Ielewe bipolar disorder

Tatizo la Bipolar "bipolar disorder"

Tatizo la Bipolar changamoto ya akili ambayo husababisha mabadiliko yasiyo ya kawaida katika hisia, umakini, na uwezo wa kutekeleza majukumu ya mtu ya kila siku. Mara nyingi watu wenye tatizo la bipolar hupitia vipindi vya hisia kali. Hizi huitwa "episodes"  kama vile:

  • Mania au hypomania: Hivi ni vipindi vya furaha kupita kiasi hisia za juu "high mood"  mtu anakuwa mchangamfu zaidi lakini Hypomania ni kipindi ambacho mtu anakuwa katika kile ambacho kinaitwa "low moods" uchangamfu unapungua sana   

  • Unyogovu "depresssion": Ni kipindi ambacho mtu anakuwa na huzuni nyingi, kutokuwa na tumaini la maisha

Watu wenye tatizo la bipolar mara nyingi huwa na  wakati mgumu kudhibiti mabadiliko yao ya hisia. Wanaweza kupata mabadiliko ya hisia ghafla sana au kuwa na hisia mbalimbali kwa wakati mmoja

Kipi ni cha kipekee kuhusu bipolar disorder?

Watu wenye matatizo mengine ya kiafya kama vile magonjwa ya moyo kisukari hupitia hisia zinazofanana na hisia zilizotajwa hapo juu wanapopambana na hali zao za kiafya 

wakati mwingine ni ngumu kutambua tatizo hili kwani hisia na mabadiliko ya mood uliyoyaona hapo juu hutokea mara kwa mara hivyo inachukua muda mrefu hadi kufikia hatua ya kusema kwamba mtu ana tatizo hilo na tatizo hili linaweza kuwa tofauti kulingana na namna ambavyo unalitazama "perspective"  japo baadhi ya watu wataona kwamba tabia ya mtu fulani ni tofauti au mwenendo wake umebadilika watu hao wanaweza kuwa na imani tofauti juu ya nini kimemfanya mtu huyo awe hivyo alivyo Angalia kwa umakini mfano huu

Clara ambaye ni mama mwenye watoto wake yupo bize kweli kweli ,kila asubuhi baada ya kuwapeleka watoto wake watatu shule huelekea gym kufanya mazoezi kwa lisaa limoja kila siku baada ya hapo hujiandaa na kuelekea kazini akitoka kazini jioni pia anakwenda na kuwachukua watoto wake toka shuleni huwapikia na baada ya hapo hutumia muda mwingi kufanya mazoezi baada ya wiki mbili alijihisi amechoka sana mara hii anaanza kulala kwa muda mrefu alikiri kwamba hali hii inajirudia rudia (anapitia dalili zote ulizoziona pale juu) 

sasa angalia namna ambavyo Clara ,mama yake na daktari mitazamo yao ilivyo juu ya wanachokipitia Clara anasema kwamba anachokipitia kimesababishwa na majukumu yake kuwa mengi "kulea watoto watatu peke yake ,majukumu ya kazini,kusimamia nyumba yake,kufanya shughuli za nyumbani anasema hana marafiki wa kumsaidia kwa chochote kwahiyo wakati mwingine hujikaza kufanya yote peke yake Mama yake naye anadhani Clara sio muwajibikaji kwamba ni mbinafsi anapenda kufanya mazoezi badala ya kuwalea wanae vizuri 

daktari wake naye anasema Clara ana tatizo ya Bipolar stage ya pili

yupi yupo sahihi? Clara anafikiri hali anayopitia inatokana na mazingira aliyopo na majukumu Mama yake Clara anafikiri kwamba Clara anapitia hali hiyo sababu Mwanae ni mbinafsi (anajali yake tu) na Daktari wake anafikiri kwamba Clara ana tatizo la mood Inamueka matatani Clara kwani yeye anaona anachohitaji ni msaada na wala hana shida zaidi ya hiyo ,mama yake anaona kwamba Clara sio muwajibikaji hivyo anapaswa awajibike zaidi na Daktari wake anafikiria kumpa dawa itakayosaidia kuweka mood yake sawa "mood stabilizers"

Mpaka hapa umeona namna ambavyo tatizo hili linaweza kuwa na mkanganyiko kutokana na mitazamo yetu mtazamo ni muhimu katika kuelewa tatizo hili huenda wakati mwingine mtu hana hata tatizo hili anachohitaji ni msaada tu kama Clara dawa zisingeweza kubadili ukweli kwamba ana majukumu mengi sana yanayomchosha kila siku hivyo tatizo halikuwa katika ubongo wake ila mazingira na majukumu yaliyokuwa mbele yake kila siku yalimfanya aangukie katika hali hii hadi Daktari ahisi kwamba ana tatizo la Bipolar  

Ili kutofautisha Bipolar na mabadiliko ya kawaida ya mood unapaswa kujiuliza maswali yafuatayo

1.Je mabadiliko ya mood yanasababisha matatizo katika maisha yako ya kijamii na kifamilia?

