sehemu ya pili

SEHEMU YA PILI  

7. THEY DON’T MAKE THE SAME MISTAKES OVER AND OVER &  THEY DON’T GIVE UP AFTER THE FIRST FAILURE

Tafsiri yake :Hawarudii makosa yale yale kila mara na pia hawakati tamaa baada yakushindwa mwanzoni

 The only real mistake is the one from which we learn nothing. -JOHN POWELL

kuhusu makosa mwandishi anasema kitakachosaidia ni 

kukiri kwamba tumekosa 

kuangalia namna ya kutokurudia kosa kuelewa mambo yaliyotufanya tukosee na kuyaepuka huko mbeleni 

kuhusu makosa mambo haya hayawezi kusaidia

kuleta visingizio vya kwanini umekosa au kukataa kukiri kosa lenyewe 

kujiweka katika nafasi ya kukosea na kujifanya kwamba tunaweza kushinda majaribu na mwsihowe unakosea tena 

Kuhusu makosa tunapaswa kukubali ukweli huu kwamba ukiangalia mara nyingi ambapo ulijitetea sana kuhusu jambo fulani ukitulia na kuwaza vizuri utagundua kwamba ulikuwa unahusika ila ulitumia visingizio kukimbia majukumu 

 8. THEY DON’T RESENT OTHER PEOPLE’S SUCCESS 

Tafsiri yake : Hawaonei wivu mafanikio ya watu wengine/Hawachukii kufanikiwa kwa wengine.

Mwandishi anamnukuu Nelson Mandela "Resentment is like drinking poison and then hoping it will kill your enemies"

kwamba kufanya hivyo ni kama kunywa sumu na kutegemea kwamba itamuua adui yako

mwandishi ameweka wazi kwamba jealous ni kusema “I want what you have,” nataka ulichonacho na resentment ni kusema kwamba nataka ulichonacho na sitaki wewe uwe nacho

je moja wapo ya sifa hii inaonekana kwako? unajilinganisha kila mara (hadhi yako,vitu,muonekano) na watu wengine? ni ngumu kwako kuweza kuwasikiliza wenzako wakielezea mafanikio yao? unahofu kwamba wenzako watakuona kama mpotezaji/uliyefeli "loser"? unaona aibu juu ya kukosa kwako mafanikio?

kwanini tunajifananisha na watu wengine? ni swali la kujiuliza 

Kujifananisha kila mara kunaweza kukuletea hisia za kutokutosheleka na kukosa amani ya ndani na kunasababisha wakati mwingine kuwa na hasira juu ya wengine

Ni muhimu kujifunza kufurahia matokeo ya wengine na mafanikio yao na kujifunza toka kwao

9. THEY DON’T FEAR ALONE TIME 

 All man’s miseries derive from not being able to sit quietly in a room alone. —BLAISE PASCAL

Tunaishi katika kipindi ambacho tunaogopa kuwa peke yetu (kumbuka upo utofauti kati ya kuwa peke yako na kuwa mpweke)

kila wakati tupo mtandaoni wengi wanapitia hofu ambayo imepewa jina la FOMO -fear of missing out kwamba tunaogopa kupotea mtandaoni 

unaweza ukabisha kwamba huna FOMO lakini ili uielewe FOMO ni kile ambacho kinatokea simu yako inapokaribia kuisha chaji na umeme umekata laptom nayo imeisha chaji na unalazimika kukaa masaa mawili kusubiri umeme urudi kwa asilimia kubwa hofu na mhemko unaopitia muda huo ndio unaoitwa FOMO 

tunaogopa "missing out" tupo na simu zetu kila mahali hadi unapokwenda uani upo nayo na unaendelea kuperuzi,unaogopa "missing out" tunajiskia vibaya kukaa bila kufanya chochote 

Amy anatuambia kwamba watu hao hawaogopi muda wa kukaa peke yao mwandishi ametaja baadhi ya watu katika dini kubwa duniani kama Vile Yesu,Mtume Muhammad,Buddha wote hao walionekana mara nyingi wakipata muda wa kukaa peke yao kwa utulivu 

mwandishi anatuambia tuwe na ujasiri wa kukaa peke yetu hata kwa muda mfupi anasema tu "SCHEDULE A DATE WITH YOURSELF" kutafakari kuhusu maendeleo yako ulipofikia na unapoelekea,

10. THEY DON’T FEEL THE WORLD OWES THEM ANYTHING 

Tafsiri yake:Hawatarajii ulimwengu kuwapa chochote.

 Don’t go around saying the world owes you a living. The world owes you nothing. It was here first. —ROBERT JONES BURDETTE

Hii inaelezea watu ambao wana mtazamo wa unyenyekevu na uhalisia kuhusu maisha. watu wanaofahamu kuwa mafanikio, furaha, na bahati nzuri haviwezi kuhakikishwa au haviwezi kupatikana moja kwa moja. Badala ya kuhisi kuwa wana bahati ya kupata matokeo chanya, wanachukua jukumu la maisha na matendo yao. Hawaulalamikii ulimwengu au watu wengine wakati mambo hayaendi sawa.

mwandishi anasema kwamba mtazamo huo utatuweka katika Matarajio yasiyo ya kweli,Ukosefu wa shukrani: sababu watu wanapohisi wanastahili mambo fulani, wanaweza kushindwa kuthamini juhudi za wengine au thamani ya kile walicho nacho. Hii inaweza kusababisha uhusiano uliojaa misukosuko na ukosefu wa shukrani kwa ujumla.ugumu wa kukabiliana na shida: Hisia za kustahili zinaweza kufanya iwe vigumu kukabiliana na vikwazo, kushindwa, au kukosolewa

moja ya kitu mwandishi anasema ni kwamba kutokuhesabu "dont keep score" ushazoea unahesabu watu waliokusaidia na unategemea kusaidiwa tena hapo baadae ukweli ni kwamba inaweza isiwe hivyo na kama ukiendelea na mtazamo huo utahuzunishwa sana

Unyenyekevu utakufanya uwe imara zaidi

11. THEY DON’T DWELL ON THE PAST & THEY DONT FEAR TAKING CALCULATED RISK

Tafsiri yake:Hawaishi katika mambo yaliyopita

 "We do not heal the past by dwelling there; we heal the past by living fully in the present."—MARIANNE WILLIAMSON

mwandishi ameweka wazi kwamba hatuwezi kupona kama tutaendelea kuyaishi yaliyopita 

Je unatamani kama ungeweza kugeuza yaliyokupata huko nyuma ? Unatumia muda mwingi kuwaza kwamba kama ninge....." 

aina hiyo ya mawazo yatakuzuia kuishi vizuri katika wakati uliopo yatakufanya uhisi kwamba huna unachoweza kukifanya 

hivyo unaweza ukachagua kuwekeza zaidi nguvu zako katika wakati uliopo na kama ulielewa pale juu kwenye namba 4 mambo yaliyopita pia yapo nje ya uwezo wako huwezi kurudi na kuyabadilisha tena ila unaweza ukaamua hali yako ya sasa hivi

MWISHO

 

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...