Kukabiliana na shinikizo la juu la damu
Shinikizo la juu la damu ni chanzo kikubwa cha Matatizo ya moyo na mishipa ya damu matatizo ambayo yanaathiri takribani watu bilioni 1 duniani kote na linazidi kuongezeka kila kukicha
Zingatia kupima mara kwa mara ili kujua hali yako ya kiafya kwani tatizo hili huwa halionyeshi dalili mapema
Ili kuhakikisha presha ya damu inakuwa katika viwango sahihi ni muhimu kuongeza aina ya virutubisho fulani katika mlo wako wa kila siku ambavyo vitasaidia mchakato huo kama ifuatavyo
Virutubisho Muhimu na Vyanzo vyake
1.Potasiam
Potasiamu ni muhimu sana kwani husaidia kusawazisha viwango vya cha sodiam mwilini kwa kufanya hivyo husaidia kudhibiti shinikizo la damu.
Vyanzo vyake ni kama vile Ndizi,Viazi vitamu,mboga za majani,parachichi
2.Magnesium
madini haya husaidia kupumzisha kuta za mishipa ya damu kwa kufanya hivyo damu hutembea vizuri
vyanzo vyake ni kama vile mboga za majani,karanga,mbegu kama vile almonds na mbegu za maboga "pumpkin seeds" vyote hivi ni vyanzo vizuri sana vya magnesium
Tafiti zinaonyesha kwamba muunganiko wa magnesium,potassium na kupunguza matumizi ya chumvi (hasa madini ya sodium) husaidia sana katika kurudisha presha ya damu katika viwango vya kawaida muunganiko huu pia umeonekana kusaidia ufanyaji kazi wa dawa zingine
zingatia muunganiko wa magnesium na potassium kwa pamoja
Rejea :chapisho katika page yao "national institute of health (NIH)"
3.Vyakula vyenye nyuzi nyuzi "fibers"
Vyakula hivi husaidia afya ya moyo na mishipa ya damu kwa ujumla kwa kufanya hivyo husaidia kudhibiti shinikizo la damu
Vyanzo vyake ni kama vile mbogamboga za majani,na matunda,nafaka nzima(oats na mchele kahawia "brown rice)
4.Omega -3
Hivi hasa vinasaidia kupunguza shinikizo la damu virutubisho hivi vinapatikana sana kwenye samaki,chia seed,karanga,
5.Nitrates
Mwilini mwako huzalishwa kemikali inayoitwa nitric oxide ambayo kazi yake kubwa ni kupumzisha kuta za mishipa ya damu kwa kufanya hivyo husaidia sana mzunguko mzuri wa damu
dawa nyingi unazoziona zinatumika hasa kwa wagonjwa wenye shinikizo la damu kwa namna moja ama nyingine zinafanya kazi kama kemikali hii au zinasaidia uzalishwaji wake kwahiyo ni muhimu sana
unazipata wapi?
unazipata katika mlo wako ila haziji moja kwa moja zinakuja kama nitrates ambazo mwilini ndio hubadilishwa na kuwa nitric oxide
Ili kuongeza uzalishaji wa nitriki oksidi mwilini, vyakula Mboga za majani kama ni vyanzo vizuri vya nitrati. Kitunguu saumu huongeza uzalishaji wa nitriki oksidi kwa kuongeza shughuli Matunda kama vile machungwa, limao, na zabibu, pamoja na karanga na mbegu kama walnuts, chia seed, zina virutubisho vinavyosaidia uzalishaji wa nitric oxide mwilini matuinda kama vile Tikiti maji ina kitu kinachoitwa L-citrulline, ambayo hubadilishwa kuwa L-arginine na kisha hubadilihwa kuwa nitric oxide. Nyama, kuku, na dagaa pia husaidia katika kuhifadhi nitric oxide mwilini.
Mbali na hayo zingatia pia haya
- Punguza Sodiamu: Kupunguza ulaji wa sodiamu ni muhimu kwa kupunguza shinikizo la damu.
- Punguza Vyakula Vilivyosindikwa: Vyakula vilivyosindikwa mara nyingi huwa na sodiamu nyingi na mafuta yasiyofaa.ambayo yanachangia kuongeza shinikizo la damu
- Punguza au acha kabisa matumizi ya pombe:matumizi ya pombe yanaweza kuongeza shinikizo la damu.
- Zingatia uzito wa wastani: Kupunguza uzito, ikiwa inahitajika(kama una uzito mkubwa), kunaweza kuboresha shinikizo la damu kwa kiasi kikubwa.
- Fanya mazoezi mazoezi yanasaidia sana kuimarisha mzunguko mzuri wa damu watu wanaofanya mazoezi mara kwa mara wanapunguza hatari ya kupata matatizo ya shinikizo la damu kwa asilimia kubwa
Join the conversation