faida za moringa kiafya
Moringa oleifera hujulikana pia kama 'the tree of life" /"miracle tree" kutokana na faida zake nyingi kiafya tafiti za kifamasia zinaonyesha kwamba zao hili huweza kuwa na uwezo wa kulinda moyo "cardioprotective" kupunguza uvimbe "inflammation" hulinda ini 'hepatoprotective" umeonekana kwamba ni njia nyepesi zaidi ya kupata virutubisho na lishe njema kwa afya na karibu sehemu zote za mti huu zimeonekana kuwa na faida kwa afya .Una beta-carotene za kutosha madini mbalimbali kama vile calcium na potassium ambayo ni muhimu kwa afya
Mti huu unazidi kupata umaarufu kutokana na wingi wake wa virutubisho na faida zinazowezekana kiafya. hapa chini utaona faida hizo:
Unga wa mlonge una vitamini, madini, na kemikali nyingine zenye manufaa, ikiwa ni pamoja zifuatazo
Vitamini: Vitamini A, Vitamini C, Vitamini E, na vitamini vya B (kama B6, riboflavini, na folati).
Madini: kama vile Chuma, calcium potasiam, magnesiam, na zink
Protini: ni moja kati ya mmea unaotajwa kuwa na amino acid zote za muhimu
#amino acids ni vitu vidogo vidogo vinavyoungana pamoja kutengeneza protini
Antioxidants ambazo husaidia Kinga-Mwili: Mmea huu una kemikali kama flavonoids na carotenoids. ambazo husaidia sana kuimarisha kinga ya mwili
Faida za kiafya kwa undani zaidi:
1.Kuongeza Kinga ya Mwili: Una Vitamini C na antioxidants kwa wingi, ambazo husaidia kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili.
pia wingi wa Antioxidants (Kinga-Mwili): Husaidia kuzuia radicals huru hatari mwilini, hivyo kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa sugu.
#free radicals hizi kikawaida huzalishwa mwilini mwako na zinapaswa kuondolewa kwani zinaweza kuleta uharibifu na kusababisha magonjwa sugu
2.Husaidia Kupunguza Uvimbe: Una kemikali ambazo zinaweza kusaidia kupunguza uvimbe.yaani "inflammation"
#Inflammation nao ni mchakato ambao unatokea mwilini mwako mchakato huu ndio unaokusaidia kupona kidonda na hukinga mwili dhidi ya tishio fulani wka muda mfupi hali hii ikiendelea kwa muda mrefu "chronic inflammation" athari yake ni kwamba inasababisha magonjwa sugu
3.Kusaidia kuimarisha usikivu wa insulini: Baadhi ya tafiti zinaonyesha unaweza kusaidia kuboresha usikivu wa insulini hasa kwa watu wenye kisukari cha aina ya pili kwani kwao mchangamoto kubwa ni ukinzani wa insulini kwamba insulini inakuwepo ila haifanyi kazi kwa ufanisi kwahiyo kunakuwa na viwango vikubwa vya sukari mwilini
4.Kusaidia afya ya moyo: Unaweza kusaidia kupunguza kiwango cha chokesterol kwa wale watu wenye kiwango kikubwa cha cholesterol na pia husaidia kupunguza shinikizo la damu.
5.Kupambana na Upungufu wa Damu (Anemia): Chanzo kizuri cha chuma, ambacho ni muhimu kwa utengenezaji wa seli nyekundu za damu.
6.Kuimarisha Mifupa: Una wingi wa madini ya calcium na phosphorus, ambazo ni muhimu kwa afya ya mifupa.
7.Kuboresha Afya ya Ubongo: Antioxidants zinaweza kulinda seli za ubongo dhidi ya uharibifu na hivyo kuimarisha utendaji kazi wa ubongo
8.Husaidia ngozi yenye afya: Vitamini na antioxidants zinaweza kuchangia afya ya ngozi na kuifanya ionekane changa zaidi na mng'ao
9.Unaweza Kukuza Afya ya Tezi Dume: Saratani ya tezi dume ni saratani mojawapo inayoongoza kwa vifo vya wanaume vitokanavyo na saratani mmea huu una baadhi ya kemikali fulani ambazo kupambana na saratani na kusaidia kudhibiti matatizo ya tezi dume kwa wanaume
Zingatia haya:
Ingawa kwa ujumla ni salama kwa kiasi cha wastani, ni muhimu kufahamu madhara yanayowezekana na tahadhari:
na pia elewa kwamba miili yetu imetofautiana hivyo muitikio na kiasi kinaweza kutofautiana pia
kwa watu wenye shinikizo la chini la damu na mapigo ya Polepole ya Moyo: Mlonge unaweza kupunguza shinikizo la damu, ambayo inaweza kuwa tatizo kwa watu wenye shinikizo la chini la damu tayari.
Inashauriwa kupendelea unga wake zaidi na sio sana mizizi
Jinsi ya Kutumia:
Unaweza kuongeza katika
Smoothies (Vinywaji Vilivyosagwa): Unaweza kuongeza kijiko kimoja au viwili kwenye smoothies yako.
Vinywaji: Changanya na maji, juisi
Chakula: Unaweza kunyunyizia kwenye supu,uji, au vyakula vingine.

Join the conversation