faida za kutembea baada ya kula
MBINU HII INAWEZA KUKUSAIDIA KUIMARISHA AFYA YAKO
Kuongezeka mara kwa mara kwa sukari kwenye damu baada ya kula husababisha kuongezeka kupita kiasi kwa insulini na matokeo yake ni usugu wa insulini ama "insulin resistance" hali ambayo ndio mzizi wa magonjwa mengi sugu tunayoyaona sana kipindi hiki kama vile kisukari magonjwa ya moyo na mengine
Katika moja ya tafiti uliofanyika na kuchapishwa katika tovuti ya national institute of health mwanamke wa miaka 60 ambaye alikuwa na historia ya ugonjwa wa kisukari na mwingine mwenye miaka 67 ambaye naye alijitolea katika majaribio ya kuangalia namna ambavyo kutembea kunaweza kukaweka sawa viwango vya sukari katika damu viwango vya sukari katika damu vilipimwa kila mara baada ya kula na vilipimwa walivyotembea baada ya kula na siku ambazo pia hawakutembea baada ya kula na matokeo yake yalirekodiwa
viwango vya sukari katika damu "blood sugar levels" siku ambazo alitembea baada ya kula na siku ambazo hakutembea baada ya kula
| Viwango vya sukari siku ambazo hakutembea | Viwango vya sukari siku ambazo alitembea |
292 | 51 |
217 | 89 |
178 | 99 |
191 | 79 |
wastani=219.5 | wastani=79.5 |
Chanzo :Tovuti halisi ya national institute of health (NIH)
Kuhakikisha chapisho hili angalia hapa bonyeza hapa kuangalia chapisho lao halisi
Baadhi ya faida za kutembea baada ya kula ni hizi hapa
Udhibiti bora wa sukari kwenye Damu: Utafiti ulionyesha kuwa kutembea baada ya kula kunaweza kusaidia viwango vya sukari kwenye damu kupanda na kushuka taratibu zaidi. Hata dakika chache tu za kutembea kwa mwendo wa kawaida kunaweza kuboresha viwango vya sukari kwenye damu ikilinganishwa na kukaa
Usagaji Bora wa Chakula: Kutembea kunaweza kusaidia chakula kupitia mfumo wa usagaji kwa ufanisi zaidi. Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa kutembea baada ya kula kunaweza kupunguza hatari ya matatizo ya mmeng'enyo wa chakula kama vile kiungulia.
Udhibiti wa Uzito: Kutembea baada ya kula kunaweza kusaidia kuchoma kalori, na hivyo udhibiti wa uzito. Utafiti ulionyesha kuwa kutembea baada ya mlo kunaweza kuwa na ufanisi zaidi kwa kupoteza uzito kuliko kusubiri saa moja kabla ya kutembea
Jizoeshe kutembea baada ya kula anza kutembea dakika kadhaa kila baada ya mlo
Muunganiko wa pamoja wa faida hizi utaleta matokeo ya wewe kuwa mwenye afya zaidi
Join the conversation