Umuhimu wa Magnesium Mwilini
Magnesium ni madini muhimu sana ambayo hufanya kazi zaidi ya 300 mwilini. ina faida zifuatazo kwa mwili
-
Kazi katika Misuli na Neve:
- Husaidia misuli kupumzika na vizuri
- Husaidia kuzuia maumivu ya misuli na misuli kukakamaa.
- husaidia pia kupunguza ukali wa "migraines" "kipanda uso"
- pia husaidia kwa watu wenye shida katika kupata usingizi "insomnia"
- Inasaidia utendaji mzuri wa neva (mishipa ya fahamu) na mapigo ya moyo.
-
Udhibiti wa Sukari ya Damu:
- Husaidia insulin kufanya kazi vizuri mwilini hivyo kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu.
- Inaweza kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari cha aina ya 2.
-
Udhibiti wa Shinikizo la Damu:
- Husaidia mishipa ya damu kupumzika, hivyo husaidia shinikizo la damu la kawaida.
- Inaweza kupunguza hatari ya shinikizo la juu la damu na magonjwa ya moyo.
-
Uzalishwaji wa Nishati:
- Ni muhimu kwa kutengeneza ATP, ambayo ndio nishati kuu inayotumiwa na seli
Afya ya mifupa:
- Ni sehemu muhimu ya mifupa na pia husaidia katika ufyonzwaji wa madini ya calcium, hivyo kuimarisha mifupa na kuzuia ugonjwa wa mifupa ( kama vile osteoporosis).
-
Utengenezaji na ukarabati wa DNA:
- Inahitajika kwa ajili ya kutengeneza na kukarabati DNA na RNA.
-
Kinga ya Mwili (Antioxidant):
- Inasaidia kulinda mwili dhidi ya uharibifu unaosababishwa hasa inasaidia kuzuia uharibifu wa seli
-
Udhibiti wa hisia:
- Inaweza kusaidia kupunguza dalili za wasiwasi "anxienty" na unyogovu ama "depression" kwa kusaidia utendaji wa kemikali za ubongo (neurotransmitters).
Unajuaje kama una upungufu wa magnesium?
Upungufu wa magnesiamu unaweza kusababisha dalili mbalimbali, kama vile:
- Uchovu na udhaifu wa mwili
- Maumivu ya misuli na kukakamaa
- Kichefuchefu na kutapika
- Kukosa hamu ya kula
- Kutetemeka
- Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida
- Kufa ganzi
Kumbuka sio kila dalili hizi zinapojionyesha zinatokana na upungufu wa magnesium sababu inaweza kuwa nyingine kabisa pia upungufu wa muda mrefu unaweza kuongeza hatari ya magonjwa sugu kama vile ugonjwa wa moyo, shinikizo la juu la damu, kisukari cha aina ya 2, na osteoporosis.
Vyanzo vya magnesium kwenye vyakula:
Ili upate magnesiamu ya kutosha, kula vyakula kama:
- Mboga za majani kwa wingi
- Karanga na mbegu (almond, mbegu za maboga, chia seeds)
- Jamii ya kunde (maharagwe, dengu)
- Nafaka nzima (mchele)
ikiwa unaona huipati ya kutosha katika mlo wako unaweza ukatumia virutubisho vyake "supplements"

Join the conversation