"Déjà vu" :Tayari nimeona ,je ni tatizo la afya ya akili?

Umewahi kuona kama kile ambacho unakiona mbele yako ulishawahi kukiona? na kiuhalisia hukuwahi kukiona? na hukumbuki vizuri labda ulikiona wapi na ilikuwaje? Umewahi kufika mahali ukahisi kwamba ni kama vile ulishawahi kufika ila hukumbuki ilikuwaje (na kiuhalisia hukuwahi kufika hapo) ,umeingia zako eneo fulani ghafla kama wimbi la hisia linakupata na unahisi kwamba ni kama uliwahi kuwa hapo na kiukweli hukuwahi kufika hapo ,huenda umewahi kutana na hisia hizi 

Umekutana na hali inayoitwa "Déjà vu"

Déjà vu  ni neno lenye asili ya kifaransa linalomaanisha kwamba kitu fulani kimeshaonekana/jambo fulani limeshatokea au "Tayari nimeona" ("already seen") 

Dejavu ni hali ya kuhisi kama umewahi kupitia jambo fulani hapo awali ama kabla ya jambo hilo kutokea mara nyingi inatokea unaposafiri kwenda sehemu mpya

Ingawa hisia ya Déjà vu huwatokea watu mbalimbali mara nyingi sio kwamba ni ishara ya tatizo la afya ya akili wakati mwingine inaweza kuhusishwa na masuala ya kiakili (yaani neurological) .Kwa wengi Déjà vu ni hisia isiyo na madhara na haidumu sana ila inapokuwa mara kwa mara au ikiambatana na dalili nyingine kama degedege au maumivu ya kichwa inaweza kuashiria tatizo la kiakili lililofichika kama vile kifafa na hivyo huhitaji uchunguzi wa kiafya zaidi 

Historia yake 

Hisia ya "Déjà vu" inayomaanisha kwamba "Tayari nimeona" ina historia ndefu historia yake inaturudisha miaka mingi sana iliyopita neno ""Déjà vu" lilibuniwa mwishoni mwa karne ya 19 na mtu aliyefahamika kwa jina la Emile Boirac ila hali hii ilionekana miaka mingi hata kabla ya kupewa jina hilo mfano Mt .Agustine mwaka wa 400 AD aliita hali hiyo "Kumbukumbu za uongo" 

Emile Boraic alibuni jina "Déjà vu" mwaka 1879 akilitumia kisayansi kuelezea hisia ya kufahamiana na jambo jipya/geni tangu wakati huo tafiti nyingi zimefanyika ili kufahamu zaidi hisia hizo zinatokana na nini baadhi ya sababu ni kama vile makosa katika kumbukumbu,tatizo la kiakili na mfanano kidogo katika mambo mbalimbali mfano unaweza ukatembelea mkoa mwingine ukaingia katika ukumbi fulani labda kwa kuwa katika ukumbi huo kuna baadhi ya mambo ambayo labda yanafanana na ukumbi mwingine ambao uliwahi kwenda utahisi kama vile ulishawahi kuwepo hapo

Kipindi fulani miaka ya nyuma hali hii ilitupiliwa mbali hasa katika masomo ya saikolojia ilionekana ni kitu fulani cha ajabu "sio cha kisayansi" baadhi ya watu waliofanya tafiti kuhusu hali hii walionekana kiajabu ni kama wanasayansi kufanya tafiti kuhusu uwepo wa mizimu 

Ila ukweli ni kwamba hali hii mara nyingi watu wanapitia japo haina madhara kwa wengi ila kwa baadhi ni kiashiria cha kwamba kuna kitu hakipo sawa 

Lisa na "Déjà vu"

Katika kufuatilia kuhusu hali hii tunakutana na kisa cha kweli cha mwanamke aliyejulikana kwa jina la Lisa ambaye kwa miaka 7 mfululizo alikutana na hali hiyo kwake hisia hizi hazikuwa za kawaida ilitokea mara kwa mara na kwenye maeneo mengi ya maisha yake sio tu sehemu alizotembelea hadi watu hakwenda kutafuta msaada  alinunua vitabu vingi vya saikolojia na philosophy na katika moja ya vitabu hivyo alikutana na maelezo yanayofanana na alichokuwa anakipitia alikutana na sehemu inayoelezea kuhusu "Déjà vu" na ilitaja pia aina ya kifafa na dalili zote alijiona anazo na alipofuatilia hospitali na kupata msaada

Kulingana na tafiti za kisaikolojia alichokuwa anakipitia Lisa kipo sambamba na aina hiyo ya kifafa na cha kushangaza ni kwamba "Déjà vu" inayoambatana na aina hiyo ya kifafa ni inafanana kabisa "Déjà vu" ambayo wengi pia huipitia tofauti ni kwamba walikuta kwamba kwa wagonjwa wa kifafa hali hiyo huendelea kwa muda mrefu 

Sababu ni ngumu kufanya majaribio kuhusu ""Déjà vu" watu wenye aina ya kifafa iitwayo "temporal epilepsy" wao ndio hutumika zaidi ili kuelewa hali hii na inafikiriwa kwamba inahusiana na swala zima la kumbukumbu 

mara nyingi kumbukumbu zinatusaidia kutabiri yanayoweza kutokea mbeleni "Subconcious future prediction" 

na wakati mwingine inatokea hali kinyume na 

 Bado haieleweki ni nini sababu hasa na kwanini hisia hizi zinatokea ila ni moja ya namna ya ajabu ya namna ubongo wako unavyofanya kazi 







 


Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...