Approval addiction :Chanzo chake ni nini?
Siku yangu ya kwanza nikiwa darasa la pili, nilikwenda shuleni na kugundua kuwa kulikuwa na msichana mpya na mrembo sana darasani—mtu ambaye hakuwepo miaka miwili iliyopita. Jina lake Tumuite Bertha na ndani ya saa moja, alikuwa kila kitu kwangu.
Ukiwa na miaka saba, kiukweli hakuna hatua zozote maalum unazoweza kuchukua inapotokea kwamba umependa mtu. Huelewi hata unachokitaka muda huo kinachokuwepo pale ni hamu tu isiyo na umbo ambayo inakuwa ni sehemu ya maisha yako
Lakini kwangu mimi, ilianza kuwa muhimu ghafla miezi michache baadaye, wakati wa mapumziko siku moja, mmoja wa wasichana darasani alianza kuwauliza kila mvulana, “Unataka kumuoa nani?” Aliponiuliza mimi, haikuwa na ubishi jibu lilikuwa rahisi nilimjibu “Bertha.”
Jibu hilo liliniweka matatizoni
Kuwa kutokana na hali ya kuwa mgeni katika ubinadamu sikugundua kwamba jibu pekee lililokubaliwa kijamii kuhusu unataka kumuoa nani ni "Hakuna"
Mara tu nilipomjibu, yule msichana katili alikimbilia kwa wanafunzi wengine, akimwambia kila mmoja kwa nguvu kwamba “amesema anampenda na anataka kumuoa Bertha!” Kila mtu aliyemwambia alicheka kicheko kisichozuilika. Nilikwisha niliona kama maisha yamekwisha.
Habari hizo zilimfikia Bertha mwenyewe kwa haraka sana, ambaye alikaa mbali nami kadri iwezekanavyo kwa siku kadhaa baadaye.
Hili tukio la kutisha lilinifundisha somo muhimu sana maishani—inaweza kuwa hatari sana kujitambulisha jinsi ulivyo(Uhalisia wako), na unapaswa kuwa mwangalifu sana kijamii kila wakati."
Jambo hili limesomwa kwa miaka mingi iliyopita na kuelezewa vyema na Albert Bandura ambaye alikuwa msaikolojia alieleza namna ambavyo watu hujifunza kutokana na namna ambavyo watu wengine wanafanya mambo
kutokana na hali hiyo wakati mwingine tunajifunza mambo ambayo mwishowe huishia kutudhuru sisi wenyewe
Kipindi cha utoto tunakuwa wazi sana kuhusu kile tunachohitaji lakini kadri tunavyokua tunaanza kupata picha mpya ya namna ambavyo tunapaswa kuishi na kwa mambo mengine inakuwa ni kama uigizaji badala ya kuishi uhalisia au wakati mwingine kuongea mambo ambayo tunapitia inakuwa ni vigumu sababu kuna namna ambavyo tutaonekana wa ajabu
Mafano tunaficha mateso tunayoyapitia kimya kimya na kuogopa kutafuta msaada unapitia kipindi kigumu kihisia lakini unaogopa kusema
Unakuwa mtu wa kusema "ndiyo" huku kiuhalisia ulitaka kusema "hapana"
Unajikuta katika kile ambacho kinaitwa "people pleasing" kutaka kuridhisha kila mtu matokeo yake unajiongezea uoga,stress na unashindwa kujali mahitaji yako ya muhimu
Unajikuta katika jambo lingine ambalo linaitwa "approval addiction" inachochewa zaidi na kile nilichoelezea kuhusu "people pleasing" lakini yenyewe inakuwa imezidi kiasi kwamba kila wakati unajikuta una stress huzuni au uoga mwingi sababu ya kutaka kuridhisha watu wengine au wale waliokuzunguka
Kuna kipindi mambo yanaweza kuwa magumu kwa upande wako na hali hii inaweza kukutaka utulie usitafute msaada ila ni vyema sana kuwa mjasiri na kutafuta msaada au kufanya kile ambacho kitakuweka huru zaidi
Ingekuwa ni rafiki yako anapitia kile ambacho unapitia leo ungemsaidiaje?
Usisahau kujipa nafasi hiyo na wewe pia jijali kama ambavyo ungemjali rafiki yako wa karibu kumbuka rafiki yako wa karibu zaidi ni wewe

Join the conversation