Nature's antidepressant
Sayansi iliyopo nyuma ya kukaa kwenye mazingira asilia
Biophilia ni hali ya kawaida ya binadamu kuunganishwa na kuthamini mazingira na viumbe hai vingine.Kwamba tunavutiwa zaidi na mazingira asilia kutenganishwa na ulimwengu asilia kwa muda mrefu kunaonekana kuwa na athari
Matatizo ya afya ya akili mengi yalionekana zaidi mijini ukilinganisha na vijijini japo upo umuhimu wa kuwepo kwenye mazingira ga asili athari za kisaikolojia za kutengwa na mazingira asilia zilianza kufanyiwa utafiti miaka michache iliyopita
Kundi la watafiti wa chuo cha Essex huko Uingereza waliangalia afya za akili zaidi ya wakazi 5000 kwa jumla ya miaka 3 waliangalia makundi mwili kundi la kwanza ni lile walilohamia kwenda mijini na kundi la pili ni wale waliohamia vijijini walitaka kujua mabadiliko hayo yanaathirije afya zao za akili
Walichokiona ni kwamba kundi la watu waliohamia vijijini walikuwa na viwango vya chini vya depression ukilinganisha na lile kundi la mwanzo ambao walihamia mjini
Shughuli kama vile mazoezi yanaturudisha katika mazingira asilia na kuleta faida zaidi kwa afya ya akili na tafiti zipo wazi pia kwamba upo utofauti mkubwa kati ya mazoezi yanayofanyika ndani (gym kwa mfano) na yale yanayofanyika katika mazingira asilia
Ukiachana tu na kwamba binadamu wanapata athari wanapoachana na mzingira asilia wanyama pia huonyesha dalili za depression wanapoondolewa katika mazingira yao asilia
Isabel Behncke ambaye ni moja kati ya watafiti aliyefatilia athari hii huyu Isabela alifanikiwa kutembea katika misitu ya kongo alitumia muda wake mwingi akiishi na nyani katika msitu huo akiwasoma Isabel anasema *"Ni ngumu sana kwa mnyama anayetembea eneo hili kupata depression"*
Wanyama walioondolewa katika mazingira yao ya asili walionekana na ishara za depression
Miaka ya 1970 huko Michigan ilikuwa kwa bahati mbaya miaka ya 1970 katika moja ya gereza nusu ya wafungwa waliwekwa mahali ambapo waliweza kuona mazingira asilia vitu kama miti na mashamba na nusu ya wengine walifungiwa katika magereza ambapo hawakuona chochote nje matokeo yake ilionekana kwamba wale nusu ya kwanza walikuwa asilimia 24% ya kutokupata matatizo ya afya ya akili
Tafiti zingine zilionyesha kupungua kwa dalili za depression au msongo wa mawazo baada ya kuangalia video yenye mazingira asilia "nature"
Nature🌿🍃 is medicine ila kwa kuwa haiuzwi hakuna anayeitangaza pata muda wa kukaa kwenye nature
Ikiwa ni mwezi wa uelimishaji kuhusu afya ya akili ungependa zaidi kuelewa sababu halisi za depression?
Endelea kutufuatilia zaidi
#Raising healthy generation

Join the conversation