Pop corn brain ni nini?
Pop corn brain ni nini?
Huenda umeshuhudia tabia yako ya kutazama simu yako kila mara inazidi kuongezeka Unaona jinsi kadri muda unavyozidi kwenda ugumu wa kufanya jambo moja kwa muda mrefu bila kuwa "distracted" unazidi kuongezeka hizo ni baadhi tu ya kile ambacho alikieleza mtafiti David Levy alipokuja na neno "pop corn brain"
Ni neno lililoanzishwa na David Levy, mtafiti katika Chuo Kikuu cha Washington mnamo 2011 kuelezea kinachotokea kwenye ubongo wetu tunapotumia muda mwingi sana mtandaoni kwamba inaweza kuathiri utendaji kazi na ufanisi wetu wa kila siku mfano mtu anakuwa na mawazo yaliyotawanyika, umakini uliogawanyika na mwelekeo wa akili kuhama kwa haraka kutoka kwenye kitu kimoja kwenda kingine, akifananisha hali hiyo na mlipuko wa haraka wa punje za popcorn kwenye sufuria moto
Unaangali simu yako mara ngapi kwa siku?
Tafiti zinaonyesha kwamba kwa kawaida ni mara 160 na zaidi kwa siku pia vitu kama "swipe,tap ,scroll,clicks" ni mara 2617 kwa siku na watumiaji mahiri hufanya "swipe,tap ,scroll,clicks" hadi mara 5,427 kwa siku
Kwa kufanya hivi ubongo unazoea na inakuwa rahisi zaidi kuwa distracted na kupunguza uwezo wako wa kuweka umakini katika kazi moja hadi iishe
Dalili za "Popcorn Brain"
Hali hii imechangiwa sana na matumizi ya vifaa vya kidigitali kwani tumezungukwa na viichocheo vingi hasa vya kidijitali wakati wote
Kadiri muda wetu wa kutumia screens(hasa simu) na msongo wa mawazo unavyoongezeka, inaweza kuwa vigumu kutambua baadhi ya dalili za kawaida za "popcorn brain" kwani zinaanza kuonekana "kawaida". Lakini ingawa ni za kawaida, sio za kawaida.
Dalili hizi zinaweza kujumuisha:
Kupungua kwa muda wa kuzingatia (jiulize unaweza kufocus kwa muda kiasi gani kwenye jambo moja bila kuhama hama? attention span inazidi kupungua na uwezo wetu wa kuweka mkazo katika jambo moja na kulimaliza unazidi kupungua
Ugumu wa kuzingatia
Mvurugiko wa hisia
Ubora duni wa usingizi "poor sleep quality"
matokeo yake ni kupungua hata kwa ufanisi kazini au hata shuleni
Madhara yake ni yapi hasa?
Katika kitabu chake cha Stolen Focus: Why You Can't Pay Attention—and How to Think Deeply Again, Johann Hari anachunguza sababu za kupungua kwa uwezo wetu wa kuzingatia. Anataja utafiti, kama vile kazi ya mtafiti wa Chuo Kikuu cha California, Gloria Mark, ambaye, katika kitabu chake Attention Span: A Groundbreaking Way to Restore Balance, Happiness, and Productivity aligundua kuwa wastani wa muda wa kuzingatia umepungua kutoka dakika 2.5 mwaka 2004 hadi sekunde 47 tu katika miaka ya hivi karibuni. Hari anasema, kama Mark, kwamba kudhoofika huku kwa umakini, kunakosababishwa na sababu mbalimbali, hakupunguzi tu ufanisi bali pia huongeza msongo wa mawazo kwa kiasi kikubwa, kwani kubadilisha umakini mara kwa mara huongeza mkazo wa kiakili
Uwezo wa kuweka umakini na uwezo wetu wa kuzingatia mambo unazidi kupungua jaribu kufikiria jambo ambalo uliwahi kulifanya kwa mafanikio makubwa labda ni masomo au kusoma kitabu na kukimaliza au hata wewe kuisoma makala hii na kufika hapa imechangiwa sana na uwezo wako wa kuzingatia "ability to pay attention and focus" na uwezo huo unazidi kupungua unafkiri utaweza kufanya mambo ya muhimu kwa ufanisi tena?
mitandao ya kijamii ina taarifa nyingi na inataka kutulisha taarifa hizo kila dakika kuifanya iwe changamoto kwa watu binafsi kuchakata taarifa hizo ubongo hushambuliwa na jumbe mbalimbali kila wakati hivyo uwezo wetu wa wetu wa kuzingatia kazi mojaumepungua na unazidi kupungua Mrundikano wa taarifa nyingi pia huathiri uwezo wetu wa kukumbuka kujifunza na kufanya udhibiti wa hisia zetu na kufanya maamuzi
Linapokuja swala la mapambano kati yako na distractions mara nyingi distractions zinashinda sio kosa lako na haimaanishi kwamba wewe ni mdhaifu huenda ni mbinu unayoitumia umejaribu mbinu nyingi kupambana na hali niliyoelezea hapo juu au ikiwa ndio unatafuta ni nini ufanye? zipo mbinu nyingi zinazoweza kukusaidia na zitaelezewa katika machapisho yajayo ila leo nikuachie hii moja inaweza kukusaidia kwa kuanzia
Jambo la muhimu la kuelewa unapoanza safari ya kupambana na distractions ni kwamba kwa hali ilivyo hivi sasa na uhusiano wetu na vifaa kama vile simu mapambano ya peke yako mara nyingi yatagonga mwamba jitahidi uwe na rafiki ambaye mmeambizana kupambana na distraction
#Tokomeza pop corn brain
Mbele hapa nimeeleza aina za distractions
Aina za distractions tunazokutana nazo kile siku
1.External distractions hizi ni zile ambazo tunakutana nazo kutokana na vitu vya nje kama vile simu watu aina hii ni rahisi kukabiliana nayo kwani unaweza ukahama au kuviondoa vitu ambavyo vinakuletea usumbufu na kukuondoa katika kazi unayoifanya mfano kelele za watu walio karibu yako zinaweza kukufanya ukapoteza focus hivyo unaweza ukahamia sehemu nyingine
2.Internal distractions
Umeshawahi jikuta upo kwenye kikao au darasani ukajikuta unaangali simu kila mara sababu ya kuhisi kuboeka au kuwa na wasiwasi wa nini kinachotokea mtandaoni kwa kutaka kujua kinachoendelea unajikuta unaangalia simu yako mara kwa mara
Hii inachangia asilimia kubwa ya distraction tunazokutana nazo na zinazopunguza ufanisi wetu ni vitu kama vile stress hisia za upweke kuboeka hofu haya hutufanya tuwe distracted kila mara
kwahiyo hapa unahitaji kukabiliana vyema na "internal discomfort" unapaswa kukabiliana na hali kama hizo njia moja wapo ni hii mfano upo unafanya jambo moja alafu unakumbuka kuna mtu ulipaswa kumtafuta unaanza kupata wasiwasi na unatamani uache kile unachokifanya uli umtafute mtu huyo badala yakeunaweza ukaweka katika diary yako kwamba utamtafuta baada ya kumaliza kazi hiyo kwa kufanya hivyo utaendelea kwa utulivu na kazi ambayo ilikuwa mbele yako
katika machapisho yajayo tutaangazia zaidi mbinu zingine za kukabiliana na distractions
Join the conversation