Commitment devices
Han Xin alikuwa jenerali mahiri wa kijeshi aliyeshiriki mapambano mengi miaka mingi sana iliyopita Katika moja ya vita vyake maarufu, alikabiliana na jeshi la adui lililokuwa kubwa kuliko lake kwa idadi. Ili kuepusha ile hali ya wao kukimbia kiurahisi alitumia mbinu moja ambayo pia inaweza kukusaidia Han Xin kimkakati aliweka askari wake na mto wenye maji mengi na mamba nyuma yao.
Hatua hii ambayo kimsingi ilikuwa na madhumuni muhimu ya kisaikolojia. Kwa kuondoa uwezekano wowote wa kurudi nyuma, Han Xin aliondoa chaguo la askari wake kujisalimisha au kukimbia. Walielewa kuwa nafasi yao pekee ya kuishi ilikuwa katika kuwashinda audi waliokuwa mbele yao ilikuwa kama "kufa na kupona" iliongeza sana morali na azimio lao la kupigana. Askari walipigana kwa ujasiri na ukali wa ajabu, wakishinda vikwazo na kupata ushindi wa kushangaza.
Ni wazi kwamba wanajeshi hawa walielewa kwamba wanapaswa kushinda ila mara nyingi kama ambavyo wengi hufanya mambo yanapokuwa magumu hukimbia na kukata tamaa hivyo kiongozi wao alihakikisha anaondoa "option" ya kukimbia au kutoroka kabisa
Unaweza ukaitumia mbinu hii kuwa na muendelezo katika tabia zako za kiafya kama vile kufanya mazoezi
1. Unaweza ukawataarifu ndugu zako wa karibu nia yako ya kuanza kufanya mazoezi au jambo ambalo unahitaji kulianza
matarajio yao ya kukuona wewe ukianza mazoezi labda au jambo lolote ambalo umewaambia utalifanya itakusukuma kufanya kile ulichosema
2.Ondoa vyakula ama vitu ambavyo hutakiwi kuvila karibu yako ili usiwe na urahisi wa kuvipata
3.Jiunge na rafiki kuanza program ya mazoezi
4.Unaweza ukakubaliana na mtu kwamba akuchaji kiasi fulani cha pesa endapo hutafanya kile ambacho umemuambia
kwa kuzingatia mbinu hii ya "no retreat" unaweza kupunguza uwezekano mkubwa wa wewe kufanya machaguzi mabaya na itakutengenezea mazingira sahihi ya wewe kuwa mwenye afya zaidi

Join the conversation