Stress na udhibiti

Yote yanaangukia kwenye uwezo wa udhibiti. Wanasayansi wamekuwa wakisoma msongo wa mawazo kwa miaka mingi sasa na matokeo yapo wazi:mara nyingi si msongo wa mawazo wenyewe unaotulemea, ni ukosefu wa udhibiti

Bila shaka kuna siku ulilemewa na stress leo kuna kitu utajifunza ambacho kitakusaidia hasa katika kudhibiti msongo wa mawazo

Wanadamu sio viumbe pekee wanaopata msongo "stress" zaidi ikiwa hawana udhibiti.utafiti uliofanywa kwa panya, mbwa, nyani, na wanyama wengine unaonyesha wazi kwamba msongo usioweza kudhibitiwa ni hatari zaidi kwa ubongo, mwili, na tabia ya viumbe wengine ukilinganisha na msongo unaoweza kudhibitiwa

Hii inatupa picha kwamba wote tunaweza tukakutana na msongo "stress" lakini athari yake ikatofautiana kutokana na uwezo wetu wa kuidhibiti kwahiyo jambo la muhimu sana sio stress ila uwezo wako wa kuidhibiti

Katika utafiti mashuhuri wa kile ambacho wasaikolojia hukiita "learned helplessness" (kujifunza kutokuwa na msaada) (Seligman na Maier 1967), mbwa walitengwa katika makundi mbalimbali na waliwekwa kwenye hali ya kupata mshtuko "shoti" ya umeme katika vyumba vidogo "cages" ila baadhi ya mbwa walikuwa na kitu ambacho wakikibonyeza wanaweza kuzima shoti ya umeme (kwa maana kwamba waliweza kuidhibiti shoti) vikundi vingine vya mbwa hawakuwa na kifaa hiko hivyo shoti kwao hawakuweza kudhibiti shoti hiyo matokeo yake ni kwamba Ingawa vikundi vyote vilipata kiwango sawa cha mshtuko kwa ujumla, mbwa waliopata mshtuko usioweza kudhibitiwa walionyesha msongo zaidi. Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba mbwa walipowekwa baadaye kwenye kisanduku ambacho wana uwezo wa kutoroka endapo shoti ikitokea kwa kuruka juu ni wale tu waliokuwa wamepata mshtuko unaoweza kudhibitiwa hapo awali ndio walijifunza kwa mafanikio namna ya kutoroka. Mbwa ambao walikuwa wamepata mshtuko usioweza kudhibitiwa hapo awali hawakuweza kutoroka mshtuko huo.

na zaidi sana watafiti waligundua kwamba stress zisizotarajiwa pia zina madhara zaidi ya zile ambazo zinatarajiwa na zile zinazokuja katika majira ambayo yanatabirika 

Watafiti walieleza kuwa mbwa katika hali ya mshtuko usioweza kudhibitiwa walikuwa wamejifunza hapo awali kwamba tabia zao au chochote wanachofanya hakiwezi kuwaondoa katika taabu ya shoti kwa hivyo waliacha kujaribu. Na hivyo hata walipowekwa katika vyumba ambavyo wanaweza kutoroka kiurahisi hawakujifunza kamwe kuwa hali zilikuwa zimebadilika na kwamba kutoroka sasa kulikuwa ndani ya uwezo wao. Profesa Seligman aliamini kwamba matatizo haya katika kujifunza na motisha yalikuwa sawa na yale yanayopatikana kwa watu wenye huzuni. Alipendekeza kwamba "learned helplessness" inasababishwa na msongo usioweza kudhibitiwa katika maisha ya awali

Bila shaka uelewa huu umebadili mtazamo wako juu ya msongo wa mawazo sivyo? Yanabadilisha jinsi unavyofikiria kuhusu msongo wa mawazo

Muhimu ni kujenga hisia za udhibiti. Anza kidogo, tambua maeneo ambayo unaweza kuleta mabadiliko, na ujenge kutoka hapo.

mara nyingi unapokutana na hali ngumu ni rahisi kukata tamaa kama unaona huna ambacho unaweza ukakifanya hali hiyo itakuathiri zaidi badala yake unaweza ukaangalia kile ambacho unaweza ukakifanya kuhusu jambo lililopo mbele yako inaweza ikawa ni kumtafuta mtu anayeweza kukusaidia.

Una maoni gani kuhusu "learned helplessness? Umewahi kukumbana nayo?

Kama ambavyo imebadili uelewa wako juu ya stress share na mwenzako naye imsaidie

Tuanzishe mazungumzo kuhusu kurejesha udhibiti wetu juu ya stress


Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...