hayo inaathiri jinsi tunavyojiskia
kitabu hiki ni namna ambavyo mwandishi alivyoweza kugeuza nyakati mbaya maishani mwake kuwa nyakati njema zaidi (turning worst emotions into best life) baadhi hapa ni mambo ya muhimu toka kwenye kitabu yanayoweza kukusaidia kuimarisha uwezo wako wa kuthibiti hisia zako na pia kuimarisha afya yako ya akili
Kwanini ni ngumu kujipenda(self love)?
Ni rahisi sana kusema unajipenda lakini sio kweli unapokuwa kwenye tatizo fulani huwa unajiambia nini? unapoumwa labda huwa unajiambia nini? mara nyingi utakuta kwamba unajiambia labda hali yako itabakia hivyo hivyo au itaendelea kuwa vibaya zaidi
Mwandishi anasema "so many of us have difficulty with self love because our automatic thoughts override it automatic thoughts are immediate thoughts that occur after negative events"
Tafsiri yake:"wengi tuna shida ya kujipenda kwa sababu mawazo yetu ya moja kwa moja hulipuuzia hilo mawazo ya moja kwa moja ni mawazo ya haraka ambayo huja baada ya matukio mabaya"
Baada ya tukio baya kutokea huwa unajiambia nini? huwa unawaza nini juu yako?
Fanya hivi :Unapokutana na changamoto labda ni ugonjwa au changamoto nyingine badala ya kuona kwamba hali itakuwa mbaya zaidi fikiria ingekuwa ni rafii yako au ndugu yako yupo katika hali hiyo ungemuambia nini? Jiambie hayo na ujiwazie hayo
mawazo mabaya ama "distorted thoughts" yanatokea kila mara tunapokuwa katika hali ngumu tunahitaji kukaa chini na kuyaangalia kwamba je yana ukweli ndani yake ? unachojiwazia kinaweza kuathiri unavyojiskia
Mwandishi anasema ukijifunza kufikiria tofauti unaweza kubadili namna so tu unavyoiona dunia bali namna ambavyo tunaenenda
mwisho mwandishi kaelezea namna ambavyo unajiweka katika mzunguko wa distorted thinking
Filtering: Kuchuja. Hii inahusisha kuzingatia tu mambo mabaya ya hali fulani huku ukipuuza mazuri. Ni kama kuangalia mambo kwa kutumia "black filter" ambapo mambo mabaya tu ndiyo yanaonekana.
Mfano: Unapokea maoni kuhusu kazi uliyoifanya unasifiwa mambo mengi lakini pia unapewa mapendekezo madogo ya kuboresha. Ila unazingatia ukosoaji tu na kupuuzia sifa zote nzuri na kuamini ulifanya vibaya.
Polarized Thinking (Black and White Thinking): Kufikiri kwa pande. Huku ni kuona mambo kwa njia mbili nyeupe au nyeusi baya au jema, bila kuwa na katikati
Mfano: Unaweka lengo la kufanya mazoezi kila siku. Unakosa siku moja kwenye mazoezi na kuhitimisha kuwa umeshindwa kabisa na ni bora uache kabisa kufanya mazoezi umeshindwa kwenda siku moja haimaanishi kwamba ni kila siku utafanya hivyo
Overgeneralization: Kutoa hitimisho pana/kubwa zaidi na hasi kulingana na tukio moja au kipande kidogo cha ushahidi. Kwa mfano, kama mtu mmoja hakupendi, unaweza kudhani kwamba kila mtu hakupendi.hii watu wengi wanaipitia na haiwapi amani
Mfano: Unatuma maombi kadhaa ya kazi na hujaitwa popote na unahitimisha kuwa huajiriwi na hutapata kazi kamwe.
Au hujafanya vizuri somo moja unaona kama vile ndio umeshindwa kabisa
Jumping to Conclusions: Kurukia hitimisho hasi bila ushahidi wa kutosha. Hii inaweza kuwa katika mfumo wa kusoma akili yaani "mind reading "(kudhani unajua kile ambacho wengine wanafikiria,hasa vibaya juu yako ) au kutabiri mabaya (kutabiri matokeo mabaya bila uthibitisho wowote).
Mfano wa Kusoma Akili "mind reading: Rafiki yako yuko kimya wakati wa chakula cha mchana. Unadhani amekukasirikia bila kumuuliza,.
Mfano wa Kutabiri Mabaya: Una ripoti labda au presentation na kichwani mwako unawaza utakosea na kila mtu atafikiri huna uwezo, kwahiyo unajikuta una wasiwasi sana
Catastrophizing: Kukuza ukubwa au uwezekano wa matukio mabaya.hapa ni ile kudhani hali mbaya zaidi itatokea kila wakati.
Mfano: Unaumwa kichwa kidogo hapo hapo unaanza kuhisi ishara ya ugonjwa mbaya na unaanza kuogopa.
Mawazo yanaathiri namna unavyojisikia na afya yako ya akili kwa ujumla
Jifunze kwamba si kila unachokiwaza ni sahihi / kina ukweli ndani yake
Mwandishi anasema kwamba
"You are so used to your features you forget how beautiful you look to strangers"-Unknown
Tafsiri yake ni :"Umezoea sana sifa zako kiasi kwamba unasahau unavyoonekana mrembo kwa watu usiowajua"
Itandelea..
Ijayo: Mwandishi anaonya kuhusu tabia anayoiita "self cherishing" anasema "self cherishing is the root of all suffering self cherishing sounds positive but it's more like self obsessing it is a mindset that arises from believing that we are the center of universe and our specific desires goals and wishes are most important"
"You are not the center of universe"
Tafsiri :Kujithamini kupita kiasi ndio chanzo cha mateso yote; kujithamini kupita kiasi inaonekana kuwa ni vizuri lakini ni zaidi kama kujifikiria kupita kiasi; ni mawazo yanayotokana na kuamini kwamba sisi ndio kitovu cha ulimwengu na kwamba matamanio, malengo, na matakwa yetu maalumu ndio muhimu zaidi
Ni kwanini mwandishi anasema hivi? kwanini ni chanzo cha mateso tutaona katika toleo lijalo
Tupe maoni yako katika comments umejifunza kipi?

Join the conversation