Unachoweza Kujifunza Kutoka kwa Watu wa Kwanza Waliofika Ncha ya Kusi(south pole)
Je kuna jambo unajaribu kulifanya ila kila mara unaishia njiani na kukosa muendelezo?
Share na mtu wako wa karibu kama itaweza kumsaidia pia
Mnamo mwaka 1911, timu mbili za wapelelezi zilianza safari ya kufika Ncha ya Kusini. Moja ya timu iliongozwa na Roald Amundsen, ambaye aliweka lengo thabiti kwa timu yake. Timu nyingine iliongozwa na Robert Falcon Scott, ambaye aliruhusu mazingira ya nje na hisia zake kusababisha matokeo mabaya ya safari yake na ya timu yake.
Tofauti ya mbinu zilizotumika
Amundsen aliamua kufuata utaratibu rahisi – kila siku, yeye na timu yake walipaswa kusafiri wastani wa maili 15 za baharini kwa siku.kwa mwendo wa kawaida usiochosha sana, na pia haukuwa rahisi sana pia. Haijalishi hali ya hewa (isipokuwa hali mbaya sana), yeye na timu yake walisafiri si zaidi (na si chini) ya maili 15 hadi 20 za baharini. Muda uliobaki, yeye na timu yake walipumzika ndani ya tent zao za kulalia.
Scott alichagua mbinu ambayo ilimfelisha (labda ndio njia pia ambayo umeichagua ndio maana mambo yanakuwa magumu kila wakati)
Scott, kwa upande mwingine, aliitembeza timu yake hadi kuchoka kipindi cha hali ya hewa ilikuwa nzuri na hakutoka kwenye hema lake wakati hali ya hewa ilikuwa mbaya. Aliamini kwamba juhudi hazina faida hadi ujitesa kabisa.
*Matokeo yake:Nani aliyefika mapema?*
Amundsen na timu yake walifika Ncha ya Kusini kwanza – na walirudi miezi michache baadaye ili kusimulia kisa hicho.Maskini Scott na timu yake walikufa njiani kurudi – wakiwa wameishiwa nguvu kwa safari ngumu zaidi ya kurudi.
Hakuna shaka kwamba wanaume wote walikuwa na uvumilivu. Haikuwa kazi rahisi (na bado si rahisi hadi leo) kufika Ncha ya Kusini kwa miguu. Hata hivyo, ni Amundsen aliyefanikiwa – sababu ya uvumilivu mkakati mzuri na nguvu ya kupumzika vizuri, si kwa sababu ya kujisukuma sana yeye na timu yake kwa nguvu
Itumie mbinu hii kuimarisha afya yako
#Anza kufanya mazoezi anza taratibu usilenge kufanya kwa muda mrefu mwanzoni anza kutembea kwa dakika kadhaa kila siku, kisha utaendelea kuongeza muda kadiri utakavyozoea
#Malengo madogo na yanayoweza kufikiwa hufanya safari ya kuwa ya kuwa mwenye afya iwe rahisi na endelevu kuliko kujaribu kufanya mabadiliko makubwa mara moja.
#Sikiliza mwili wako na pumzika vya kutosha ili kuepuka kuchoka sana na kukata tamaa
#Kama lengo lako ni kula vizuri zaidi unaweza ukaongeza tunda moja katika mlo wako wa kila siku
#Kama lengo lako ni kuimarisha afya yako ya akili jitahidi kuboresha mahusiano ya karibu zaidi (tumia angalau dakika 5 kila siku kuwasiliana na watu wako wa karibu hata mtu mmoja jadili naye mambo mbalimbali )
#Raising healthy generation
Join the conversation