Tatizo la ED kama ishara ya magonjwa ya moyo kwa wanaume



                                              

Japokuwa ni tatizo kubwa na linazidi kukua kila kukicha Erectile dsyfunction (ED) na ni idadi ndogo ya watu wanaotafuta msaada wa tatizo hili wengi utakuta kwamba wanashindwa kutafuta msaada sababu ya kuona aibu hasa kwani tatizo hili linaonekana kuweza kuathiri mtu anavyoonekana na jamii

japo ukweli ni kwamba mtazamo huo si mzuri kwani ED inaongea mengi kuhusu hali ya kiafya ya mtu 

Japo tatizo hili linaonekana ni la upande wa uzazi tu "reproductive health" ukweli ni kwamba ni muda mrefu umeonekana uhusiano wa tatizo hili na magonjwa ya moyo ukweli huo umeshikiliwa na tatfiti nyingi sana yaani tatizo la ED linaweza kuwa ni kishiria kikubwa cha magonjwa ya moyo

ED ni kifupisho cha Erectile dsyfunction

ED ni nini hasa?

Ni hali ambayo mwanaume anashindwa kusimamisha uume ili kuweza kushiriki tendo linaweza kuwa la muda mfupi au mrefu linasababishwa na mambo mbalimbali kama vile hali ya kiafya ya mtu husika (kama mtu ana magonjwa kama vile kisukari,uzito mkubwa "obesity",shinikizo la juu la damu yote hayo yanachangia tatizo hili),mitindo ya kimaisha kama vile kutokufanya mazoezi,unywaji wa pombe,uvutaji wa sigara,madawa ya kulevya ,sababu nyingine ni za kisaikolojia (msongo wa mawazo,wasiwasi "anxienty",depression matatizo katika mahusiano au hata kile ambacho kinajulikana kama perfomance anxienty" na mwisho ni dawa anazotumia mtu zinaweza kuleta athari mfano dawa kama "anti depressants" dawa kwajili ya matatizo ya tezi dume n.k 

Uhusiano upoje?

ED na magonjwa ya moyo yana uhusiano mkubwa kwani mara nyingi ED husababishwa na tatizo katika mishipa ya damu midogo midogo kwenye uume kikawaida mishipa hii hutanuka na kusinyaa (relaxing and expand) ili kusaidia mzunguko wa damu na kusimama kwa uume 

Katika mishipa ya damu huzalishwa kitu kinachoitwa nitric oxide ambayo ni muhimu sana kusaidia kusinyaa na kutanuka kwa mishipa ya damu ili kusaidia mzunguko mzuri wa damu 

unafikiri nini kitatokea ikiwa kuna shida katika uzalishwaji wa nitric oxide? bila shaka jibu ni kwamba mishipa ya damu itaanza kuathiriwa na pia kutakuwa na tatizo katika mzunguko wa damu na mishipa ya kwanza inayoanza kuathiriwa ni mishipa midogo midogo sana ya damu ambayo moja wapo ni mishipa katika uume ndio maana tunasema kwamba tatizo la ED linaweza kuwa kishiria kikubwa cha tatizo la moyo miaka ijayo kwani linaanza kuonyesha kwamba kuna kitu kimeanza na kinaendelea kuathiri mishipa ya damu na kisipodhibitiwa haraka kitaendelea na kuathiri mishipa mingine ya damu 

Shida katika uzalishwaji wa nitric oxide inaweza kusababishwa na nini?

mambo mbalimbali yanaamua ufanisi wa mchakato mzima wa uzalishwaji wa nitric oxide ikiwemo umri (kadiri unavyozidi kukua zaidi ufanisi unapungua ndio maana hatari ya kupata ED inaongezeka kulingana na umri) ,magonjwa sugu kama kisukari pia yanaathiri sana mishipa ya damu pia matatizo kama vile shinikizo la juu la damu huongeza hatari zaidi ,msongo sugu wa mawazo,

Kwanini ED inaweza kuwa kishiria cha magonjwa ya moyo?

Kama umeelewa pale juu utagudua kwamba mishipa midogo midogo ndio ambayo inaanza kuathiriwa ndio maana inaweza kuwa ni ishara ya kile ambacho kinaendelea mwilini tayari

Muhimu: Ni muhimu kujua kwamba ED sio kwamba ndio kisababishi cha magonjwa ya moyo na sio kwamba wakati wote inaweza ikaashiria tatizo/dalili ya magonjwa ya moyo huko mbeleni kwani tatizo la ED linaweza kuja pia kutokana na hali ya kisaikolojia ya mtu (mfano msongo wa mawazo,uoga au kile ambacho kinajulikana kama performamnce anxienty yanaweza kuchangia ED kwa watu hata ambao hawana shida yoyote ile mwilini)

Je ED ni kishiria kizuri kwa namna gani cha magonjwa ya moyo?

Mpaka hapa umeelewa kwamba ED inaweza kuwa kishiria kizuri cha magonjwa ya moyo tuangalie moja ya utafiti mkubwa uliowahi kufanyika juu ya uhusiano wa ED na magonjwa ya moyo 

Mrejesho wa Meta analysis uliohusisha washiriki takriban 92757 ambao walifatiliwa kwa miaka takriban 6.1 matokeo yake yalionyesha kwamba upo uhusiano mkubwa kati ya ED na hatari ya kupata magonjwa ya moyo waandishi wa utafiti huu waliripoti kwamba dalili za ED zilionekana miaka 2-5 kabla dalili za magonjwa wa moyo kuanza kuonekana na ED sugu zaidi ilionekana kuwa na uhusiano mkubwa zaidi na kuwa kishiria chenye nguvu zaidi 

Rejea utafiti huu : katika website yao "American heart association" kwa kubonyeza hapa bonyeza hapa kuona chapisho halisi la utafiti huu

                                                                     Usipuuzie ED

Japokuwa upo uhusiano mkubwa kati ya ED na matatizo ya moyo bado uelewa katika jamii ni mdogo kwa maarifa haya uliyopata chukua hatua na ikiwa unamfahamu ambaye ameanza kupata tatizo hilo jitahidi kutafuta msaada 

Jambo jema ni kwamba ED inaweza kudhibitiwa kwa mitindo mizuri ya kiafya kama ulaji mzuri,mazoezi,kupunguza uzito,kuacha uvutaji wa sigara na pia zipo dawa pia hutolewa ili kusaidia kupambana na tatizo hili 

Kutafuta msaada ni muhimu sana 


Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...