Ielewe uric acid

Katika makala utaelewa nini athari za uric acid nyingi mwilini na pia kwanini uric acid huwa nyingi zaidi kwa wanaume na nini cha kufanya 

Uric acid ni kemikali inayozalishwa mwilini kutokana na mchakato wa kuvunjwa vunjwa kwa vitu vinavyojulikana kama "purines" kama umewahi kusikia vinasaba purines ndizo zinazojenga vinasaba (DNA & RNA) 

baada ya kuvunjwa kwa purines ,uric acid hutengenezwa na hutolewa nje ya mwili wako kwani viwango vya juu vya uric acid vina madhara kwa afya 

Zipo tafiti nyingi zimefanyika kuhusu uric acid na ambacho inaweza kufanya mwilini mwako na katika utafiti mmoja wapo watafiti walijiuliza nini kitatokea kama viwango vya uric acid vikiwa vikubwa mwilini wakawafanyia majaribio panya kwa kuongeza viwango vya uric acid katika miili yao baada ya kufanya hivyo waligundua kwamba viwango vya juu vya uric acid vinaweza kuongeza presha ya damu ,na kupelekea kutokea kwa magonjwa mengine sugu 

tafiti kwa binadamu zinaonyesha kwamba kwa watu ambao walikuwa na viwango vya juu vya presha ya damu baada ya mchakato wa kupunguza uric acid presha ya damu ilirudi katika hali ya kawaida 

Baadhi ya mambo ya mambo yanayochangia uric acid kuongezeka mwilini

  1. Vyakula au vinywaji vyenye sukari nyingi kama vile soda
  2. Vinywaji kama vile pombe
  3. Red meat
  4. Kuwa na uzito mkubwa
  5. Kutokunywa maji ya kutosha huzuia uondoaji wa uric acid 
  6. Magonjwa ya figo 
  7. Magonjwa sugu kama vile kisukari
Matatizo yanayoweza kutokea kutokana na viwango vya juu vya uric acid
  1. Husababisha tatizo linaloitwa gout ambalo huathiri wanaume zaidi
  2. Huongeza hatari ya magonjwa ya figo
  3. Inahusiswa na hatari ya kupata magonjwa  mengine kama vile kisukari,magonjwa ya moyo,shinikizo la juu la damu
kwanini wanaume huwa na viwango vikubwa zaidi?
zipo sababu mbalimbali ikiwemo utofauti wa homoni kwa mfano wanawake wana viwango vikubwa vya homoni ya estrogen ambayo inasaidia kuondolewa kwa uric acid,wanaume pia utakuta kwamba wana misuli na katika misuli kila mara kuna uvunjwaji wa seli hivyo uric acid huzalishwa zaidi kwa wanaume na pia utakuta kwamba wanaume wengi hula nyama zaidi na pombe pia ambazo zinachangia kuongezeka kwa viwango vya uric acid mwilini 

Kuuweka mwili wako katika hali nzuri ni jukumu lako kuchukua hatua fanya yafuatayo ili kuweka sawa viwango vya uric acid 
  1. Zingatia kupunguza ulaji wa vyakula au vitu vinavyoongeza uric acid mwilini kama vile pombe
  2. Punguza ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi na wanga rahisi "simple carbs"
  3. Ongeza ulaji wa matunda na mbogamboga
  4. Kunywa maji kwa wingi
  5. Zingatia kupunguza uzito kama una uzito mkubwa
  6. Zingatia kufanya mazoezi mara kwa mara
  7. Zingatia kupata usingizi wa kutosha
  8. Vitamin C imeonekana kusaidia kupunguza viwango vya uric acid hivyo unaweza ukazingatia vitu vyenye vitamin c kwa wingi matunda kama vile machungwa,limao,berries mbogamboga kama vile brocolli au unaweza ukatafuta supplements zake kuongeza zaidi viwango vya vitamin c mwilini itasaidia pia kupunguza uharibifu wa seli pia hupunguza ufyonzaji wa uric acid katika figo
  9. Ikiwa una ugonjwa wa kisukari jitahidi kuudhibiti pia
  10. Fuata ushauri wa daktari ikiwa umejikuta una viwango vya juu vya uric acid au tatizo la gout zipo dawa ambazo hutumika kwa tatizo hilo


Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...