Suluhisho :Part 1
Mara nyingi tunaona ushauri kuhusu nini cha kufanya unakuwa mrahisi sana kwamba zingatia mitindo mizuri ya kiafya bila kuelezwa kwa undani nini ufanye na kwa nini natumaini utaelewa na sasa utajua pa kuanzia moja ya changamoto kubwa ni hii hapa na suluhisho lake kwa undani
Matatizo katika mzunguko wa damu
Moja ya adui mkubwa wa afya sio tu ya uzazi ila afya ya mtu
kwa ujumla ni mzunguko mbovu wa damu ‘poor blood flow” na mzunguko ukiwa mbaya
sehemu moja ya mwili inawezekana kabisa ni kote kuna tatizo hilo mzunguko unapokuwa
mbaya
Kwa mfano ili uume usimame vizuri ni lazima mzunguko wa damu
uwe mzuri pia ikitokea mtu ana matatizo kama vile magonjwa ya moyo,hafanyi
mazoezi mzunguko wa damu utakuwa na shida ndio utaskia anashindwa kusimamisha
uume vizuri “erectile dysfunction” na
kulingana na tafiti asilimia kubwa ya wanaume wanaopitia tatizo hili wana
hatari ya kuja kupata matatizo ya moyo mara nyingi matatizo ya mishipa mishipa
midogo ndiyo inayoanza kuathiriwa zaidi
Yaani kama mishipa midogo kwenye uume imeanza kutokufanya
kazi vizuri unategema baada ya muda mishipa mikubwa nayo itaanza kuathiriwa magonjwa
kama vile kisukari pia huleta uharibifu katika mishipa ya damu na idadi ya watu
wanaopata ugonjwa wa kisukari na pia uzito mkubwa inazidi kuongezeka
Kazi nyingi ambazo tunazifanya zinatufanya tukae kwa muda
mrefu hupati muda wa kufanya mazoezi na likija swala la mzunguko wad amu mazoezi
ni muhimu sana kwani yanasaidia mzunguko mzuri wad amu,yanasaidia kuzuia uzito
mkubwa,kupunguza hatari ya ugonjwa wa kisukari na magonjwa ya moyo.
Katika suluhisho tutaona nini ufanye ili kuimarisha mzunguko
mzuri wa damu
1.Epuka chochote ambacho kinadhuru mishipa ya damu
Kutokufanya mazoezi,kutokunywa maji ya kutosha
2.Tafuta matibabu ya tatizo lolote ambalo linalosababisha mzunguko
mbaya wa damu
Kuwa serius kuhakikisha unakuwa na mkakati wa kuthibiti
matatizo kama vile kisukari (diabetes & pre diabetes),magonjwa ya moyo,matatizo
ya presha ya damu,tatizo la kukosa usingizi “insomnia”,matumizi ya pombe wote hawa
ni maadui wa mzunguko mzuri wa damu na mzunguko mzuri wa damu ni muhimu kwa
afya yako ya uzazi (uzalishwaji wa homoni ,ukuaji wa seli mbalimbali,”strong erections”)
3.Punguza uzito
Ikiwa kipimo cha BMI kimezidi 25 (Unaweza ukaangalia namna
ya kukokotoa kwa kuchukua uzito wako (kg) gawanya kwa (urefu*urefu) mfano kama
una kilo 80 na urefu wa mita 2 kwahiyo BMI=uzito/(urefu*urefu)
BMI=80/(2*2)
BMI=20
Kama yako imezidi 25 jitahidi upunguze uzito uzito mkubwa
nao ni adui mkubwa sio tu wa mzunguko wa damu ila hata homoni kama vile testosterone
ambayo ni muhimu sana katika kuleta hamu ya tendo”sex drive”,uzalishwaji wa
mbegu za kiume, na kazi zingine nyingi
Uzito mkubwa unapelekea viwango vidogo vya homoni hii unafikiri
homoni hii ikiwa kwa uchache nini kitatokea?
Amua upunguze uzito au la
4.Zingatia mikakati ya asili kuhakikisha presha na mzunguko wa
damu unakuwa vizuri
·
Kula mbogamboga na matunda kwa wingi vitu hivi
vinasaidia utengenezwaji wa “nitric oxide” mwilini ambayo inasaidia kulegeza
mishipa yad amu “relax blood vessels” hivyo husaidia mzunguko wa damu kufanyika
kwa urahisi zaidi
·
Ondoa kabisa /punguza unywaji wa pombe tafiti za
hivi karibuni zinaonyesha kuwa hakuna kiwango ambacho ni salama kwako na pia
punguza matumizi ya
· Kunywa maji ya kutosha kila sik
5.Zingatia vyakula ambavyo vinasaidia kuweka presha ya damu katika viwango sahihi
·
Zingatia vyakula vyenye magnesium ya kutosha
magnesium inafanya kazi pia ya kulegeza mishipa ya damu “relaxing blood vessels”
hivyo husaidia mzunguko mzuri wa damu mboga mboga za majani ,matunda kama vile
parachichi yatasaidia kuongeza magnesium mwilini mwako pia vitu vingine kama
vile almonds,mlonge “moringa”,chia seeds, mbegu za maboga “pumpkin seeds” vina
magnesium ya kutosha
Tafiti zinaonyesha kwamba viwango vya chini vya magnesium vinaongeza hatari zaidi ya matatizo kama vile "erectile dsyfunction"
5.Fanya mazoezi
Mazoezi ya mara kwa mara yana boost ile nitric oxide ambayo tuliona inasaidia kuimarisha mzunguko mzuri wa damu tafiti zinaonyesha kwamba mazoezi ya mwili ya mara kwa mara, hasa mazoezi ya aerobic(kukimbia,kutembea,kuruka kamba), yanaweza kuboresha nguvu za kiume na kupunguza hatari ya upungufu wa nguvu za kiume (ED) pia mazoezi yatakusaidia kuimarisha balance ya homoni mwilini mwako
6.Vyakula vya kuzingatia zaidi
Zingatia vyakula vyenye fibre ya kutosha ,vyakula vyenye vitamin E,K,B ya kutosha pia vyakula vyenye omega -3 ya kutosha kama vile Samaki hizi zitasaidia sana katika kuimarisha afya ya mishipa ya damu
Changua kitu kimoja wapo hapo juu anza kukizingatia kuanzia leo
Machapisho yajayo yataeleza kuhusu vipengele vingine na nini cha kufanya
Stay tuned
Join the conversation