Kuunda Mazingira Yanayosaidia Kuwa na Tabia Nzuri za kiafya
UNAPOBADILI MAZINGIRA KUNA UWEZEKANO MKUBWA WA TABIA YAKO KUBADILIKA
Kipindi cha vita ya vietnam matumizi ya dawa za kulevya aina ya "heroine" lilikuwa tatizo kubwa sana hasa kwa wanajeshi wengi wao walikuwa watumiaji wakubwa wa heroine walipokuwa katika uwanja wa vita hata wewe ungehofia kwamba wangerudi mtaani wangekuja kuwa mateja na watumiaji wa dawa za kulevya hata serikali yao ilihofia sana kuhusu wao kwamba watakuwa na watu wengi wanaotumia madawa hayo ya kulevya cha kushangaza ni kwamba karibu asilimia 90 ya wanajeshi ambao waliokuwa watumiaji wakubwa wa heroine waliporudi mtaani hawautumia tena heroine walipoondoka katika mazingira yaliyojaa hofu,wasiwasi an walipokuja katika mazingira tulivu na kutengeneza mahusiano mengine iliwasaidia kuondokana na matumizi ya heroine
Walijitoa kwenye mazingira ambayo yalikuwa na vishawishi ambavyo viliwafanya kutumia dawa hizo
Jitoe kwenye mazingira yanayokuwekea vishawishi zaidi kufanya kitu ambacho hukipendi na jiweke kwenye mazingira yanayokushaiwshi zaidi kufanya unachokitaka
Ukilinganisha na ambao hawakwenda vitani wananchi wa kawaida waliokuwa wanatumia heroine na kupata msaada katika vituo vya afya juu ya namna ya kuacha mara kwa mara walijikuta wakirudia tena matumizi ya dawa hizo
Hivyo unapotaka kubadili tabia jitahidi kuyatengeneza mazingira ambayo yatarahisisha wewe kufanya kile unachotaka na sio kile ambacho hukipendi
Kuunda Mazingira Yanayosaidia Kuwa na Tabia Nzuri
Mazingira tunayoishi yana jukumu kubwa katika kuunda tabia zetu. Kwa kufanya mabadiliko madogo katika mazingira yetu, tunaweza kufanya uchaguzi mzuri wa afya uwe rahisi na wa haraka. Hivi ndivyo:
Fanya Chakula Chenye Afya "healthy food" Kionekane na Kipatikane kwa Urahisi
Mfano:Hifadhi vitafunwa vyenye afya sehemu inayoonekana kwa urahisi au kwenye friji
Kwa nini inafanya kazi: Wakati vyakula vyenye afya vinaonekana kwa urahisi, vinakuwa chaguo la kawaida na ni rahisi kuvichagua
Tenga Maeneo kwa ajili ya shughuli Maalum
Mfano: Unda eneo la mazoezi nyumbani lenye vifaa vya mazoezi, au weka sehemu ya kusomea yenye viti vizuri na mwanga mzuri
Kwa nini inafanya kazi: Maeneo yaliyotengwa huunda uhusiano wa kiakili, na hivyo kufanya iwe rahisi kushiriki katika shughuli unayotaka.
Fanya namna urahisishe Kupatikana kwa kile unachokitaka
Mfano: Weka viatu vya mazoezi karibu na mlango, au tumia ngazi badala ya lifti
Kwa nini inafanya kazi: Unapunguza msuguano zaidi mfano kulazimika kutafuta vifaa vya mazoezi
Tumia Viashiria na Vikumbusho Vinavyoonekana kwa urahisi
Mfano: Weka nukuu za motisha ili kuhamasisha tabia nzuri. Weka vikumbusho kwenye simu yako ili kunywa maji au kupumzika au kutoka kukaa muda mrefu
Kwa nini inafanya kazi: Viashiria na vikumbusho vinavyoonekana vinaweza kuchochea tabia unazotaka na kukusaidia kuendelea kuwa sawa.
Boresha Mazingira Yako ya Kulala
Mfano: Fanya chumba chako kuwa katika mpangilio mzuri godoro na mito mizuri
Kwa nini inafanya kazi: Mazingira mazuri ya kulala huchangia usingizi mzuri, ambao ni muhimu kwa afya kwa ujumla.
Mazingira ya Kijamii
Mfano: Jizungushe na marafiki au wanafamilia wanaokusaidia ambao wana malengo sawa na yako ya kiafya. Jiunge na kikundi cha mazoezi
Kwa nini inafanya kazi: Msaada wa kijamii utakusaidia kutoa faraja, uwajibikaji, na motisha ya kushikamana na tabia nzuri. unapowaza kuanza mazoezi siku nyingine tafuta mtu wa kushirikiana naye

Join the conversation