Tunawezaje kushida katika nyakati ngumu za maisha

 


Victor Franklin ana mengi ya kutufundisha kuhusu nyakati ngumu na nini tunaweza kukifanya nyakati hizo. 

 Frankl, daktari wa neva na mtaalamu wa saikolojia kutoka Austria, alivumilia mateso yasiyofikirika wakati wa Holocaust. Mnamo 1942, yeye, mke wake, na wazazi wake walisafirishwa hadi kwenye kambi za mateso ( Nazi camps) . Katika kipindi cha miaka mitatu iliyofuata, alifungwa katika kambi nne tofauti, Baba yake alifariki huko ,mama yake na kaka yake waliuawa pia , na mkewe pia alifariki katika misukosuko hiyo 

Alipoteza karibu kila kitu isipokuwa kimoja ambacho atatueleza hapo mbele 

 Victor aliweza kujua ni nani anayekwenda kufa kwa kuangalia tu!

Katikati ya hali mbaya ya kila siku ya kupigwa, njaa, na tishio la mara kwa mara la kifo, Frankl aliona jinsi wafungwa wengine waliweza kuishiwakati wengine walikufa na aligundua kwamba wale waliokuwa na hisia za kusudi "sense of purpose" Na sababu ya kuendelea kuishi walikuwa na uwezekano mkubwa wa kuvumilia mateso. 

Alisema kwamba  

"Sisi tuliokaa katika kambi za mateso tunaweza kuwakumbuka wale watu waliotembea kupitia vibanda wakiwafariji wengine, wakitoa kipande chao cha mwisho cha mkate. Huenda walikuwa wachache kwa idadi, lakini wanatoa ushahidi tosha kwamba kila kitu kinaweza kuchukuliwa kutoka kwa mtu isipokuwa kitu kimoja: uhuru wa mwisho wa kibinadamu -- kuchagua mtazamo wa mtu katika hali yoyote ile, kuchagua njia yake mwenyewe."

Kwamba haijalishi ni hali ngumu kiasi gani unapitia bado unao uamuzi wa kufanya

 Katika kipindi hiko aliweza kuja na nadharia mpya kwenye ulimwengu wa saikolojia

Uchunguzi huu ukawa msingi wa nadharia yake ya logotherapy, aina ya tiba ya kisaikolojia inayozingatia nia ya maana yaani "sense of purpose" Hata katika kukabiliana na wakati mgumu Frankl hakuchagua kujisalimisha kwa kukata tamaa. Alizingatia kutafuta maana katika uzoefu wake na Pia alipata njia za kuwasaidia wafungwa wenzake, akiwapa faraja na kuwahimiza wapate sababu zao za kuishi.

*Baada ya mambo kuwa sawa* 

Baada ya kuachiliwa kwake mnamo 1945, Frankl hakuendeshwa na uchungu au chuki. Badala yake, alijitolea maisha yake kuwasaidia wengine kupata maana katika maisha yao, bila kujali hali zao aliandika kitabu *"Man's search for meaning "ambacho kimeelezea nguvu ya uzoefu wake na logotherapy, ambayo am mamilioni ya watu ulimwenguni kote kuwasaidia katika maswala ya afya ya akili 

Maisha ya Frankl yanaonyesha uwezo wa roho ya mtu kushinda mateso na kupata maana ndani yake Alituonyesha wazi kwamba hata katika hali mbaya zaidi, tuna uhuru wa kuchagua mtazamo wetu na kupata kusudi ambalo linaweza kutusaidia.  

Victor Frankl anasema kwamba "When we are no longer able to change a situation, we are challenged to change ourselves"

Tunapokuwa hatuwezi kubadili mambo tunapaswa kujibadili sisi wenyewe

#Raising mentally strong people

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...