Faida za Kiafya za Jamii
Faida za jamii kwa afya ziligunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo miaka ya 1950 katika mji mdogo wa Roseto, Pennsylvania, wakati madaktari wa eneo hilo waligundua kuwa wakazi walikuwa na kiwango cha chini sana cha ugonjwa wa moyo kuliko kilichopatikana katika mji jirani sawa. Baada ya uchunguzi zaidi waligundua kuwa wanaume wa Roseto zaidi ya umri wa miaka sitini na tano walikuwa wanakufa kwa kiwango ambacho kilikuwa nusu ya wastani wa kitaifa, hata ingawa walikuwa wakifanya kazi ngumu sana katika machimbo ya karibu, wakivuta sigara ambazo hazijachujwa, wakila nyama kwa wingi na kunywa divai kila siku.
Kwa nini?
Watafiti walihitimisha kuwa ilikuwa uhusiano thabiti wa kifamilia na msaada wa jamii wa watu walioishi katika eneo hilo la Roseto ambao ulikuwa ukiwasaidia kuimarisha afya zao Utafiti wa mnamo 1992, ambao uliangalia rekodi kamili za afya na kijamii za Roseto za miaka hamsini, ulipata ushahidi zaidi wa nadharia hii.kwa wakati huo, kiwango cha vifo huko Roseto kilikuwa kimepanda kutokana na kuharibika kwa uhusiano wa kifamilia na kijamii na kimila kutoka mwishoni mwa miaka ya 1960 na baadaye. kadiri matajiri zaidi kati yao walivyoanza kuonyesha utajiri wao kwa njia za majivuno zaidi na kufunguliwa kwa maduka makubwa zaidi , na nyumba za familia moja zilizozungushiwa uzio zilipoanza tu kujitokeza ndivyo faida za kiafya ambazo zilipatikana kutokana na muunganiko wa jamii yao zilipopungua.
kikawaida kuna maeneo machache sana duniani ambayo yanaonekana kuwa na watu wenye afya zaidi na wanaonekana kuishi kwa miaka mingi zaidi ukilinganisha na maeneo mengine mengi maeneo hayo hujulikana kama "Blue zones" ambayo mwandishi Dan Buettner ameyaeleza vyema katika baadhi ya vitabu vyake
Baada ya kuzunguka na kufanya tafiti katika maeneo hayo Dan Buettner anasema "Huwezi kutembea nje ya mlango wako wa mbele bila kukutana na mtu unayemjua."
Ni wazi kwamba kipengele cha social health kilikuwa imara sana kwa watu hawa na iliwasaidia kuwa wenye afya zaidi
Join the conversation