Mambo ya kuelewa kuhusu addiction


Sehemu ya kwanza:Wakati mwingine inatokana na mazingira uliyopo

kipindi cha vita ya vietnam matumizi ya dawa za kulevya aina ya "heroine" lilikuwa tatizo kubwa sana hasa kwa wanajeshi wengi wao walikuwa watumiaji wakubwa wa heroine walipokuwa katika uwanja wa vita hata wewe ungehofia kwamba wangerudi mtaani wangekuja kuwa mateja na watumiaji wa dawa za kulevya hata serikali yao ilihofia sana kuhusu wao kwamba watakuwa na watu wengi wanaotumia madawa hayo ya kulevya cha kushangaza ni kwamba karibu asilimia 90 ya wanajeshi ambao waliokuwa watumiaji wakubwa wa heroine waliporudi mtaani hawautumia tena heroine

walipoondoka katika mazingira yaliyojaa hofu,wasiwasi an walipokuja katika mazingira tulivu na kutengeneza mahusiano mengine iliwasaidia kuondokana na matumizi ya heroine

wakati mwingine badili mazingira ambayo yanakufanya kutumia kitu ambacho unaona umekuwa mraibu wa hiko kitu kubadili mazingira kama kuna mazingira yanayokufanya kila mara kurudia jambo ambalo hulipendi unaweza ukayaaga mazingira hayo inaweza kusaidia

"wakati mwingine ni kwasababu ya kile ambacho unakipitia/ulipo kwenye maisha yako"

 Haya ni baadhi ya mambo yanayoweza kukusaidia/ukatumia kumsaidia anayepambana na uraibu "addiction":

  1. Mazingira uliyopo kwa wakati huo yana mchango mkubwa sana linapokuja swala la uraibu: Kuhusu hawa wanajeshi umeona kwamba unaona kuwa mazingira yaliyojaa msongo, hofu, na wasiwasi ya Vita vya Vietnam inawezekana yalichangia sana matumizi ya heroini kwa wanajeshi.na waliporudi katika mazingira tulivu na yenye msaada zaidi, kichocheo cha uraibu wao kiliondolewa kwa kiasi kikubwa, na kusababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa matumizi. Hapa unajifunza kwamba kama kuna uraibu ambao umekuwa ukipambana nao kwa muda mrefu unaweza kufaidika sana kwa kubadilisha mazingira ambayo yanakuchochea zaidi kwenda kwenye mazingira ambayo hayachochei zaidi kufanya jambo ambalo hulipendi  

  2. Mahusiano ya kijamii na msaada ni muhimu sana ili kupona: Umejifunza kwamba kuunda mahusiano mapya katika mazingira tulivu kuliwasaidia wanajeshi kushinda matumizi yao ya heroin.na hii inasisitiza zaidi kuhusu umuhimu wa mahusiano chanya ya kijamii na mfumo mzuri wa msaada katika mchakato wa mtu kupona.kuwa na kusudi ambalo linaweza kuchukua nafasi ya uhitaji wa kile ambacho kinakusababishia uraibu 'addiction" badala ya kupambana mwenyewe tafuta msaada"

  3. Uraibu Unaweza kutokana na mazingira uliyopo kwa muda huo: Ukweli kwamba idadi kubwa ya wanajeshi waliacha kutumia heroini waliporudi nyumbani hapo unaona kwamba uraibu wao, kwa kiasi kikubwa, ulihusiana na hali mahususi waliyokumbana nayo Vietnam. kwahiyo kama unapambana na uraibu ikupe matumaini kwamba uraibu unaweza kuwa si tabia ya ndani isiyoepukika, bali ni mwitikio wa hali wanayopitia sasa na kubadilisha hali hiyo kunaweza kusababisha mabadiliko makubwa katika tabia zao za uraibu.

  4. Wakati mwingine kuacha mazingira yanayochochea ni uhimu:  Yaage mazingira ambayo kila mara unajikuta yanakuletea tabia usiyoitaka ikiwa mtu aliye na uraibu anajikuta akirudia tabia hiyo mara kwa mara kwa sababu ya maeneo, watu yanaweza kuwa muhimu kujiondoa kwenye mazingira hayo ili uweze kuvunja mzunguko wa uraibu.

  5. Swali la msingi ni kwanini umejikuta katika hali hiyo: wakati mwingine sababu ni kile ambacho unakipitia/hali ya kimaisha kwahiyo jambo la muhimu sio tu kuacha matumizi ya vitu kama vile "pombe' 'sigara" au chochote ambacho unahangaika kukiacha ila inakuwa ngumu zaidi unachopaswa kushughulikia na swali la kujiuliza ni "kwanini uraibu?"

Safari ya kupambana na "addiction" inahitaji msaada usipambane peke yako




 

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...