2.Je mabadiliko yako ya mood yanasababisha kupungua kwa utendaji kazi wako kazini?

3.Je mabadiliko yako ya mood yanadumu kwa muda au hubadilika pale kitu kizuri kinapotokea?

4.Je mabadiliko yako ya mood yanakuwa kiasi kwamba unahitaji polisi aitwe kukutuliza au wewe kuwepo hospitalini ?


Chanzo cha Bipolar Disorder


Maswali makuu wanayojiuliza watu ambao wanahisi/wameambiwa hospitalini kwamba wana tatizo la Bipolar ni kwamba "Nimepataje tatizo hili?" na nini kimesababisha? au wengine hurahisisha mambo na kusema kwamba "Ubongo wangu una shida gani?" hapa utaelewa mambo yanayoweza kuchangia tatizo hili la Bipolar

1.Kuwa na historia ya tatizo hili katika familia yenu inaongeza hatari zaidi (lakini haimaanishi kwamba utapata ni kwamba ukikaa kwenye mazingira yanatayotibua tatizo ndio litakuwa rahisi kuonekana na usipokuwa katika mazingira hayo unaweza usipate kabisa tatizo hilo)

cha muhimu cha kuelewa hapa ni kwamba "genetics & biology" pekee haviwezi kujitosheleza kuelezea tatizo hili au kusimama kama chanzo cha pekee 

2.Sababu zingine 



Kufikiria kwamba bipolar disorder ni shida ya ubongo peke yake ni urahisishwaji wa mambo au kufikiria kwamba ni tatizo la kisaikolojia peke yake na kwamba suluhisho ni rahisi pia ni kurahisisha mambo sana na kama tukiwa na aina hiyo ya fikra inaweza ikatuzuia katika utatuaji watatizo hili kwani yapo mengi yanayoweza kuchangia tatizo hili sababu za kibaiolojia zipo na zina mchango wake na mazingira anayoishi mtu ,haiba ya mtu "personality" ,msongo wa mawazo,yana mchango mkubwa sana katika swala zima la Bipolar

kipengele cha genetics chenyewe pia kuna mambo unapaswa kuyaelewa kwamba ikiwa una historia ya tatizo hilo katika familia yenu pia kama nilivyotangulia kusema pale juu sio kwamba ni lazima kwamba utapata tatizo hilo 

tafiti nyingi za watu pacha yaani 'twin studies" zinaweza kutupa mtazamo mwingine pia kuhusu swala ya genetics 

kwa mfano watu mapacha wana "genetic make up " inayofanana kwahiyo ungefikiria kwamba kama mmoja wapo akiwa na tatizo hilo pacha wake naye atakuwa na tatizo hilo sababu ya wote kuwa na genetic make up inayofanana hasa kama ni pacha wanaofanana ambao kwa asilimia kubwa huwa na genetic make up inayofanana 

tafiti za twin studies zinaonyesha kwamba kwa pacha wanaofanana kuna uwezekano wa nusu kwa nusu (50%,50%) kwa pacha mwingine kuwa na tatizo la bipolar kama pacha wake analo tayari hii inaonyesha kwamba japo tatizo la bipolar linachangiwa na  kipengele cha "genetics" lakini kama haliwezi kuwaathiri pacha wote kwa pamoja ikiwa mmoja wapo ana tatizo hilo hapo tunajua kwamba zipo sababu zingine pia ambazo zinaweza kuongeza uwezekano zaidi wa mtu kupata tatizo hili tunaziita "non genetic and enviromental factors) 

 Baadhi ya mambo haya yanaongeza hatari zaidi

1.Maisha yenye msongo zaidi "stressful life" tulichokiona kwa Clara pale juu  ni maisha ambayo yalikuwa na msongo sana kiasi kwamba akaonekana kwamba ana tatizo hili

2.Matumizi ya pombe na madawa ya kulevya

3.Kukosa usingizi wa kutosha

4.Kukosa uendelevu katika matumizi ya dawa hasa kwa watu ambao wameonekana wana tatizo hili na kupewa dawa kutokumaliza dozi kunaweza kukaongeza hatari na ukali wa tatizo

Ijayo 

1.Kwa wanawake pekee :Unachopaswa kuelewa kuhusu bipolar disorder na afya yako

2.Namna ya kukabiliana na bipolar disorder

Endelea kutufuatilia

#Raising healthy generation



Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...