Mazoezi yalivyomsaidia kupambana na ADHD



Chanzo cha habari hii:Kitabu cha "Brain Energy: A Revolutionary Breakthrough in Understanding Mental Health--and Improving Treatment for Anxiety, Depression, OCD, PTSD, and More 

Chris Palmer MD 


Sarah alikuwa na umri wa miaka kumi na saba nilipokutana naye kwa mara ya kwanza. Alikuwa amegunduliwa na tatizo la ADHD na ulemavu wa kujifunza akiwa darasa la nane, alikuwa akisumbuliwa na wasiwasi na kukosa usingizi kwa muda mrefu kadiri alivyoweza kukumbuka, na alianza kupata hofu za ghafla (panic attacks) akiwa na umri wa miaka kumi na nne. Pia alikuwa amehuzunika "depressed" na na kujiamini kwa kiwango kidogo. Alihangaika shuleni, licha ya kutumia dawa kwa ajili ya ADHD yake, na alikuwa na marafiki wachache. Alikuwa na historia kubwa ya matatizo ya akili katika familia yake, huku mama yake, kaka yake, dada yake, bibi yake, wajomba zake wawili, na shangazi yake wote wakiwa wamegunduliwa na msongo wa mawazo, matatizo ya wasiwasi "anxienty", na  ugonjwa wa bipolar. Hilo halikuashiria matokeo mazuri kwa muda mrefu kwa upande wake. Alikuwa tayari amejaribu dawa nane tofauti, ambazo zilisaidia uwezo wake wa kuzingatia, lakini pia zilikuja na madhara ya pembeni na dalili zinazoendelea. Wakati hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba alikaa kitandani siku nzima. Zaidi ya hayo pia alikuwa na maumivu ya kichwa ya migraine na maumivu ya tumbo ya mara kwa mara.

Aliingia chuo kikuu na alijitahidi kadiri awezavyo, lakini alihangaika sana. Familia yake ilimuwekea matarajio makubwa ,ilitarajia amalize chuo kikuu, na hii ilimsumbua zaidi. Mara nyingi alihisi kwamba hawezi kamwe kufikia matarajio ya watu. Alijaribu dawa zaidi za mfadhaiko/depression (antidepressants), lakini hazikumsaidia.

Mambo yalibadilika alipoamua kuchukua masomo ya Pilates. Alianza kufanya mazoezi mara kwa mara na aligundua kuwa dalili zake nyingi za hisia za wasiwasi zilikuwa zinazidi kuwa bora. Akiwa na umri wa miaka ishirini na tatu, alipata kazi kama mwalimu —sasa alikuwa akifanya mazoezi karibu kila siku kwa muda mrefu kila siku. Hiko ndicho kilichobadilisha mchezo wote kwa upande wake. Alikuja kwenye miadi baada ya takriban miezi miwili  akisema, “Najisikia vizuri sana! Sijawahi kujisikia vizuri hivi katika maisha yangu yote.” Zaidi ya mazoezi, alikuwa amependezwa sana na kuwasaidia wengine kuboresha afya zao, alikuwa amepata marafiki wapya, na sasa alikuwa na mpenzi. Licha ya matarajio ya wazazi wake kwamba amalize chuo kikuu, aliamua kuacha masomo na kuzingatia mazoezi kama kazi yake. Hiyo ilikuwa karibu miaka kumi iliyopita na Sarah anaendelea vizuri hadi leo. Bado anatumia dawa za kuchochea kwa dalili zake za ADHD, lakini aliweza kuacha dawa zingine zote. Baada ya kupunguza matumizi yake polepole, alisema alijisikia vizuri zaidi.

Habari hii ya Sarah inaonyesha nguvu ya mazoezi kama tiba ya kimetaboliki, lakini pia vipengele vya kisaikolojia na kijamii vinavyosaidia  kupata maana na kusudi katika maisha, husaidia kupunguza msongo wa mawazo na kuwa na watu wenye msaada na pia kutokuruhusu matarajio ya wengine kututawala kwani Sisi sote ni tofauti, na tunataka—na tunahitaji—mambo tofauti. Sarah alipata njia yake mwenyewe hata wewe au yule anayehangaika na matatizo hayo anaweza kupata suluhisho 

Kuhusu Dr Chris Palmer

Ni mtaalamu wa afya ya akili toka chuo cha Havard ni moja kati ya waanzilishi wa "metabolic psychiatry" ni mbinu ambayo inazidi kutumika hasa kwa matatizo ya afya ya akili kama vile depression,bipolar disease ikiwa katika kiini kwamba matatizo ya afya ya akili wakati mwingine huja kutokana na shida katika mfumo wa kawaida wa utendaji kazi wa mwili ,ukosefu wa baadhi ya virutubisho,ukosefu wa mazoezi pia matatizo kama vile ukinzani wa insulin yote hayo yanaweza kuongeza hatari ya mtu kupata matatizo ya afya ya akili 

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...