Nini kitatokea ikiwa utakosa mwanga wa jua kwa siku 40 mfululizo?


Siku hizi unatumia masaa mangapi ndani? unatumia muda kiasi gani nje ? 

Fikiria simu yako ndio simu yako hiyo unayotumia sasa hivi ikae bila kuchaji kwa siku 40. ni ngumu, si ndio? kama unabisha jaribu uone Ndivyo ilivyo kwa miili yetu na mwanga wa jua! Jua ni kama "chaja" yetu kuu, inatupatia Vitamini D muhimu sana kwa afya yetu. Lakini nini unafkiri nini hutokea unapoikosa chaja hiyo kwa muda mrefu – labda tuseme  siku 40 mfululizo? Je, kweli mwangaza wa jua ni muhimu kiasi hicho? Katika makala hii ya leo, tutachunguza athari za kukosa mwangaza wa jua kwa muda mrefu na kuelewa ni kwa nini mwanga huu ni muhimu zaidi kuliko unavyoweza kufikiria

 Tafiti zinaonyesha kwamba watu duniani kote wanatumia muda mwingi zaidi ndani na kwa sababu hiyo hawapati mwanga wa jua wa kutosha na hali hiyo inaonekana kutokana na kuwa na idadi ya watu wenye upungufu wa Vitamin D.

Kwahiyo nini kitatokea ikiwa utakosa mwanga wa jua kwa siku 40 mfululizo?

Kukosa mwangaza wa jua kwa muda mrefu, kunaweza kuathiri sana afya ya binadamu, hasa kutokana na upungufu mkubwa wa Vimini D na usumbufu katika ratiba ya kulala na kuamka (circadian rhythms) kwani mwili unategemea jua/mwanga kwaajili ya mzunguko wa kawaida wa kulala na kuamka "circardian rhythm" . Haya ni baadhi ya mambo yanayoweza kutokea:"


Upungufu Mkubwa wa Vitamini D

Mwanga wa jua hasa jua la asubuhi ndiyo chanzo kikuu cha asili cha Vitamini D, ambayo ni muhimu sana kwa kazi nyingi sana mwilini kama vile ufyonzaji wa madini kama vile calcium "kalisiamu" na pia afya ya mifupa. Sasa baada ya siku 40 bila jua, viwango vya Vitamini D vitashuka sana, na kusababisha:

  • Athari Afya ya Mifupa:Vitamin D ni muhimu sana kwa afya ya mifupa viwango vinapokuwa vidogo inasababisha kulainika kwa mifupa,maumivu ya mifupa,na kuongezeka hatari ya kuvunjika mifupa
  • Kinga ya Mwili Kudhoofika: Vitamini D ina  umuhimu sana katika mfumo wa kinga. Upungufu mkubwa unaweza kukufanya uweze kuambukizwa magonjwa kwa urahisi (kama homa, mafua, n.k.) na unaweza kuhusishwa na hatari iliyoongezeka ya magonjwa ya kinga ya mwili (yaani autoimmune diseases, ni yale magojwa ambayo kinga yako ya mwili inageuka na kushambulia mwili wako italelezewa zaidi katika post zijazo endelea kutufuatilia)
  • Hatari Nyingine za Kiafya: Viwango vya chini vya Vitamini D vimehusishwa na hatari kubwa ya magonjwa mbalimbali sugu, kama vile:
    • Baadhi ya saratani (k.m., matiti na utumbo mpana)
    • Magonjwa ya moyo na shinikizo la damu
    • Ugonjwa wa kisukari aina ya 1
    • Magonjwa ya akili (kama Alzheimer's)

Usumbufu wa Ratiba ya Kulala na Hali ya kihisia

 Giza/kukosa mwanga wa jua kwa muda mrefu litasumbua sana ratiba ya asili ya kulala na kuamka Hii inaweza kusababisha:

  • Huzuni na Kubadilika kwa Hisia: Kupungua kwa mwangaza wa jua huathiri viwango vya serotonin (homoni ya "kujisikia vizuri" kwenye ubongo), na kusababisha hisia za huzuni, uchovu, na kukasirika kirahisi.
  • Matatizo ya Kulala: Usumbufu hasa katika uzalishaji wa melatonin (homoni ya usingizi) unaweza kusababisha kukosa usingizi usiku na uchovu wakati wa mchana.
  • Kuongezeka kwa Hamu ya Kula: Unapokosa usingizi hupelekea ongezeko la homoni ya njaa siku inayofuata hasa vyakula vya wanga, ambayo kwa muda mrefu inaweza kusababisha kuongezeka uzito.
  • Ugumu wa Kuzingatia(focus/attention): Uwezo wa kufikiri unaweza kuathirika 

Madhara Mengine Yanayowezekana

  • Uchovu na Upungufu wa Nguvu: Mchanganyiko wa upungufu wa Vitamini D na usingizi uliovurugika unaweza kusababisha uchovu wa kudumu au kile wanachokiita uchovu sugu "chronic fatique" hapa ni pale ambapo unakuwa unapitia uchovu mfululizo kwa muda mrefu

Kwa kifupi, kukosa mwangaza wa jua kunaweza kusababisha athari hizo hapo juu hivyo jitahidi kupata mwanga wa jua hasa la asubuhi kupata faida zake kwani kadri siku zinavyozidi kwenda muda unaotumika nje unazidi kupungua na wengi hawapati viwango vya kutosha 

Je una maoni au kuna kitu ungependa kielezewa ukielewe ? basi usisite kutuambia kupitia chanel yetu

Tunakutakia afya njema ,pamoja kujenga watu wenye afya njema kila siku 

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...