Depression inachukia lengo la kusonga mbele
"Kama kukimbia kumenifundisha kitu ni hiki mambo yanabadilika"
Haya ni maneno ya mwandishi wa kitabu hiki. Mbali na kuwa alitoka katika familia ambayo wazazi wake walikuwa walevi, maisha yake ya utu uzima yalighubikwa na vipindi vikali vya huzuni (depression). Mara kwa mara alikutana na mtaalamu wa afya ya akili ili kupata vidonge vya "antidepressants" ili kupambana na huzuni. Kadiri siku zilivyozidi kwenda, dozi iliongezeka, na alitambua wazi kwamba haiji bure; mbali na gharama za dawa, kulikuwa na madhara mengine ya pembeni (side effects). Alijiuliza, "Nifanye nini?"
Huzuni ilimfanya maisha yake yavurugike. Siku zingine alishindwa hata kuamka, na siku zingine hakuweza kuoga. Maisha yake yalivurugika, alikosa mwelekeo, na alitaka sana kutoka katika hali aliyokuwa anapitia.
Mabadiliko yalianzia hapa
Alikutana na tovuti ("website") ambayo ilishauri kitu fulani ambacho aliona anaweza kukifanya. Ilishauri sekunde 60 za kukimbia na sekunde 90 za kutembea. Ilionekana rahisi machoni pake; hata sisi tunaona ni sekunde chache tu hizi. Lakini alipaswa kufanya mzunguko huo kwa jumla ya dakika 20. Alijifunza kwamba hatua ndogo tu za kutembea zinaweza kuleta mabadiliko.
Alikutana na rafiki yake ambaye alikuwa na tabia ya kufanya mazoezi kila mara, na rafiki huyo alimwambia jinsi ambavyo mazoezi yanaweza kuimarisha hali ya kihisia ya mtu ("emotional wellbeing"). Alimuelezea waziwazi faida za mazoezi kwa afya yake. Kipindi cha nyuma, ushauri wowote unaohusiana na mazoezi ulipofika masikioni mwake, alitoa visingizio kama vile, "Nimechoka, kuna baridi, mimi ni mnene sana, itaniharibia magoti yangu, sipendi mazoezi." Lakini kipindi hiki, mtazamo wake ulibadilika, na aliamua kuanza taratibu.
Kama ambavyo wengi wanavyokuwa na mtazamo juu ya mazoezi, alihisi kwamba kukimbia kutamuumiza magoti. Kutokana na hilo, alijiuliza kama kuna namna anaweza kukimbia vizuri ili asipate maumivu hayo. Alitafuta viatu vizuri visivyoumiza na alianza taratibu kutembea na mbwa wake, akikimbia sekunde 60 kisha anatembea sekunde 90. Alianza taratibu, na taratibu alianza kuona mabadiliko. Japo alichoka na kuumia wakati mwingine, alijua kwamba kote kuna maumivu; katika maeneo yote ya maisha kuna maumivu. Siku zote tunachagua maumivu; maumivu hayaepukiki, lakini maumivu yote sio sawa. Yapo yenye faida. Kwa upande wake, kufanya mazoezi kulimuumiza, alichoka, lakini maumivu hayo yalikuwa bora kuliko maumivu anayoyapitia kutokana na huzuni.
Mwandishi anasema, "We repeated this combination two more times to complete week three. Each day I grew stronger." Yaani, walirudia mzunguko wa mazoezi mara mbili zaidi kuikamilisha wiki ya tatu, na alijiona akiwa imara zaidi kila siku.
Kwake pia haikuwa rahisi elewa alichokifanya
Haikuwa rahisi. Mabadiliko aliyoyafanya (ya kuanza kufanya mazoezi) hayakuwa rahisi. Mbali na zoezi lenyewe kuchosha, mara nyingi kunakuwa na uoga wa ndani wa namna watu watakavyokuona. Alikuwa na aibu ya kufanya mazoezi jirani. Alipokuwa akikimbia, alihisi watu wanamcheka. Kichwani mwake, aliona watu walimdhihaki na kumtania, ila kiuhalisia hakukuwa na aliyekuwa anafanya hivyo. Anasema, "“You’re old and fat. People will make fun of you and you’ll die of heart failure.” Most people have these competing voices. Mine are just louder." Alijifunza namna ya kutuliza sauti hizi ambazo zilikuwa zinataka kujaribu kumuondoa katika uamuzi wake mpya. "We went for our little jog. Like the first week, I thought of the people in their houses possibly laughing at me in my oversized T-shirt and spandex bell bottoms with the dog walking beside. But I pushed the thoughts away and continued, challenged, but successful."
Mwandishi anasema, "From decades of facing various phobias, I knew that whatever I ran from would trap me, constricting my world." Alijua toka miaka mingi aliyopambana na hofu mbalimbali, alielewa wazi kwamba chochote unachokiogopa na kukikimbia kitakutega. Aliendelea mbele, na kila siku alishinda hofu zote na kuanza kufanya mazoezi sehemu za wazi ("public places") bila kuogopa watu. Kila mara sauti hizo zilimjia ndani, ila alizikabili vyema.
Japokuwa alifanikiwa kweli katika kufanya mazoezi, bado ilibidi aendelee kupingana na sauti za ndani zilizojaribu kumkatisha tamaa, kama hii hapa: "“Look at you in your ‘workout’ clothes, pretending to exercise. Save yourself the embarrassment and play computer solitaire instead.” Rejecting those voices and working out anyway renewed my sense of self-esteem and accomplishment. I almost enjoyed it, especially once we had finished." Alipokuwa akikimbia nje, alijisemea ndani kwamba "“Look at me jogging in public!”" kila alipopita karibu na nyumba fulani. Aliendelea mbele na kujiunga na vilabu vya wakimbiaji ("jogging clubs"), na hii ilimuongezea motisha zaidi na alizidi kujiamini zaidi.
Kama wengi, naye alikutana na wazo ambalo huwapata wengi pia: kwamba kama anafanya mazoezi, basi anaweza kula chochote anachokitaka. Ila alijifunza kwamba japo kufanya mazoezi ni bora kuliko kutokufanya kabisa, kufanya kwake mazoezi haikuwa kisingizio cha yeye kula chochote kile. Kama anavyosema, "You can't outrun your mouth."
Matokeo yake yalikuwa chanya :Aliweza kupambana na depression
Daktari wake, ambaye ni mtaalamu wa afya ya akili, alishangazwa na mabadiliko. Dalili za huzuni zilipungua, na ilifikia mahali dozi yake ya dawa ilipungua zaidi. Aliona jinsi ambavyo afya yake iliimarika zaidi. Alikuwa anatumia aina 6 za dawa, lakini idadi hiyo ilishuka hadi dawa 3 pekee. Aliendelea kufuatilia vitabu mbalimbali kuhusu namna ya kuimarisha afya yake na kuhusu ulaji. Alikuwa anasoma kitabu kiitwacho "The 4-Hour Body" cha Tim Ferriss. Pia alijiunga na makundi mbalimbali ya wakimbiaji wa marathon. Hali yake iliimarika kila kukicha.
Kweli deression inachukia depression inachukia lengo la kusonga mbele
Kama umejifunza kitu unaweza ukashare na mtu wa karibu

Join the conversation