Njia 3 za Kupata Ufunguzi/Hitimisho
Njia 3 za Kupata Ufunguzi/Hitimisho
Ingawa Closure ni hali ya binafsi sana, hapa njia za kukusaidia kuipata au kutatua
Shughulikia hisia zako kwanza
Kubali hisia zako: Jipe ruhusa kuhisi hisia zozote zinazojitokeza, iwe ni huzuni, hasira, au kuchanganyikiwa. usijaribu kuzipuuza kuziepuka kutakufanya uumie zaidi
Jieleze: Tafuta njia zenye afya za kueleza hisia zako. Hii inaweza kuhusisha kuandika "journalling" kuzungumza na mtaalamu au rafiki unayemwamini, kushiriki katika shughuli unazozipenda au kufanya mazoezi ya mwili.
Jijali: Kuwa mwema na mwelewa kwako mwenyewe(Ingekuwa ni rafiki yako anatafuta msaada kuhusu closure ungemuambia nini? au ungemsaidia nini? fanya hiko ) Tambua kwamba ni sawa kuhisi jinsi unavyohisi, na uponyaji/wewe kuwa sawa kunachukua muda.
Tafuta Uelewa wa hali halisi
Tafakari hali hiyo: Jaribu kuelewa kilichotokea. Matukio gani muhimu yalitokea? Jukumu lako lilikuwa nini, na jukumu la mtu mwingine lilikuwa nini? kuelewa majukumu kutakusaidia kupunguza maumivu zaidi huenda unaumia kwa jukumu ambalo halikuwa lakwako
Tambua uliyochojifunza: Fikiria ni nini unaweza kujifunza kutoka kwa uzoefu huo. Umekubadilisha vipi? Ungefanya nini tofauti katika siku zijazo?
Chukua Udhibiti wa Kile Unachoweza (kile ambacho kipo ndani ya uwezo wako)
Weka mipaka: Ikiwa ukosefu wa closure unatokana na uhusiano, inaweza kusaidia kuweka mipaka na mtu huyo mwingine. Hii inaweza kuhusisha kupunguza mawasiliano, kukomesha uhusiano, .
Zingatia zaidi sasa na wakati ujao(usiendeshwe na yaliyopita peke yake): Ingawa ni muhimu kushughulikia yaliyopita, usiruhusu yakutawale. Hamisha umakini wako na nguvu zako zaidi kwa kile unachoweza kudhibiti sasa na kile unachotaka kufikia wakati ujao.
Join the conversation